Roberto Carlos ayatimba kwa mkewe, huenda akafirisika kisa kesi ya talaka

Roberto Carlos ayatimba kwa mkewe, huenda akafirisika kisa kesi ya talaka

Kama wewe ni tajiri, maarufu na wala sio mcha Mungu unaoa kwa ajili gani?
Sisi wengine ambao tuna pambana na maisha na tuna mcha Mungu ( hatutaki kuzini) lazima tuoe.
Mimi maisha yangu yame improve sana baada ya kuoa.
Lazima ya improve, Kwa ushauri wake ili baadae aje kukunyonyoa. Ni kama anapalilia kibubu chake.

Wanawake wengi atakupa ushauri mzuri tu lakini huwa wanawaza vitu viwili 1. Huyu jamaa aki danja ananiachia nini? 2. Huyu Mwamba akinitema au nikimchoka naondokaje?

Hiyo namba Moja inawezakuwa Kwa mapenzi ya Mola au Yake (refer Machame widows)
 
Mtatoa povu hapa bure hizo mali zimewakuta ndani ya ndoa huyo Ronaldo hata asipooa anamlipa georgina $85,000 kwa mwezi. Halafu hata hizo mali wengi wao wanawapa hao wake zao ili family iendelee ku stick together.
 
Ndoa ni mkataba (mradi tata) wa kitapeli ulio buniwa na kurahimishwa na mamlaka za kiserikali bila kumshirikisha mwanaume, kwahiyo mwanamke na mamlaka za kiserikali hawa wote wanajuana ni matapeli walio ungana kumpiga vita mwanaume. Ndoa ni vurugu, ndoa ni vita, ndoa ni adui wa mwanaume. Kataa ndoa
 
🤣🤣😂😂😂Bado nasubiria ifike mbali kidogo kuepuka masuala ya kusubiria next episode
nacheka Sana, bado niko holiday so Kuna group la Wana k drama .

yaani reaction zao zina nifanya nicheke mno, eti Wana muonea Jamaa.
 
Roberto Carlos, beki maarufu wa zamani Real Madrid, anaripotiwa kuishi katika uwanja wa mazoezi wa klabu ya, Real Madrid Sports City huko Valdebebas, huku akipitia talaka ya juu kutoka kwa mke wake wa miaka 15, Mariana Luccon.

Wawili hao, waliofunga ndoa mwaka 2009, kwa sasa wako kwenye vita vya kisheria kuhusu utajiri wa Carlos, ambao unakadiriwa kufikia pauni milioni 133, kulingana na ripoti kutoka Goal. Wakati nyota huyo wa Brazil amechukua makazi kwa muda kwenye uwanja wa mazoezi, mke wake wa zamani anasalia katika nyumba yao kuu, na wazazi wake wanakaa katika mali nyingine inayomilikiwa na Carlos. Wenzi hao wa zamani wana mabinti wawili, Manuela na Mariana.

Carlos, ambaye ali ichezea Real Madrid kwa zaidi ya muongo mmoja, anajivunia maisha mazuri, baada ya kushinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa na mataji manne ya La Liga. Zaidi ya soka, maisha yake ya kibinafsi pia yamevutia, kwani amekiri hadharani kuzaa watoto 11 na wanawake saba katika nchi tofauti.

Huku taratibu za kisheria kuhusu mgawanyo wa mali ukiendelea, bado haijulikani ni muda gani Carlos atakaa katika kituo cha mafunzo au matokeo ya mwisho ya kesi hiyo yatakuwaje. Mbali na mafanikio yake ya zamani uwanjani, sasa anatumika kama balozi wa Real Madrid.

Fununu zina sema "mwanamke ndie aliye msaliti r. Carlos" na alipo ulizwa kwanini kafanya hivyo .yeye kakimbilia talaka.

ushauri tu,
ikiwa wewe ni maarufu na umepata pesa, hakuna haja ya kuoa. Ndoa daima huisha kwa talaka. Kuwa kama Christiano Ronaldo.

KATAA NDOA LINDA UHURU WAKO, KATAA NDOA LINDA UCHUMI WAKO.
KATAA NDOA LINDA JUHUDI ZAKO.
NDOA NI MKATABA WA KITAPELI.
View attachment 3196441
kibongo bongo kuwa kama Mond plutinumz
 
Muheshimiwa Ashraf Hakimi alishatufundisha namna ya kumshinda shetani bila kutumia nguvu nyingi ile mbinu yake ni bora zaidi dhidi ya mshetani
 
Huo ni uoga mara kataa ndoa mara oa Mwanamke mwenye kazi yake sitaki goolkeeper mara usioe mara kataa single mom mara kataa vitoto vya 2000 mara warangi hawafai mara wazigua mara wanyakyusa Wana vile mara sekta ya afya hawafai mara wa singida Kaa mbali nao mara mara mara mara maneno meeeengi, wewe kama ni mwanaume SEMA Mimi sitaki Mwanamke tujue wewe ni mwanaume kweli, Bali mwanaume wa kweli ni huyu Anapenda kweli, anaoa, anamtunza mke wake na familia yake, anapambana na kumaliza changamoto zinazojitokeza, na akimalizana na mke wake mume hubaki mshindi kwa kuwa hakutenda uonevu dhidi ya mke wake, anatafuta mke mwingine maisha yanasonga, Ewe kataa ndoa usikatae ndoa tu Bali kama unaweza kataa wanawake tujue kweli wewe ni mwanaume. Na Raha ya Dunia ni wanawake hawatakosa changamoto wapende na malizana nao kiungwana kabisa.
 
The key point ni nini summarize
 
Back
Top Bottom