Roberto Carlos: Badala ya kumkaba Ronaldinho Gaucho nilicheka Kwa kukumbuka chenga alilompiga Gattuso

Mleta mada ni mke halali wa wabrazil thread zake zote kawasifia kinoma

Jamaa ana mahaba na wabrazil sijui walimfanyia kitu gani aise 😀😀😀 wabongo bana tunapenda kujishusha hadhi
 
Neymar games 26 PSG goals 26

Gaucho games 98 goals 25

Who is the best?

Au mnapenda anavyokenua?
Afu kumbuka kipindi hichi hakuna wachezaji wenye talent za kutosha ndiyo maana unaona watu kama Messi na Ronaldo wanaishia kubadilishana tuzo kila mwaka. Kipindi cha kina Dinho hata beki unaweza kushangaa kabeba tuzo ya mchezaji bora. Sio saa hvi unakuta Messi anajua kabisa hasiposhinda yeye basi lazima Ronaldo achukue
 
Mleta mada ni mke halali wa wabrazil thread zake zote kawasifia kinoma
Mkuu umefika mbali kutokana na lugha isiyo njema. Vinginevyo wabrazil wanasifika kutokana na "ball dance" wanayoonyesha ndani ya dimba, ambayo inatufanya tuburudike
 
Acheni kutokwa mapovu hizi ni zama nyingine tofauti na zile zama zile za mastaa wengi kina dingo,delima,figo,zizu na wengineo mnafananishaje na zama hizi za wanyoa viduku waliojaa ubishoo?hakuna soka wenye soka lao walishasepa nalo saiv kinachowabeba wachezaji wengi ni matangazo
 
Ronaldinho ni mchezaji mzuri wa aina yake hajawahi kutokea mchezaji kama Ronaldinho na hatakuja kutokea.

Tungeweza kumuhesabu kama mchezaji bora wa mda wote kwenye karne hii,Ila Ronaldinho kwenye hilo ana tatizo moja tu nalo ni Lionel Messi.
 
Pale barca Dinho haina kachukua UCL mara 2, Brazil kachukua world cup
Sasa huyo mnyoa viduku wako mimi sijui kachukua nini?
Nimekusoma vibaya ama ndiyo ukweli wenyewe? Dinho kachukua UCL 2? Siyo moja kweli (2006) maana ile ya mwaka 2009 alikuwa ameshaenda AC Milani.
 
Barca isingeweza kumwachia mchezaji muhimu hata siku moja, ni Wa kawaida ndo maana wakamwacha aende PSG.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…