nilifanikiwa kuingia shamba na kulima na kupanda ekari kadhaa za mazao ya chakula na biashara na nikafanikiwa kupalilia vema. Namshukuru Mungu, kwa neema na baraka zake natarajia kuvuna hivu karibuni
mengine katika mipango na matarajio yangu kwa mwaka huu mpya2024, mathalani ya ufugaji na siasa, kwa kiasi kikubwa yanasogea taratibu na kusonga mbele vizuri. Naimani kwa bidii, maarifa na kwa kuto kukata tamaa kwangu, Mungu ataendelea kunifadhili na kunikirimia zawadi hii muhimu sana ya uhai na afya njema, alizonipa bure, ili hatimae niweze kuyafikia na kutimiza yote mema niliyopanga na kuyatarajia kwa mwaka huu, sawa sawa na mapenzi yake Mungu