Roho inaniuma sana, mabati niliyoezekea nyumba yangu yamepauka sana

Sawa mkuu au kwa mama wahenga nako nasikia ipo
Sina uhakika na uaminifu wake,maana pana watu wao uangalia pesa ya leo na sio kujenga uaminifu.Kwann.Kwa dar bora uende kiwandani Alaf unapeleka vipimo vyake wanakukatia kulingana na vipimo vya mchoro wa nyumba yako hii inaepusha mambo ya kukata hovyo bati
 
Kuna bati za migongo mipana zimeezekwa madarasa pale same secondary lile darasa limejengwa mwaka 1970 uko hadi leo bado kama limepigwa jana...haya mabati nadhani yanagrades zake na nna uhakika wengi hatuwezi kumudu bei kwa Mali safi...tunapenda vitu ambavyo havina ubora just bcoz zinafanana na vyenye ubora
 
Sio kila kitu chenye bei kubwa ni kizuri au kila kitu chenye bei ndogo ni hafifu.
Kuna watu wametumia Alaf Original kutoka kiwandani bati zimepauka.
 
Sio kila kitu chenye bei kubwa ni kizuri au kila kitu chenye bei ndogo ni hafifu.
Kuna watu wametumia Alaf Original kutoka kiwandani bati zimepauka.
Kwahyo unaona alaf pekee ndio bati bora?watu wanaagiza mabati nje na vifaa vingine ya ujenzi .ni pesa yako tu
 
Umepigwa maturu
 
Hivi ni kitu gani huwa kinawafanya watu wawe wavivu kwenda Kiwandani ukapewa mzigo wako wenye kueleweka! Unapenda buguruni/tazara unategemea kupata bati original kweli? Pale ni full fake.
 
Mkuu kupaka rangi upya utaongeza stres hazishiki rangi
 
Hii ndio bati ya ALAF original....alama zake katikati ya mgongo moja na mwingne kuna njia tatu namaaisha migongo midogo mitatu.....hakuna kampuni yeyote ipo hvyo...kingine muhuri wa moto nyuma ya bati kingine muhuri wa kugonga ambao umeandikwa ALAF
 
Relax bro hiyo ipo kwa wote
Niliezeka bati upande umepauka na upande mwingine zipo vile vile,nyumba ipo kama ina aina 2 za bati,ila nilinunua sehemu moja,duka moja bei moja...ila ukiangalia kwa jirani bati zipo poa tu
Ilimradi sinyeshewi haina shida
Na wewe.walikuchanhanyia na feki
 
Mimi nilienda kiwandani pale ALAF....nilipo fika wakanishauri kuwa kiwandani tunapokea oda then ndio wanatengenea kwa mteja....pia mpaka kuja kupata zitachelewa pia bei ya kiwandani pale ALAF ni kubwa kuliko kwa mawakala wao....wakaniambia ukitaka kusubir subir lipia oda lakini kama unataka nenda kwa mawakala wetu....wakanitajia mawakala wao...na namba zao za simu....pia wakanipa namna ya kutambua bati ya ALAF....na wakaniambia kama ikipauka njoo kiwandani utoe taarifa....
Nikauliza kwanini bei ya kiwandani ni kubwa kuliko kwa wakala wenu...wakanijibu kuwa wakala wanampa punguzo la 10% ya kila bati kama bati kiwandani sh 39900 bhas wakala ananunua kwa 39900-10%=35910....kwa hyo wakala ndio anajipangia bei yake wengine watauza 38000 na 37500....hyo ndio taarifa....kwa hyo kwa bati ya Alaf bora ununue kwa wakala utapata bei rahisi....nenda kwa wakala ambaye ni legit(halali)..au nenda kiwandani kuchukua namba tu na kupata elimu ya utambuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…