ROHO NI NINI
Hii ni miongoni mwa elimu ngumu sana katika kutolea maelezo. Lakini nitajotahidi kadiri nijuavyo lakini ajuaye zaidi ni Mungu.
Roho ya mtu huumbika (nurtured) sambamba na kuumbika kwa mwili wa mtu anapokuwa tumboni mwa mama yake yaani kama inavyojulikana mtu hadi awe kiumbe kamili huanza kutoka kwa baba kama tone la shahawa (sperms) ambapo katika shahawa moja ndipo hutokea mtu mmoja (naomba tusahau juu ya mapacha ili tuelewe kwa urahisi), hivyo roho huwemo ndani ya shahawa katika hali ya udhaifu (delicate and elusive) na wakati shahawa inapoingia kwenye ovary ya mwanamke ili irutubishwe kuwa kiumbe kamili hapo hapo pia roho iliyomo ndani ya shahawa nayo inarutubika sambamba na shahawa yenyewe pindi shahawa inapokuwa kiumbe kamili nayo roho inakuwa kamili na uhai unakuwa umekamilika, hivyo roho inaanzia kuwemo ndani ya shahawa na hukuzwa ndani ya tumbo la mama sambamba na kukuzwa kwa mwili mzima wa mtoto ndani ya tumbo la mama.
Basi ili tuweze kuifahamu roho inatupasa tutoe mifano ya vitu tunavyoishi navyo, Roho siyo sehemu ya mwili kama vile jicho au mkono au sikio nk, yalivyokuwa ni sehemu ya mwili lakini roho inayo mahusiano ya kiathari (cause and effect) na mwili mfano kama mtu atukanwe vibaya hapo moja kwa moja atapata maumivu katika roho na anaweza kutoka machozi kwa uchungu na utaona hayo machozi ni dalili kuwa mwili umepata athari halikadhalika kama mtu apewe mateso makali ya mwili athari itaenda kwenye roho kiasi kwamba mwili unakuwa si mahali pazuri kwa roho kukaa na hivyo roho huondoka na hatua hiyo tunaiita kifo, pia mtu anapofanya Ibada kwa vitendo (kimwili) anaipa athari za kiibada hiyo roho yake.
Kifupi ni kwamba roho imejificha ndani ya mwili kama vile moto ulivyojificha ndani ya njiti ya kiberiti, njiti ni njiti na moto ni moto wala havifanani lakini vinahusiana.