ROHO ni nini?

ROHO ni nini?

Roho ni kitu katika maisha ya mwanadamu ambacho kinampa uwezo wa kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu.

Popote neno “roho” limetumika, linaashiria sehemu ya ndani ya mwanadamu ambayo “yakutanika” na Mungu, ambaye Yeya mwenyewe ni Roho (Yohana 4:24).
 
Hata saivi nawaza Roho ni kitu kisichoonekana ila tunakihisi uwepo wake wengine hudhani roho ni moyo
Hawajui...ila Roho ni sehemu ya ndani ya mwanadamu inayokutanika na Mungu Yohana 4: 24
 
Hawajui...ila Roho ni sehemu ya ndani ya mwanadamu inayokutanika na Mungu Yohana 4: 24
Roho ni kitu katika maisha ya mwanadamu ambacho kinampa uwezo wa kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu.


Popote neno “roho” limetumika, linaashiria sehemu ya ndani ya mwanadamu ambayo “yakutanika” na Mungu, ambaye Yeya mwenyewe ni Roho (Yohana 4:24).
 
salam wan jf
kwa wenye uwezo wa kureason naomba kupewa maana halisi ya neno roho na inamuingiliano gani na akili?
na je viumbe vyote vina roho??
Roho ni mjumiiko wa imani ya moyo,akili na mawazo katika mtizamo.
 
baadhi ya wachungaji wanamfafanua binadamu katika sehemu tatu, mwili(FLESH), nafsi au soul, roho(spirit or ghost)
Mwili ndo hii minyama na kazi yake ni kuwezesha roho na nafsi ziweze kuishi (adapt)hapa duniani na ndio unaotuwekea mipaka tusiweze kuona au kuwasiliana directly na ulimwengu wa roho ambao wenyewe haufungi na muda au umbali,ukitoka katika mwili (ukifa) ndipo nafsi na roho zinapoingia katika ulimwengu wa roho.
Nafsi ni kama soft ware iliopo katika mwili ambao pia naufananisha na hardware, utendaji kazi wa nafsi ndio unaodhirisha ubora wa myu hasa, vitu kama hisia(huzuni, furaha, upendo, tamaa, kiburi n.k) ni matunda ya jinsi nafsi ya mtu inavyofanya kazi, nafsi inakua updated na roho.
Roho ndio enegry au powa ya kufanya mwili na nafsi zifanye kazi, KUNA ROHO NZURI NA ROHO NZURI(HOLLY)-TAKATIFU NA ROHO MBAYA(EVIL) matendo yetu ya nafsi na mwili yanategemea tuko kwenye infuence ya roho ipi.
 
salam wan jf
kwa wenye uwezo wa kureason naomba kupewa maana halisi ya neno roho na inamuingiliano gani na akili?
na je viumbe vyote vina roho??
Tuanzie hapo kwenye neno "viumbe" kwa maana nyingine mada yako inatakiwa kujadiliwa kiimani kwani unapozungumzia "viumbe" maana yake kuna "muumba" aliyeviumba ambaye kwa neno la jumla wanamwita Mungu. Kabla hatujaenda mbele, chagua mada yako ijadiliwe kwa imani ipi maana kuna imani nyingi kila moja ikiwa na mtazamo tofauti kuhusu "roho".
 
Cc Donatila
Cc Demiss
Naona mnagoogle definition za roho na quotes za bible..mnatupanga hapa kwamba mpo deep spiritually...
Hakuna aliyesema yupo deep spirutually...
 
ROHO ni kiumbe kisichoonekana alichokiweka Muumba kwenye mwili wa kila kiumbe ili uweze kuishi
 
ROHO NI NINI


Basi ili tuweze kuifahamu roho inatupasa tutoe mifano ya vitu tunavyoishi navyo, Roho siyo sehemu ya mwili kama vile jicho au mkono au sikio nk, yalivyokuwa ni sehemu ya mwili lakini roho inayo mahusiano ya kiathari (cause and effect) na mwili mfano kama mtu atukanwe vibaya hapo moja kwa moja atapata maumivu katika roho na anaweza kutoka machozi kwa uchungu na utaona hayo machozi ni dalili kuwa mwili umepata athari halikadhalika kama mtu apewe mateso makali ya mwili athari itaenda kwenye roho kiasi kwamba mwili unakuwa si mahali pazuri kwa roho kukaa na hivyo roho huondoka na hatua hiyo tunaiita kifo, pia mtu anapofanya Ibada kwa vitendo (kimwili) anaipa athari za kiibada hiyo roho yake.

.
Nimekuelewa .... sasa niambie roho ikiondoka inarudi tena ktk shahawa na kuendelea na maisha? Je hii ndio inaelekea kwenye life after death? Kwa maana hii roho zinazunguka tu katika miili milele na milele. Je inaweza pia hii roho ikaingia katika mnyama au lazima iingie kwa binadamu tu?
Nilipokuwa uhindini kuna mhindi mmoja alinionyehsa life circle kuwa leo unakuwa binadamu, ukifa unakuwa chui, mara nyoka na maisha yanaendelea hivyo milele... niliona ananichanganya tu nikaacha kabisa kuchunguza haya mambo.
 
Kifupi Roho ni (SPIRIT) ambayo kila kiumbe aliye Hai anayo.
Roho (spirit) ni muungano wa NAFSI (SOUL) NA Akili (MIND).

Ndo kusema combination ya NAFSI (SOUL) na AKILI (MIND) ndo inaleta kitu kiitwacho SPIRIT (ROHO) ya mtu.

Roho (SPIRIT) huwa haionekani. Roho ni structure nzima (muundo) wa mtu. Roho ndo inafanya NAFSI (SOUL) na MIND (Akili) vifanye kazi. Ikiwemo mifumo yote ya mwili wa binadamu. Ndo mana roho (SPIRIT) ikishatolewa na Muumba linalobaki ni li MWILI tu.
Roho Aina umri. Haimanishi mtoto akiwa na miaka miwili basi roho yake pia ina ukubwa wa miaka miwili lahasha!.. Roho inayowekwa kwa mtoto mdogo anaezaliwa ndo hiyo hiyo ataishi nayo mpaka uzeeni. Ndo kusema mtoto mdogo wa miaka miwili Ana ROHO yenye kutambua mambo mengi makubwa Sema tu MUNGU mwenyewe kwa kupitia kanuni na Sheria Zake za Milele (Eternal Laws) huwa anakataza watoto wadogo na wachanga kutumia uwezo mkuu wa ROHO walizo nazo kipind cha udogo wao.
Ndo. Maana utakuta wakati mwingine mtoto mdogo Ana fanya vitu vikubwa vya kushangaza watu. Na tunamuita MTOTO WA AJABU au EXTRA ORDINARY ni kwa sababu tu MUNGU kamruhusu kidogo atumie uwezo mkubwa wa ROHO ulio ndani yake. So kifupi ROHO haina umri. Wala haikua na urefu au unene au umri wa kutoka utotoni mpaka ukubwani.
Eti mwenye miaka 96 roho yake ni kubwa sana kushinda mwenye miaka 12 hakuna kitu kama hiko. ROHO ni ile Ile uliyowekewa mwanzoni na MUNGU.

Viumbe vyote Hai vina ROHO ikiwemo majani, maji, ardhi, miti, wanyama, selihai za miili yetu ambazo zinatengeneza organ za maumbile yetu. Maji na kadhalika.

Roho ni highest intelligence ya kiumbe Hai, ndio inayo control Nafsi (soul) na mind (akili).

KWA wale wana fizikia wanaweza kuelewa mfano huu katika kutofautisha Roho (spirit), Nafsi (soul) na Akili (mind).

Atom si tunaijua? Ina kuwa formed na vitu vidogo ndani yake kama Proton, neutron.

Hivyo hivyo kwa roho (spirit) ni Ile the smallest particle.. Injini ya soul na mind.

MUNGU ndie incharge wa ROHO, MUNGU hakuziumba (create), ROHO Bali anajua namna yake yeye alivyozileta kwenye existence. Literatures nyingi wanasema MUNGU aliziamrisha ziwepo zikatokea.
Maana kitu chochote kinachokua "created" kuumbwa huwa kinakufa.
Roho haijaumbwa na ndo mana roho haifi hata mtu akifa yenyewe inaelekea kwenye ulimwengu wa roho kusubiria hatua zingine.

MUNGU wakati anaanza mpango wa kuandaa Dunia kwa ajili ya maisha ya binadamu. Alitumia roho (intelligences) kwenye kutoa majukumu na roho zingine (intelligences) walikubali KUSHIRIKI kwenye uumbaji wa MUNGU wawe kama majani, wengine walichagua kuwa miti, wengine kuwa maji na wengine kuchukua nafasi mbali mbali ili kuipendezesha Dunia.

Kifupi ni kusema kwamba vitu vyote vilivyo Duniani vinavyopendezesha Dunia ni roho (intelligences) ambazo zimechagua hiyo kazi mwanzoni kabisa kule kwenye uumbaji wa MUNGU.

Intelligences wengine tulichagua kuwa binadamu, ndo mana tukaja kuzaliwa na kuwa na Roho (SPIRIT).

Kumbuka neno Intelligence hapa limetumika Sawa na neno Spirit yote yanamanisha ni ROHO.
Lakini intelligence ni kubwa na ina uwezo zaidi.

Ndo mana Kuna mambo mengi sana yamejitokeza kwenye vitabu vyetu vitakatifu ambayo wengine hawajui kwa undani kwa nn yametokea, wao wanajua ni muujiza tu hapana. Ngoja nikufahamishe!!

YESU KRISTO ndo mkuu wa Roho zote, amepewa mamlaka hayo na MUNGU, Na kama tulivyoongea Mwanzoni kwamba hizi Roho (spirit) zote zinatoka MBINGUNI na zimechagua nafaid zao kwenye uumbaji wa Dunia kama intelligences.

Hivyo intelligences zote, AU kwa lugha rahisi roho zote zilizo kwenye Viumbe hai kama majani, maji, ardhi na nyingi ambazo nimezitaja ZINAMTAMBUA pasipo na shaka UKUU wa YESU KRISTO,.

YESU KRISTO ndo top. Yeye ndo Mkuu wa intelligences zote, roho zote yeye ndo anaongoza.

Hivyo wanamtambua kwa UKUU huo. Angalia kidogo kwenye BIBLIA takatifu YESU akiziamrisha hizi Roho ambazo zilichagua kuwa vitu hapa Duniani na ZIKAMTII.. mfano aliuambia upepo ukome wakati bahari ilipochafuka. Na upepo ukamtii ukatulia kimya Ile sio muujiza kwake yeye anajua kabisa wale walikua roho waliochagua kuwa upepo (intelligences) na akawaamuru watulie.
Pia Kuna sehemu kwenye BIBLIA aliwahi kusema "kama msiponisifu basi NTAYAINUA" mawe haya yanisifu. Alijua dhahiri kuhusu intelligences walio kwenye mawe na uwezo wao wa kuongea na sifa za kiumbe hai, sisi binadamu tunaamini mawe hayana uhai lakini mawe yana uhai na yanaweza kuongea sababu Kuna intelligences ambao walichagua kuwa mawe. Ndo mana YESU akasema NTAYAINUA" kwa lugha rahisi NITAYAAMURU haya mawe.

Pia Kuna mfano mwingine kwenye kitabu hiko Hiko cha BIBLIA AMBAPO YESU alikua Ana njaa akaona mti, akadhani Kuna matunda ili ale lakini hakukuwepo na matunda na kilichofata YESU akaulaani Ule mti.. Na BIBLIA INASEMA ukanyauka hapo hapo ni concept huyo hiyo ya UTII wa intelligence (roho) za Viumbe wengine ambao walichagua kuwa vitu hapa Duniani.

Waislam Kuna mafundisho huwa wanasema Kuna siku mkono wako utaongea na kusema mabaya yote, Kuna siku ulimi au Macho utatoa ushuhuda wa dhambi zako ni kweli kabisa. Hii ni kutokana na concept hii hii ya intelligences ambao wametumika kuumba huo mkono, AU jicho lako au Aina organi nyingine mwilini mwako.

Hata kwenyewe BIBLIA tunaona Ile story ya sauli na farasi AMBAPO punda aliongea na kuwasiliana na sauli, pale sauli alipokua anamfosi punda atembee ili akaue watu wa MUNGU punda alisema 'huoni Malaika mbele hapo njiani ". Ni Ile Ile muendelezo wa concept ya INTELLIGENCES ambao wamechagua kuwa PUNDA na wanyama wengine wakipewa ruhusa ya kuongea wa naongea.

MWISHO, Intelligences ndio yenye uwezo mkubwa sana, ndio inayokua ndani ya roho (spirit). Ndo mana wakati mwingine ni ngumu kutofautisha Kati ya intelligences na roho (spirit) sababu ziko ndani ya mwingine.

Na Roho (Spirit) ni muungano wa NAFSI (soul) na Akili (mind).

Nadhani nimeeleweka.
 
Back
Top Bottom