Kifupi Roho ni (SPIRIT) ambayo kila kiumbe aliye Hai anayo.
Roho (spirit) ni muungano wa NAFSI (SOUL) NA Akili (MIND).
Ndo kusema combination ya NAFSI (SOUL) na AKILI (MIND) ndo inaleta kitu kiitwacho SPIRIT (ROHO) ya mtu.
Roho (SPIRIT) huwa haionekani. Roho ni structure nzima (muundo) wa mtu. Roho ndo inafanya NAFSI (SOUL) na MIND (Akili) vifanye kazi. Ikiwemo mifumo yote ya mwili wa binadamu. Ndo mana roho (SPIRIT) ikishatolewa na Muumba linalobaki ni li MWILI tu.
Roho Aina umri. Haimanishi mtoto akiwa na miaka miwili basi roho yake pia ina ukubwa wa miaka miwili lahasha!.. Roho inayowekwa kwa mtoto mdogo anaezaliwa ndo hiyo hiyo ataishi nayo mpaka uzeeni. Ndo kusema mtoto mdogo wa miaka miwili Ana ROHO yenye kutambua mambo mengi makubwa Sema tu MUNGU mwenyewe kwa kupitia kanuni na Sheria Zake za Milele (Eternal Laws) huwa anakataza watoto wadogo na wachanga kutumia uwezo mkuu wa ROHO walizo nazo kipind cha udogo wao.
Ndo. Maana utakuta wakati mwingine mtoto mdogo Ana fanya vitu vikubwa vya kushangaza watu. Na tunamuita MTOTO WA AJABU au EXTRA ORDINARY ni kwa sababu tu MUNGU kamruhusu kidogo atumie uwezo mkubwa wa ROHO ulio ndani yake. So kifupi ROHO haina umri. Wala haikua na urefu au unene au umri wa kutoka utotoni mpaka ukubwani.
Eti mwenye miaka 96 roho yake ni kubwa sana kushinda mwenye miaka 12 hakuna kitu kama hiko. ROHO ni ile Ile uliyowekewa mwanzoni na MUNGU.
Viumbe vyote Hai vina ROHO ikiwemo majani, maji, ardhi, miti, wanyama, selihai za miili yetu ambazo zinatengeneza organ za maumbile yetu. Maji na kadhalika.
Roho ni highest intelligence ya kiumbe Hai, ndio inayo control Nafsi (soul) na mind (akili).
KWA wale wana fizikia wanaweza kuelewa mfano huu katika kutofautisha Roho (spirit), Nafsi (soul) na Akili (mind).
Atom si tunaijua? Ina kuwa formed na vitu vidogo ndani yake kama Proton, neutron.
Hivyo hivyo kwa roho (spirit) ni Ile the smallest particle.. Injini ya soul na mind.
MUNGU ndie incharge wa ROHO, MUNGU hakuziumba (create), ROHO Bali anajua namna yake yeye alivyozileta kwenye existence. Literatures nyingi wanasema MUNGU aliziamrisha ziwepo zikatokea.
Maana kitu chochote kinachokua "created" kuumbwa huwa kinakufa.
Roho haijaumbwa na ndo mana roho haifi hata mtu akifa yenyewe inaelekea kwenye ulimwengu wa roho kusubiria hatua zingine.
MUNGU wakati anaanza mpango wa kuandaa Dunia kwa ajili ya maisha ya binadamu. Alitumia roho (intelligences) kwenye kutoa majukumu na roho zingine (intelligences) walikubali KUSHIRIKI kwenye uumbaji wa MUNGU wawe kama majani, wengine walichagua kuwa miti, wengine kuwa maji na wengine kuchukua nafasi mbali mbali ili kuipendezesha Dunia.
Kifupi ni kusema kwamba vitu vyote vilivyo Duniani vinavyopendezesha Dunia ni roho (intelligences) ambazo zimechagua hiyo kazi mwanzoni kabisa kule kwenye uumbaji wa MUNGU.
Intelligences wengine tulichagua kuwa binadamu, ndo mana tukaja kuzaliwa na kuwa na Roho (SPIRIT).
Kumbuka neno Intelligence hapa limetumika Sawa na neno Spirit yote yanamanisha ni ROHO.
Lakini intelligence ni kubwa na ina uwezo zaidi.
Ndo mana Kuna mambo mengi sana yamejitokeza kwenye vitabu vyetu vitakatifu ambayo wengine hawajui kwa undani kwa nn yametokea, wao wanajua ni muujiza tu hapana. Ngoja nikufahamishe!!
YESU KRISTO ndo mkuu wa Roho zote, amepewa mamlaka hayo na MUNGU, Na kama tulivyoongea Mwanzoni kwamba hizi Roho (spirit) zote zinatoka MBINGUNI na zimechagua nafaid zao kwenye uumbaji wa Dunia kama intelligences.
Hivyo intelligences zote, AU kwa lugha rahisi roho zote zilizo kwenye Viumbe hai kama majani, maji, ardhi na nyingi ambazo nimezitaja ZINAMTAMBUA pasipo na shaka UKUU wa YESU KRISTO,.
YESU KRISTO ndo top. Yeye ndo Mkuu wa intelligences zote, roho zote yeye ndo anaongoza.
Hivyo wanamtambua kwa UKUU huo. Angalia kidogo kwenye BIBLIA takatifu YESU akiziamrisha hizi Roho ambazo zilichagua kuwa vitu hapa Duniani na ZIKAMTII.. mfano aliuambia upepo ukome wakati bahari ilipochafuka. Na upepo ukamtii ukatulia kimya Ile sio muujiza kwake yeye anajua kabisa wale walikua roho waliochagua kuwa upepo (intelligences) na akawaamuru watulie.
Pia Kuna sehemu kwenye BIBLIA aliwahi kusema "kama msiponisifu basi NTAYAINUA" mawe haya yanisifu. Alijua dhahiri kuhusu intelligences walio kwenye mawe na uwezo wao wa kuongea na sifa za kiumbe hai, sisi binadamu tunaamini mawe hayana uhai lakini mawe yana uhai na yanaweza kuongea sababu Kuna intelligences ambao walichagua kuwa mawe. Ndo mana YESU akasema NTAYAINUA" kwa lugha rahisi NITAYAAMURU haya mawe.
Pia Kuna mfano mwingine kwenye kitabu hiko Hiko cha BIBLIA AMBAPO YESU alikua Ana njaa akaona mti, akadhani Kuna matunda ili ale lakini hakukuwepo na matunda na kilichofata YESU akaulaani Ule mti.. Na BIBLIA INASEMA ukanyauka hapo hapo ni concept huyo hiyo ya UTII wa intelligence (roho) za Viumbe wengine ambao walichagua kuwa vitu hapa Duniani.
Waislam Kuna mafundisho huwa wanasema Kuna siku mkono wako utaongea na kusema mabaya yote, Kuna siku ulimi au Macho utatoa ushuhuda wa dhambi zako ni kweli kabisa. Hii ni kutokana na concept hii hii ya intelligences ambao wametumika kuumba huo mkono, AU jicho lako au Aina organi nyingine mwilini mwako.
Hata kwenyewe BIBLIA tunaona Ile story ya sauli na farasi AMBAPO punda aliongea na kuwasiliana na sauli, pale sauli alipokua anamfosi punda atembee ili akaue watu wa MUNGU punda alisema 'huoni Malaika mbele hapo njiani ". Ni Ile Ile muendelezo wa concept ya INTELLIGENCES ambao wamechagua kuwa PUNDA na wanyama wengine wakipewa ruhusa ya kuongea wa naongea.
MWISHO, Intelligences ndio yenye uwezo mkubwa sana, ndio inayokua ndani ya roho (spirit). Ndo mana wakati mwingine ni ngumu kutofautisha Kati ya intelligences na roho (spirit) sababu ziko ndani ya mwingine.
Na Roho (Spirit) ni muungano wa NAFSI (soul) na Akili (mind).
Nadhani nimeeleweka.