Roho ya Mwanadamu Hupumzika Kati ya Hizi Sehemu Nne (4) Baada ya Maisha ya hapa Duniani

Roho ya Mwanadamu Hupumzika Kati ya Hizi Sehemu Nne (4) Baada ya Maisha ya hapa Duniani

Anayeweza kurudi baada ya kufa ni Yesu Kristo pekee. Huyo ndio mwenye uwezo wa kujifufua. Mwanadam akiondoka ameondoka. Kinachofuata anawekwa mahabusu akisubiri siku yake ya hukumu.
Nani alisema kuna hukumu baada ya kufa??

Mwanadamu mwenzako ambae ameandika hayo nae kaandika akiwa hai na hajawai kufa
 
Kwahiyo hao wazungu ndio reference kwako katika maisha yako?
Kitu kikisemwa na wazungu ndio kinakua ni cha ukweli?

Umejidharau sana.
Wazungu ni reference kwasababu kila unacho kitumia sasa hivi kwenye kila nyanja yako ya maisha wamegundua wao. Wazungu wana ufahamu mkubwa kuliko viumbe wote duniani. Wanajua mambo mengi sana. Sayansi, teknoloji, philosophy, tafiti, dini, hadi michezo wazungu ndio wanaviendeleza.
 
Nani alisema kuna hukumu baada ya kufa??

Mwanadamu mwenzako ambae ameandika hayo nae kaandika akiwa hai na hajawai kufa

Ikiwa maisha ya mwanadamu yangeishia kifo pekee, basi dhana ya haki ya kweli isingekuwepo, kwa sababu wapo wanaotenda mema yote lakini wanakufa wakiwa hawajapata thawabu stahiki, na wapo wanaotenda maovu yote lakini wanakufa bila kupata adhabu yoyote. Hii inamaanisha kuwa kama hakuna hukumu baada ya kifo, basi haki kamili haipo. Mantiki ya uhalisia wa maisha na maadili inahitaji pawepo na hatua ya mwisho ambapo kila tendo linahesabiwa na kulipiwa kwa usawa. Aidha, mwanadamu amebeba ndani yake dhamiri ambayo humjulisha tofauti kati ya jema na baya; dhamiri hiyo haiwezi kuwa bure. Ikiwa inatufanya tuwajibike tukiwa hai, basi lazima kuwe na uwajibikaji wa mwisho unaozidi maisha ya sasa. Kwa hiyo, kwa kuangalia mantiki ya haki na uwajibikaji wa kimaadili, ni wazi kwamba kuna hukumu baada ya kifo.
 
Wazungu ni reference kwasababu kila unacho kitumia sasa hivi kwenye kila nyanja yako ya maisha wamegundua wao. Wazungu wana ufahamu mkubwa kuliko viumbe wote duniani. Wanajua mambo mengi sana. Sayansi, teknoloji, philosophy, tafiti, dini, hadi michezo wazungu ndio wanaviendeleza.
Itakuchukua muda mrefu sana kuja kujitambua na kujitoa kwenye hizo fikra za kitumwa,
Inaonekana hata huijui historia za Dunia,unafikiri kua Dunia imeanza miaka hii tu.
 
Itakuchukua muda mrefu sana kuja kujitambua na kujitoa kwenye hizo fikra za kitumwa,
Inaonekana hata huijui historia za Dunia,unafikiri kua Dunia imeanza miaka hii tu.
Hizo ni story tu mkuu, uhalisia unajionyesha wenyewe. Mwaafrika hana sekta yoyote anayofanya vizuri hapa duniani. Hadi michezo tumezidiwa nawazungu.
 
Anayeweza kurudi baada ya kufa ni Yesu Kristo pekee. Huyo ndio mwenye uwezo wa kujifufua. Mwanadam akiondoka ameondoka. Kinachofuata anawekwa mahabusu akisubiri siku yake ya hukumu.
Watu wanaojiua roho zao zinapumzika wapi ongea ili watu wa JF wenye akili iyo waelewe
 
Saivi ni wachina
Wachina na wenyewe wanatuma watoto wao kusoma Ulaya na Marekani. Tena ukikutana na Mchina kasoma Ulaya au Marekani wanapenda sana. Kitu kimoja nachowapendea Wachina wanaenda kwenye vyuo vikubwa kuchota maarifa alafu wanarudi China kutumikia taifa lao.

Why Chinese students still want to attend U.S. universities
 
Hizo ni story tu mkuu, uhalisia unajionyesha wenyewe. Mwaafrika hana sekta yoyote anayofanya vizuri hapa duniani. Hadi michezo tumezidiwa nawazungu.
Ulizoleta wewe hapa ndio story tu,tena ni story zakufikirika tu,zisizokua na ushahidi wowote ule.
 
Ulizoleta wewe hapa ndio story tu,tena ni story zakufikirika tu,zisizokua na ushahidi wowote ule.

Unachosema ni sahihi, hoja ya hukumu baada ya kifo haiwezi kuthibitishwa kwa ushahidi wa kisayansi kama tunavyothibitisha mambo mengine, kwa sababu hakuna aliyekufa akarudi na kuonyesha ushahidi wa moja kwa moja.

Lakini, wazo la hukumu baada ya kifo linaendelea kusimama katika nguzo tatu kuu za logic:

1. Kanuni ya haki ya mwisho; Ikiwa hakuna hukumu baada ya kifo, basi wema na uovu vingekuwa sawa, kwa sababu hakuna hesabu ya mwisho. Lakini kwa kuwa akili ya mwanadamu hutafuta haki ya kweli, basi ni mantiki kuhitimisha kwamba pawe na hatua ya mwisho ya usawa huo.

2. Dhamiri ya ndani ya mwanadamu; Kila mtu hujua moyoni mwake kuwa anatakiwa kuwajibika. Hii dhamiri isingekuwepo bure; ni ishara kwamba kuna uwajibikaji zaidi ya maisha ya sasa.

3. Hoja ya kimantiki ya ukomo; Ikiwa maisha yamewekewa mwanzo (kuzaliwa) na mwisho (kifo), basi kwa mantiki kuna hatua inayofuata baada ya mwisho huo. Kifo hakiwezi kuwa "sifuri tupu" kwa sababu mwanadamu ameumbwa na akili inayouliza "baada ya hapo nini?"

Kwa hiyo, sio story za kufikirika tu bali ni hoja za kiakili zinazojaribu kutafuta maana ya mwisho wa maisha. Ni kweli hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa macho, ila kuna uthibitisho wa ki-logic unaojengeka juu ya haki, dhamiri, na ukomo wa maisha.
 
Back
Top Bottom