Roketi ya Elon Musk itagongana na mwezi

Roketi ya Elon Musk itagongana na mwezi

Huko itakuwa sio kuugonga mwezi bali ni kuingia kwenye mwezi kwa fujo! Navyojua vitu vinavyogongana viwe hata vinalingana ukubwa ama vinazidiana kiasi kwa jinsi mwezi ulivyomkubwa tuseme unagongwa na roketi!😂
Lugha stahiki hapo tuseme roketi inaangukia mwezini sio kuugonga mwezi.
Mwanaume mwembambaa anaweza kumgonga mwanamke mnene na mimba juu.
 
Sasa hapo marope hizo trillion atakazochota atasumbuliwa na nani kama ataondoka kwenye nafasi bila kashfa?
Kwahiyo unaona wote humo serikalini ni wajinga? Uiibie serikali halafu utoke kizembe? Watakufyatua hutaamini.

Mambo hayaendi hivyo serikalini.

Ni rahisi kuwa mwizi ili ujifiche serikalini kuliko kutoka.

Ukitoka watataka urudishe ulichoiba au wanakuzima.

Uingie serikalini akaunti zako zinasoma 10M, upate 20bn halafu ujidai unataka kutoka, utaeleza umezitoa wapi wakati mishahara ya mawaziri inafahamika.

Jiulize kwanini kina Mkuchika au Chenge mpaka leo wanagombania wakae bungeni au wateuliwe?

Au kwanini kina Abood au Shabiby wanaendelea kuwa wabunge wakati biashara zao zinawaneemesha?
 
Ushakuwa milard ayo...hivi ukubwa wa mwezi unasema inagongana ..hivi nzi anaweza gongana na boeng

Sema hilo taka taka la elon linaenda dondokea mwezi

Roketi iliyorushwa na kampuni ya uvumbuzi wa anga za juu ya bilionea Elon Musk inakaribia kugonga ndani ya mwezi na kulipuka.

Chombo kinachosaidia roketi kulipuka kwa Falcon 9 kilikwenda katika anga za juu mwaka 2015, lakini baada ya kukamilisha safari yake, hakikuwa na mafuta ya kutosha ya kukirejesha duniania na badala yake kilibakia katika anga za juu.

Mtaalamu wa masuala ya anga za juu Jonathan McDowell ameiambia BBC News kuwa itakuwa mara ya kwanza kwa roketi isiyoongozwa kugongana na mwezi.

Lakini anasema athari yake itakuwa ndogo.

Roketi hiyo iliachwa katika obit ya juu miaka saba iliyopita baada ya kukamilisha kazi ya kutuma setilaiti ya hali ya hewa katika safari ya maili milioni.

Ilikuwa ni sehemu ya mpango wa uvumbuzi wa anga za juu wa Bw Musk - SpaceX, ambayo ni kampuni ya kibinafsi ambayo lengo lake kuu ni kuwawezesha binadamu kuishi katika sayari nyingine.
X d
 
Habarini wakuu

Hivi huyu mwamba anaichukuliaje? Hii dunia anaona ni yake peke yake nini? Ujue sisi tumeshalizika na hali zetu asije akatuletea mabalaha bure

Tushajua kama ana maakili sasa anataka nini?
 
Aaaaaargh! Sa' hapa ndo ilipoharibu!! Ingedondokea tu huko baarini halafu samaki wote wanageuka kuwa na sumu, baada ya hapo ngoma droo! Haiwezekani wengine mara misamamki ya kukaanga, mara misamaki ya kuchemsha, mara sijui misamaki ya kuoka wakati wengine full tembele na maharage!

Kabla ya yeyote hajaniona mchawi, hebu jiulize mara ya mwisho umekula lini samaki, kenge wewe (sio Kasomi)!!
Watu wanawaza kuruka juu ww u unawaza kula samaki???[emoji16][emoji16]
 
Huko itakuwa sio kuugonga mwezi bali ni kuingia kwenye mwezi kwa fujo! Navyojua vitu vinavyogongana viwe hata vinalingana ukubwa ama vinazidiana kiasi kwa jinsi mwezi ulivyomkubwa tuseme unagongwa na roketi![emoji23]
Lugha stahiki hapo tuseme roketi inaangukia mwezini sio kuugonga mwezi.
Kuna lugha inazungumzwa sana kwenye ajali za garimoshi (Train), mfano:-
~Mtu kagonga treni.
~Baiskeli imegonga treni.
~Gari imegonga treni nk.
Hii ni pale ajali inapotokea kwenye reli. Hata kama gari imeharibikia relini kisha treni ikaigongea hapo, kwa lugha zao ni kwamba Gari imegonga treni!
 
Mwezi wa 3 umefika wakurungwa, itakuwa tarehe ngapi?
 
Back
Top Bottom