Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Wakati vita vikali baina ya jeshi la Israel na majeshi washirika wa Iran vikikaribia,imetajwa kuwa mashambulizi ya mara kwa mara ya Hizbullah kuzilenga rada na vituo vya ulinzi wa anga vya Israel kumeleta athari kubwa kwa Israel kujilinda kutokana na maroketi yanayorushwa na kundi hilo kutoka Lebanon.
Kwa upande mwengine hata yale makombora yanayotumwa na Israel kudaka yanayokuja kutoka kwa Hizbullah nayo yamekuwa yakiripuka yenyewe kabla kufanya kazi iliyokusudiwa.
Hiyo ni sababu hapo jana kombora moja la aina hiyo lilidongokea nyumba moja kaskazini ya Israel na kuleta mshtuko mkubwa kwa familia ambazo wala hazijapewa indhari ya kuhama na wala hawakusikia king'ora cha kuwatahadharisha kama inavyokuwa kikawaida wakati Hizbullah wakiwa wamerusha zana zao.
Utabiri wa kuzidiwa kwa iron dome kudaka silaha za adui ulitolewa zamani na Marekani na huenda nayo ni sababu kwanini Marekani inakimbiza meli zake kuelekea mashariki ya kati huku fununu zikionesha vita hivyo vya moja kwa moja vimebaki masaa machache tu kuanza.