Role of Indians in the Tanzanian Economy


Hawa nao ni wengine ambao ni untouchables! Kuna Watanzania mpaka leo hii ukisema chochote kinachofanywa vibaya na wahindi kama ufisadi, kuwaingiza wahindi wenzao nchini bila kufuata sheria za uhamiaji n.k. basi utaambiwa wewe ni mbaguzi! Kitu ambacho hakina mantiki yeyote.

Wahindi kwa kushirikiana na mafisadi waliokuwa madarakani wanafanya ufisadi mkubwa sana na tusiogope kusema ukweli, kuwabana, kuwafilisi na hata kuwafungulia mashtaka na kuwataka warudishe pesa walizojipatia kupitia ufisadi wao.
 

sema wewe mkuu, nimeiona hii nikasema haijatulia!!! imekaa kama zile incitations za KKK, SkinHeads au baguzi lolote lilokubuhu likiwa kazini kutafuta sababu.......maelezo yaweza kuwa mengi, lakini swali... what happened to the "slippery slope."?? this was a BAD CALL!!!!

Kuna tofauti gani na kusema chukia kikuyus wote kwasababu kibaki kaiba kura???? mtu atasema oooooh nimesema ma-fisi-adi. hey, una incite average joes, ambao wanaweza wasione huo mstari mchangani!!! Tuwe makini kidogo wasee................
 

Nyani huu ni ukweli kabisa kuwa mafisadi wote ni sawa. Ila fuatilia kashfa zote kuanzia za kina Kiula uone kuwa hakuna fisadi wa kiasia aliyeguswa na wahusika waliishia kwenda Canada na UK kama kawaida yao.

Issue hapa ni kuwabana wote kina Mramba na Patel pamoja nasio kuacha wengine wakitanua na multiple passports zao huku tukihangaika na wengine tu hapa.
 

Mkuu Koba,

Criminal profiling inafanya kila nchi. Nitajie nchi hata moja ambayo haina criminal profiling kwa kufuata race, age, sex, neighborhood, nk na then nitawithdraw my stand kwenye hili.
 

Nakubaliana na wewe kwamba ni muhimu kuwabana wote bila upendeleo kwani Mzee wetu hapa kila siku huwa anatuambia hapendwi mtu wala hapendelewi mtu na kinachopendwa ni Tanzania na Tanzania peke yake. Hao wanaowaachia baadhi ya watu nao inabidi tuwafanyizie. We can't have a different strokes for different folks approach when we are dealing with Mafisadis. Lady justice is and should be color, ethnicity, and national origin blind.
 

Mods naomba mushughulikie hii kauli na muifute bila kufanya ubaguzi, mimi niliwahi kusema nipo tayari kumlipuwa kwa mabomu lowassa kwa ufisadi wake, post yangu ikafutwa haraka-haraka, sasa oneni maneno hayo. na mkiiwacha ntajuwa kuna watu mnawaogopa humu ndani.
 

Huu ni ufisadi wa ukabila, kauli za huyu muasia huyu mwafrika ndio mwanzo wa kuleta huyu mchaga huyu msukuma huyu mzaramo na baada ya hapo itakuwa huyu muislamu huyu mkiristo huyu budha. Huu ni udhaifu wa kufikiri, sidhani kama utasaidia, mimi naona utazidisha balaa na chuki zisizo na mpango. Kama ni fisadi, fisadi tuu, ufisadi hauna ukabila. Mbona wengine tunaamini kuwa nyerere ndio fisadi mkubwa wa roho za watanzania, lakini hatuthubutu kusema wazanaki mafisadi, kwa sababu siamini kuwapaka mavi watu ambao hawana hatia kwa kutaja utaifa wao. Huu ni ukosefu wa busara.
 

Kweli kabisa Ngabu,

Ukiangalia hapa ni kuwa kuna haraka kubwa ya kuwashughulikia weusi huku wengine wakiachwa tu. Mfano mzuri ni hii issue ya wizi wa BoT. Ona jinsi bango kubwa lilivyoshikwa dhidi ya Balali na wakati mhusika mwingine mkuu katika skendo hii Jiiitu Patel akiachwa tu na kupeta kama hakuna kilichofanyika (kuna taarifa kuwa ana mpango wa kukimbia nchi au amekimbia nchi sasa hivi).

Ukianza kumsakama mtu kama huyu na wenzake ambao bado wako TZ sasa hivi utaanza kupewa majina kibao kuwa unaleta u-Iddi Amini katika hili. Kuna wakati criminal profiling inabidi itumike ili kupunguza gharama na kusaidia uendeshaji.
 

Naona unataka kuanzisha mission nyingine ya kugombana na JF kama ile ulianzisha wakati ule ukitumia nick ya ........ Good luck!
 
Naona unataka kuanzisha mission nyingine ya kugombana na JF kama ile ulianzisha wakati ule ukitumia nick ya ........ Good luck!

Nadhani umechemsha, mimi sijwahi kutumia goodluck na sina haja ya kugombana na JF wala yeyote mwingine. Simply najaribu kukufahamisha kuwa kauli za kibaguzi hazijengi bali zinazidi kubomowa na usitake kutia fitna ya kuwa nataka kugombana na JF. Kipi kilichokufanya useme hayo?
 

Mtanzania,

Hata mimi nimekuwa na mawazo haya kwa muda mrefu sana. Kilichobadili mawazo yangu ni hii story ambayo bado inaendelea kufuatiliwa kuwa Jiitu Patel amekimbia nchi. Katika hili na mengine mengi yaliyopita utagundua kuwa wenzetu hawa wanahusika kwa kiwango kikubwa kabisa katika wizi lakini inapokuja suala la kuchukua hatua wao wanaishia nje ya nchi wakati polisi wakibaki na watu wachache tu wenye passport moja (ya Tanzania).

Katika hili mimi nitaitwa mbaguzi ila nikiona jina la muasia katika makampuni yanayolipwa na BoT itabidi nichunguze mara mbili mbili kinachoendelea.
 
Kila siku tunasikia Wahindi kibao wamehusika kwenye scandals mbalimbali lakini nani amewahi japo kufungwa? Hakuna.

Nyie ongeleeni kwamba ni ubaguzi lakini hata huku tuliko wengine, wageni mkitaka kuishi vizuri ni kufuata sheria za nchi husika. Wakigundua kuna ufisadi unaofanywa na kundi fulani la wageni, naamini watakuwa wa kwanza kwenda mitaani.

Si mmeona USA walivyoreact kwa Waarabu baada ya September 11?

Hata hapa UK si mmeona archbishop kutamka tu kwamba baadhi ya sheria kutoka sharia zinaweza kutumika UK, watu wamekuja juu, utafikiri katenda uhaini.

Tanzania inakaribisha wageni wa aina yoyote lakini kama wengine watatumia uungwana wetu huo kutuibia, lazima tuwe tayari ku act.

Inabidi Wahindi wanaotaka kuendelea kukaa Tanzania kwa amani, basi wasaidie kuwaumbua hawa wanaotubia
 

Oh I see where you are coming from and I agree with you. We can't allow Jiitu or any other Fisadi for that matter abscond from justice.
 

Ule wakati wao wa kutumia pesa zao kununua vyombo vya habari vya Tanzania ili mambo yao yasiandikwe unakaribia mwisho. Katika vita hii ya ufisadi hakuna untouchable hapa. Hapa ni sahani moja tu na kina Patel na wenzake. Kuna wakati inabidi maamuzi makubwa sana yafanywe ili kuinusuru nchi.

Hapa marekani kina Bushi na wenzake waliingia mkataba na kampuni moja ya Dubai ili kufanya kazi ya kupakia na kusafirisha mizigo hapa Marekani na nchi nzima iliwaka moto na mkataba ukavunjwa. Kuna wakati maamuzi makubwa inabidi yafanywe hasa ukichukulia kuwa hawa jamaa wanatokea kwenye kila ufisadi nchini na mambo yakiharibika wanakimbia nchi!
 

Hiyo si point, fisadi ni yule aliyejuwa kuwa hawa wamefanya ufisadi halafu akawaacha wasafiri wapande ndege (au waliondoka na meli?), waende canada. Aliyewaachia ndie fisadi mkubwa, sasa tunataka utujulishe alikuwa muasia? mkurya? mzaramo? muhaya? mchaga? tupe jibu tukilipata basi kabila hilo tuanzae kuwaita mafisadi wote, si ndiyo utakavyo? kama umekosea ni wajibu wako kuomba msamaha binadamu wote huwa tunapotea, lakini mbora kati yetu ni yule anaekubali kupotea mapema na akarudi kwenye mstari mapema. Hili la utaif umechemsha sana mwafrika wa kike.
 

Hiyo si point, fisadi ni yule aliyejuwa kuwa hawa wamefanya ufisadi halafu akawaacha wasafiri wapande ndege (au waliondoka na meli?), waende canada. Aliyewaachia ndie fisadi mkubwa, sasa tunataka utujulishe alikuwa muasia? mkurya? mzaramo? muhaya? mchaga? tupe jibu tukilipata basi kabila hilo tuanzae kuwaita mafisadi wote, si ndiyo utakavyo? kama umekosea ni wajibu wako kuomba msamaha binadamu wote huwa tunapotea, lakini mbora kati yetu ni yule anaekubali kupotea mapema na akarudi kwenye mstari mapema. Hili la "mafisadi waasia" umechemsha sana mwafrika wa kike, ufiadi hauna rangi wala kabila wala dini.
 
Mkuu Koba,

Criminal profiling inafanya kila nchi. Nitajie nchi hata moja ambayo haina criminal profiling kwa kufuata race, age, sex, neighborhood, nk na then nitawithdraw my stand kwenye hili.

Mwafrika wa K:

Ndio criminal profiling inafanyika kila nchi lakini sio kila criminal yoyote hile inayokuwa profiled. Ufisadi mara nyingi huko katika kundi la uhalifu wa Social Engineering, fraud na white-collar crime. Katika aina hizi za uhalifu unatakiwa kuwa vigilant na kundi lolote lile kwani umdhaniaye siye kumbe ndiye (Balali).
 

Unalijua vizuri jina lako lingine so good luck na hii mission ambayo ilishindwa in the first place!
 

In the end, kama umefuatilia kesi ya Enron kwa makini, utajua kabisa kuwa investigators waliprofile watu na wakadeal na watu wachache kabisa na kuacha wengine wengi (hasa wanawake) katika uchunguzi wao!... huu ni mfano mmoja tu na defense ilijaribu kutumia hii kama defense yao ikashindwa vibaya sana kwa vile criminal profiling ilikubaliwa na judge kuwa ni sehemu muhimu sana ya uchunguzi na uendesha mashtaka.
 

Kuna hao unaosema wahindi, sijuwi unawatambuwaje? kwa rangi zao kwa majina yao au kivipi tufahamishe tuelewe. Maana huu sasa ni ubaguzi wa rangi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…