Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ufisadi hauna rangi, tubishane mpaka tutoane macho ukweli utabaki kuwa, hao wanaoitwa waasia shughuli zao zaidi ni biashara, na mfanyabishara yeyote faida mbele ukimpa upenyo kidogo kakutoka!
Wafanyabiashara wengi ninao wajua mimi Tanzania ( labda ukiondoa Bakhresa ) wengine wote wana maskendo ya kukwepa kodi, kushinda zabuni kiujanja nk si Mengi, si Manji si Mohd Ent wala Malinzi wote mwendo mdundo.
Hoja yangu hapa ni kuwa rushwa ( Grand corruption ) ambayo nadhani ndio mama wa ufisadi inapatikana zaidi kwenye mambo ya kodi na zabuni na kwa kuwa players wengi huko ni hao "waasia mafisadi" its obvious utawakuta wengi, same applies ukiangalia rushwa ndogo za mahospitalini huko hutowakuta "waasia mafisadi" bali akina sisi, the bottom line hapa ni ufisadi hauna rangi ukidhibiti mianya ya rushwa hakuna wa kufurukuta.
Jiulize swali rahisi tu hao "waasia mafisadi" mbona hawakutamba wakati wa Mwalimu?
Tuendelee tukimaliza waasia tuhamie "mafisadi wa wakenya" maanatakwimu zinaonyesha wawekezaji wakubwa Tanzania ni wakenya..... dhambi ya kula nyama ya mtu....
Nilipo nina passport mbili na sio Mwa-Asia. Kuna watanzania wengi wazawa walikimbilia South Afrika katika miaka ya 90s na kuchukua uraia wa SA.
Na kisa cha kuchukua passport ya pili sio kufanya criminal ni kuweka nafasi yangu ya ajira katika nafasi nzuri na kupata grant za biashara ya kwenda shule au kufanya biashara wakati wowote ninapotaka.
......
malumbano binafsi ya nini sasa?? mie sioni hata kwanini mmefikia hapo mlipo!!! kushambulia kwa staili mfanyayo nao pia ni UFISADI, kwani mnapoteza muda muhimu wa watu kusoma pumba zenu.
Masatu,
swali lako ni muhimu sana hapa.... mafisadi hawakutamba wakati wa mwalimu kwa sababu nyingi ikiwemo alichofanya Moringe na wenzake kabla yake..... criminal profiling ......
I just gat started, kama ulikuwa hujui, mimi ni mpuuzi sana na ndio tu nimeanza ubaguzi hapa dhidi ya mafisadi wa kiasia mpaka kieleweke.
Yakikuuma sana itabidi umeze nyembe au uende kwa fisadi Manji upewe ice cream ama maziwa.......
Mkuu nadhani umesahau kuwa kwa sheria za Tanzania za sasa ni uvunjifu wa sheria kuwa na passport mbili (hili lina mjadala wake mwingine kabisa) au sio?
Kwahiyo, hoja yako ya kuwachukia mafisadi wenye asili ya kiasia haina nguvu!!! Kumbe ufisadi sio rangi ya mtu, bali ni matokeo ya utawala.
Ninawashangaa wote mnaounga mkono hii hoja. Hivi hamjiulizi kwanini hawa wafanyabiashara wenye asili ya asia wanayafanya haya tanzania, lakini UK, Canada, Australia, China hawawezi kuyafanya haya??? Jengeni hoja za maana, sio kujenga chuki zisizo na msingi. Mimi napinga hii hoja, na ninamshangaa sana Mwafrika wa kike kwa kuanzisha hii mada!! This is not your standard mwafrika.
wewe fanya upuuzi wako wa ubaguzi na watu watakujibu kwa huo lakini usiniingilie personal na kunipachika jina la sijuwi nani wako?, huyo good luck?
Masatu,
swali lako ni muhimu sana hapa.... mafisadi hawakutamba wakati wa mwalimu kwa sababu nyingi ikiwemo alichofanya Moringe na wenzake kabla yake..... criminal profiling ......
Zomba AKA "goodluck" AKA ......
Consider yourself ignored by Mwafrika wa kike for now!
Ninachojaribu kuonyesha kuwa criminal profiling yako haina mpango wowote hule.
Umefika wakati waafrika au wazawa kuelewa kuwa chanzo kikubwa cha matatizo yao ni wao wenyewe na sio mgeni kutoka nje na hakuna sababu ya ku-profile.
mmh hata sigahamu kwanini hawako mbeya,songea wala rukwa.yaelekea sehemu ulizozitaja zina biashara sana na mianya ya biashara haramu ndio maana wapo,pia watu wa huko sio wakali sana labda lakini labda pia wanashindwa na mijipesa yao. Ni wazi kuwa hiki kigezo cha pesa kinapaswa kuondoka kwa juhudi zote kwa kusema kwamba kila mtu kabla hajaanza kampeni aseme anazo pesa kiasi gani na amezipataje kwenye tume maalumu mf.tume ya maadili na hizo pesa zinatumikaje? hasa kwenye ubunge na urais. Kwa ufupi nina maana adisclose source.zaidi ya hapo tunacheza.wataendelea kutawala wenye nazo,na sio wenye nazo wenye kutumwa na wenye nazo huko majuu wakiwamo mafia,na hao kina jeetu patel.wee unadhani NYERERE alipomkataa malecela mwaka 1995 ilikuwaje? hadi akatoa kauli hii " I CANT LET MY COUNTRY BR RULED BY DOGS" alipoulizwa kwa nini anarudi kwenye siasa wakati alishang'atuka? kuna taifa moja hapa ulaya lilishamuahidi mapesa kibao na kama angeshinda urais walikuwa na dili naye,ten hadi kanisa lilihusika mchonga akagundua mapemaaaaa,kaingilia kati.Wana JF alipoandika kitabu chake cha UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA alimaanisha sana hebu kitafuteni mkisome.Uchunguzi unapaswa kuwa kwa wote chama tawala hadi wapinzani nao.Augustoos,
1. Ila kwa nini hawa wabunge hutoka Morogoro, Igunga, Dar kwa nini wasichaguliwe kule Moshi Vijijini, au Karagwe au Rungwe?
2. Taabu kubwa ni huu utamaduni wa mtu mwenye pesa tu ndo ataweza kugombea! Sasa watu wazalendo wa kawaida vipi?
Transparance tunahitaji zaid ktk mchakato wa uchaguzi!
Ukiwa na wabunge waliochaguliwa kwa rushwa- hawawezi kuipiga vita rushwa!
masatu,
ufisadi wa wa-asia ulifubaa wakti wa mchonga kwasababu moringe alikuwa amedhibiti virutubisho vya tabia hii kushamiri. ndio maana wakina sisi tunadhani tatizo ni uzalendo kwa watz wooooooooote wa kuendekeza rushua regardless of color, gender, religions or whatever.........nimeuliza hapa na nadhani nimekuwa ignored, je ma-fisi-adi "weusi" wangapi waliofikishwa kwa pilato na kuhukumiwa??.
Haya ni mawazo yako mkuu na siwezi kukulazimisha wewe kuamini otherwise au kuamini kile ninachoamini. Mimi naamini kuwa mafisadi wa kiasia wanapata sana breki Tanzania na mimi nimeanzisha kampeni dhidi yao.
Kama nitafanikiwa au kama itachukua miaka miwili (kama muda uliopita kumtoa Lowasa) au miaka mia moja hiyo haijulikani kwa sasa ila mimi na hawa mafisadi wa kiasia ni ama zao ama zangu!
wewe unajuwa nini kuhusu criminal profiling wewe? uliambiwa kuwa criminal profiling ni ubaguzi wa rangi?
Nawe kujiunga kwenye kundi lako maana na mimi nakubaliana nawe wakati wewe unawabana zaidi wahindi mimi nitakuwa nawatafuta wazalendo aina ya Mramba, Sumaye, Lowasa,Diallo etc ili tumalize kazi kwa mara moja inshallah Mnyezi Mungu akiwa nasi ?
Ameni Lunyungu,
Miaka miwili iliyomalizika juzi ijumaa, kazi kubwa ilikuwa kumtoa fisadi mmoja mkubwa kabisa madarakani - Lowasa - na MUNGU alisaidia hili likafanikiwa.
Next phase, ni kufuatilia wanaosaidiana naye na ambao mara nyingi sana hawatajwi kwenye vyombo vya habari na hupewa breki sana kwenye news circle - mafisadi wa kiasia - tukianza na Patel na Azizi.
Good luck kwenye front yako na mimi naomba tu niendelee kuwa hai ili wote hawa wakamatwe na isibakie justice system ya upande mmoja. Katika hili nitaitwa mbaguzi na I am ok with that..... endelea kufuatilia magazeti ya nyumbani (huru) kwa miezi sita ijayo.