Kaka Wahindi na Waarabu wa Tanzania wanatubagua big tyme mbona hulioni hili ? Kuanzia kazini , misikitini na hata mahapa pa kuishi na ajira nk .Hata juzi wahindi wametangaza nafasi ya kazi kwa Mtanzia wa Asia hili vipi ? Si ubaguzi ama unaona comments za mzalendo Mwafrika za kujenga ni Ubaguzi ?
Hilo mimi nakupinga, misikitini hakuna ubaguzi kabisa, mimi ni muislamu na hilo hunielezi. Kutangaza mtu kazi kuwa anataka mfanyakazi wa kiasia sio ubaguzi, ni mahitaji nya wakati huo. Ungekwenda kutazama huyo aliyetangaza hivyo hana wafanyakazi wengine ambao si waasia?
Makanisani, sijui kwani siendi huko, labda huko kuna ka-ubaguzi. Lakini misikiti sahau, mwafrika, mwarabu muhindi, tajiri, masikini wote wanasali bega kwa bega. nakukaribisha msikiti wowote ukajionee mwenyewe.
Mbona Dar kuna msikiti wa "Manyema", ndio jina lake lakini haimaanishi wanaoswali humo ni wamanyema tuu, upo wa "Makonde", wa Wa-"Manga". lakini hukuti kubaguwana hayo ni majina tuu.
Mwafrika wa kike anachoongelea ni ubaguzi wa hali ya juu, hivi leo tukianza na "waasia mafisadi", na hawa wakina lowassa nauliza tuwaite "wamasai mafisadi"? Haiwezekani kubaguwana. Ufisadi ni ufisadi tuu, uwe muasia, muyuropa, mchina, mhehe, mnandi, mtaita, mbarbaig, hauna tofauti na mwingine juu ya ufisadi. Hatukupewa makabila ili tubaguwane, makabila ni kwa ajili ya kufahamiana tu.