Tangu mafisadi waanze kutajwa, wengi wao wamekuwa ndio wale vinara wa kuchangisha pesa, kuweka fundrising misosi kwenye hotel nzuru(kwa pesa zetu walizoiba), ili kupata pesa nyingi kwaajili ya kampeni za ccm. jambo hili wala si geni. wengi wao ni watanzania wenzetu wenye asili ya kiasia, ndio wamekuwa vinara kwa miaka mingi. Mafisadi mapapa wametajwa na wengine wameshakamatwa. macho yangu yanasubiri kuona kama mwakani ccm watakuwa tayari kupokea hela toka kwa mafisadi. najua Jeetu atachangisha akiwa segerea pamoja na yule patel mwingine. sumaiya atakuwa anarandaranda kuhamisha hela na kuuza mali zake ili zisifilisike muda huo hatakuwa nao. manji na Rostam watakuwa wanajenga magorofa na mahotel Dubai, south africa na switzerland ili hela zao ziondoke kabisa hapa bongo. wakti wowote wakitaka kukimbia nchi wachukue tu brifkes na kupanda ndege. atakayebaki kuwachangishia ccm ni nani? jamani atakuwa nani? na wakati atakayefanya hivyo naye atatakiwa kuonyesha hela na uwezo huo anautoa wapi?
hapo ndipo kilio cha Watanzania kitakaposikika na Mungu wangu(mimi mwana wa Mungu). nchi yetu imeikuwa ikiizwa kwa pesa za uchaguzi kwa miaka mingi, viongozi wetu hawana hata raha, hawana sauti vizuri kwasababu sauti zao waliziuza wakati wa kampeni kwa mafisadi. fisadi hata akijisaidia njiani mbele ya rais wa jamhuri, hawezi kukamatwa kwasababu rais amemwuzia sauti,miguu, mikono na viungo vyote akaachiwa tu macho na masikio awe anawaona na kuwasikia na kulia machozi tu. meno wamemng'oa.
viongozi wetu wamekuwa mbwa wasio na mengi, na sisi tunawarushia nyama yenye mifupa(mafisadi) ndio maana wanashindwa kung'ata, kwasababu waliuza meno yao na viungo vyao. utumwa huu utaisha lini? CCM utumwa huu utaisha lini? si bora mchangishe kwa wananchi wa kawaida kama alivyofanya Obama kuliko kuchangisha kwa mafisadi? mwakani tuna ninyi, mtatukoma. uchaguzi wa mwakani, selikali itabidi ijiandae sana, ijiandae kwa kujisafisha kwa kukamata mafisadi wote, ndipo wataonekana wasafi. na hasa mafisadi mapapa. halafu waje kambare.