Pole sana braza kwa rungu lilokupata safari hii tena licha ya mateso makali uloyapata katika kuvuka milima,mabonde na jangwa kuelekea Zimbabwe.
Braza tunajua kuwa safari yako ilitokana na wewe kuchimbwa mikwara kidogo,ila hayo tuyaache.
Braza nakupa pole sana kutokana na adhabu ulopewa baada kutoa kale kawa kawimbo ka "SITAKI KIBAXXXX MWANAUME MASHINE"
Sasa braza inakuaje rungu limekuangukia peke yako,kwani yule jamaa mwingine na kale kadada wao walifutika kwenye wimbo au ndo nanilii bado inaendelea ?
pia braza mbona safari yako ya Zimbabwe imekubadili sana hadi unaandika mambo ya ajabu ajabu sana,kwani walikulisha nini kule ?
labda nikushauri tu,hebu rudia tu katika tungo zako za zamani ila zipangilie vyema,siuna ona mjomba sizo za nje anavyofanya yani anagawa dozi na wala hata hawamsumbui,na wewe fanya tu kama yeye ili ubaki kuwa rapa na baba wa familia.
hivi vinyimbo yani kama vile vinakushusha CV yako kimtindo bila we kujijua