Roma afungiwa miezi sita kujihusisha na sanaa

Roma afungiwa miezi sita kujihusisha na sanaa

Unafurahia matusi badala ya mziki?
Kwanini hawakukagua kabla wakajiridhisha ndipo Wadanganyika tuanze kusizikia nyimbo hzo ila wakafanya kinyume chake? Trump is always right shithole country.
 
Hv yule aliyeimba Sizonje kwanini hawajamfungia au huko BASATA hawakusoma literature?
 
Nipo nasikiliza hapa bongo bahati mbaya ghetton kwangu
 
Inamaana kama hiyo ngoma ingekuwa kwenye Album, wangefungia Album au? Wananchi ndo wanapenda hizi nyimbo ajabu serikali yao haizitaki, basi wasanii wote waimbe kwaya tu au nyimbo za kuisifu serikali. Bongo Bahati Mbaya ni moja kati ya nyimbo zangu bora kabisa na haijawahi nifanya eti niwaze kwenda kuishi nje wala nini, huwa napata vibe tu na kukata stress zangu
 
Nyimbo zimehifadhiwa kwenye memory cards ya simu, ipad, flash disc na kwenye hard disk za computer zinafungiwa vipi? Zaidi nyimbo ni freely downloadable kwenye internet. Kufungiwa is mere symbolic gesture. Wamekurupuka tena.
 
Sasa hao basata toka nyimbo zitoke mpaka zimesahaulika ndoo wanazifungia walikuwa wap mda wote huo,ubabaishaji.com
 
KUTII KIVIPI? yeye ana studio ya matangazo tuseme bado anaucheza huo wimbo? Kama hana hela ya kufanya hayo marekebisho akaamua aachane na huo wimbo sabababu ishafungiwa kuna kosa hapo?... Aisee hii serikali ya sasa inahamasisha machafuko aki.
Anzisha hayo machafuko basi. Sio unakaa unapayuka payuka hovyo mtandaoni kila siku; haisaidii kitu.
 
Msanii Roma anaeunda kundi la ROSTAM amefungiwa kutokujihusisha na sanaa kwa muda wa miezi sita ikiwa ni kama adhabu ya yeye kutokutii agizo la baraza la sanaa tanzania (BASATA) la kufungiwa kwa nyimbo yake ya KIBAMIA akiwa na Stamina wakimshirikisha Maua Sama!

Nyimbo hio ilifungiwa mapema jana tarehe 28/02 na kumtaka ROMA kubadilisha maudhui ya nyimbo hio.....!Nyimbo zingine zilizofungiwa ni pamoja na
1.Hallelujah ya Diamond.
2.Waka ya Diamond.
3.Hakuna Ushemeji ya Man Fongo.
4.Pale kati ya Nay.
5.Chura ya Snura
6.Nampa Papa ya Giggy money
7.Bongo bahati mbaya ya Young Dee na zingine 7!!!
Akiongea na waandishi wa habari Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Juliana Shonza amesema kuwa amechukua maamuzi hayo kutokana na kumwita msanii huyo ili aweze kufika kwenye mkutano huo lakini hakuweza kufika wala hakutoa taarifa yoyote ile.

"Roma Mkatoliki alipigiwa simu na BASATA hapokei na anatumiwa message anasoma lakini hajibu kitu, kwa hiyo kimsingi hilo ni kosa kwa sababu tumemuita si kama tumekurupuka bali Roma Mkatoliki aliutoa wimbo wake muda kidogo unaitwa Kibamia kimsingi ule wimbo ameimba matusi matupu na ni wimbo ambao kiasi fulani unadhalilisha kwa sababu mtu unapozungumzia kibamia huitaji kujiuliza kibamia ni nini kila mtu anajua maana ya kibamia, mimi siamini hata mtu ambaye yupo hivyo anakuwa amependa"

Juliana aliendelea kutoa ufafanuzi kuhusu suala la Roma Mkatoliki

"Nakumbuka mwaka jana nilikuagiza Mkurugenzi wa BASATA kwamba umwite Roma Mkatoliki ukae naye chini, kwenye onyo lake la kwanza mwambie afanyie marekebisho huo wimbo na uzuri BASATA walimwita wakaa naye chini wakamwambia kasoro za wimbo wake na kutakiwa kufanya marekebisho ya wimbo huo ikiwepo jina lenyewe la Kibamia, pamoja na baadhi ya matusi ambayo yapo kwenye huo wimbo. Roma Mkatoliki alikubali na kusema ataenda kufanyia marekebisho hizo sehemu cha kusikitisha mpaka saizi napoongea hakuna ambacho kimefanyika na mbaya zaidi wimbo huo unaendelea kupigwa kwenye vyombo vya habari"

"Roma Mkatoliki amedharau maagizo ambayo alipewa na BASATA na kwa sababu tumemwita leo na hajafika bila taarifa yoyote hivyo amedharau wito, mimi kama Naibu Waziri wa Habari pamoja na BASATA tumekubaliana kwamba huyu ndugu Roma Mkatoliki tunampa adhabu kwa mujibu wa Katiba na kanuni, hivyo tunamfungia kwa muda wa miezi sita ndani ya muda huo wa miezi sita hakuna kufanya kazi yoyote ya sanaa, hakuna kutoa wimbo wowote, hakuna kufanya show sehemu yoyote, huo wimbo moja kwa moja tunaufungia" alisisitiza Shonza
 
Back
Top Bottom