Tetesi: Roma Mkatoliki akimbia nchi, sasa anaishi uhamishoni

Tetesi: Roma Mkatoliki akimbia nchi, sasa anaishi uhamishoni

Huyo kaenda kubeba box na njaa yake,nani kamfukuza bongo?Vijitu vingine bwana ilimradi navyo vionekane vimo.
 
Kazi na duck
Happy new year 2020 wanaJF

Kwa kitendo hiki kama ni kweli kulingana na nilivyosikia, basi nchi yetu imefikia pabaya

Msanii wa Hip hop Roma Mkatoliki baada ya kutoa ule wimbo wake "Naitwa roma" unaohusu maswala ya siasa za hapa nchini hususani zinamrengo wa kuipinga serikali, msanii huyo sasa amekimbia nchi kwa kuhofia usalama wake kufuatia kutoa kibao hicho

Roma Mkatoliki kwa sasa amekimbilia nchini Marekani akihofia kukamatwa, kutekwa, na kuuliwa na serikali hii ya Rais Magufuli

itakumbukwa miaka ya nyuma msanii huyo alitekwa na kuumizwa vibaya, mpaka sasa waliofanya tukio hilo ni watu wasiojulikana

Nahoji kama Mtanzania wa kawaida, haki ya mtanzania kuishi katika nchi yake hapa inatazamwa vipi?

Uhuru wa kujieleza na kukosoa hapa nchini ni wa kitabaka tu? Yaani CCM ndio wanahaki ya kuukosoa upinzani pekee?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sipendi mchez mchezo mimi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua polisi kuna kitengo cha Fraud? Unafikiri kwanini yule mwanachuo wa UDSM aliposema ametekwa walimkamata na kumpandisha kizimbani? Kesho nenda sehemu kajifiche ndugu au mtu yoyote asijue halafu wapigie simu ndugu na marafiki uambie umetekwa kisha waambie wakaripoti polisi. Baada ya wiki 3 jitokeze uone shughuli yake. Ndiyo utajua kama ni mradi wa kujiteka uko vipi. Jaribu kupitia vifungu vya sheria vitakusaidia kuliko kusoma umbea jamii forum na mitandao mingine ya kijamii.
Kifupi tu. Udanganyifu wa aina yoyote ni kosa la kisheria kwahiyo hapo wakigundua umejiteka lazima ukanyee ndoo kwanza ili iwe fundisho kwa wengine. Huo mfano kajaribu halafu uje utoe mrejesho hapa.
Ulivyosema sio vigezo vya mtu kupewa ukimbizi au hifadhi nchi nyingine. Kimataifa hayo ni mambo ya ndani na yanatakiwa kushughuliwa na wahusika wa ndani. Hakuna ushahidi wowote unaomuhusha Roma kutekwa na shughuli za kisiasa, kidini au kijinsia. Na muda wote toka aseme ametekwa mpaka anaondoka hakuna jambo lolote lililo msibu.
 
Sio Roma pekee ambaye yuko hatarii, kila mtanzania hivi sasa anaishi kwa hofu!
Mtu yoyote duniani anayeishi kwa kujiachia bila woga wa maisha yake, huyo mtu ni mjinga na anafikiri kila mwanadamu mwenzake ni malaika.
 
Mtu yoyote duniani anayeishi kwa kujiachia bila woga wa maisha yake, huyo mtu ni mjinga na anafikiri kila mwanadamu mwenzake ni malaika.
Umeandika nini mkuu, kwani hofu na woga yana maana sawa?
 
Ni mradi alioubuni kwa muda mrefu, kujiteka, kutoa nyimbo ya kuchafuwa watu fulani ili iwe kisingizio kama hapa Tanzania hayuko salama. Lakini Wamarekani sio wajinga, Bobi Wine alishidwa kubadili ukaaji wake nje, sidhani kama Roma ana kigezo chochote cha kubeba kesi yake.
Alijiteka na kusingizia watu wasoijulikana!
Kumbe mahesabu, lakini ilimsaidia kupata kiki
 
Back
Top Bottom