Roma Mkatoliki akumbushia alivyotekwa na mambo aliyofanyiwa

Roma Mkatoliki akumbushia alivyotekwa na mambo aliyofanyiwa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Msanii wa muziki wa Hip hop, Ibrahim Mussa maarufu kama Roma Mkatoliki, amekumbushia kwa uchungu tukio la kutekwa kwake lililotokea mwaka 2017, akieleza namna alivyoishi katika hofu, mateso na hali ya sintofahamu kwa siku kadhaa alipokuwa mikononi mwa watu wasiojulikana.

"Wito wangu ni tukemee na kupinga kwa nguvu zote, kwa uwezo wetu wote, pale ambapo tunaona haki haijatendeka. Tutengeneze huo utamaduni, utatusaidia sana. Tusisubiri mpaka limkute mwingine kwa sababu litakuja katika namna ambayo hutalitegemea."

"Naongea haya nikiwa natamani sana haya mambo yasimkute mtu yeyote yule, hata ambaye ni adui yangu, ananichukia."

"Unamuona marehemu Enock alivyokuwa anapigwa, hiyo video nimeitazama ime-trigger vitu vingi sana. Naweza kusema hivyo vitu nikiviona inapa trauma. Sasa mimi nilipigwa na watu sita kwa mkupuo na kila mtu na silaha yake."


 
Aseme yotee, asifiche kitu. Ili umma ujue kinaga ubaga ya watekaji. Lol
 
wakuu

======

Mwanamuziki na mwanaharakati maarufu nchini Tanzania, Roma Mkatoliki, amekumbushia kwa uchungu tukio la kutekwa kwake lililotokea mwaka 2017, akieleza namna alivyoishi katika hofu, mateso na hali ya sintofahamu kwa siku kadhaa alipokuwa mikononi mwa watu wasiojulikana.

 
Back
Top Bottom