Roma Mkatoliki amwibua Mwakyembe, adai hana elimu ya kumshauri yeye mwenye digrii 4. Kama anapenda siasa aanzishe chama cha siasa


He is trying to instill common sense that mr Phd does not have
 
Binafsi mpaka sasa siamini kama Mwakyembe ndio kuongea huo upumbavu vinginevyo nitaendelea kuamini tuna watawala wapumbavu kuliko tunavyodhani
 
Hapa waziri amechemka. Akili sio una phd ngapi akili niuwezo kujibu changamoto nakutatua matatizo.
 
Hilo ni ingizo jipya kwenye mradi wa kulipwa elf 7
We jamaa, kwani usipochangia kila uzi unaoletwa humu jukwaani utapungukiwa nini? Au ndiyo siku haitaingia! Hivi huoni unakidhalilisha chama na pia unamdhalilisha mwenyekiti wako!!
 
Alafu nilazima mkumbuke kijana anamlenga mtu mwingine kabisa wala sio hao tunawafhani. Sio waziri wala sio rais ila kuna mtu anamlenga. End
 
Mkuu embu turekebishie kichwa ha habari.
Nimejaribu kukigeuzageuza kinakataa kila uelekeo.
Aliyebeba kichwa cha habari ni Roma au ni Mwakyembe?
 
Mtanisamehe watani zangu Wanyakysa hivi huyu ndo roll model wenu vile
 
Tatizo la wasomi wa taifa letu ni wao kuwa wabinafsi kutokana na umahiri wao ktk madesa, na kujiona fahari zaidi ya watu wengine kutokana na vyeti walivyovipata ktk taaluma zao. Huku wakiwaona watu waliokosa fursa kama wao kuwa ni vilaza na hawana akili ya kuweza kuchangia jambo la maana ktk jamii, isipokuwa ni wao "elites" tu.

Ktk hili la msanii Roma Mkatoliki, Dr. Mwakyembe kajipambanua kuhusiana na hulka hiyo potofu hakuwa juu wa watu wengine, hakuwa makini na hata amedhihirisha kukurupuka na kuropoka juu ya kazi ya kisanii iliyotolewa na msanii huyu. Hayo maganda yake manne ya shahada mbalimbali hayampi uhalali wa kudharau haki ya kikatiba ya mtu mwingine.

Hata kama Roma kaishia darasa la saba, kwa wakati wake si ndiyo ili kuwa elimu ya msingi. Elimu ambayo waheshimiwa wenzake na Mwakyembe umewafanya wastahili kuwa wabunge! Msukuma, Kibajaji n.k tunawaona walivyoamiwa na kuwa sehemu ya "think tank" ndani ya chama tawala, ktk hili sijui yeye analisemaje kwa kigezo hicho hicho cha maganda yake ya elimu ya juu.

Ukienda ktk makundi ya wafanyabiashara maarufu, wasanii wa filamu na muziki maarufu, viongozi wa dini na hata wazee wengi wastaafu, kwao kukosa elimu kama yake hakumfanyi kustahili kuwapa heshima, wala kuweza kujadiliana nae! Eti kwa kigezo hicho hicho cha kukosa elimu ya juu kama yeye. Nafikiri alipata mhemuko tu ili kumridhisha bosi wake, na wala si vinginenevyo.
 
Mitume na manabii wa vitabu vya dini tunazoamini na kufuata hawakwenda shule yoyote. Ajishushae huinuliwa BUT ajiinuae hushushwa!
 
GPA za kumeza(Kukariri usiku mzima) kisha unatema kesho kwenye paper ndo kuwa na akili? Si huyu huyu aliyekana thesis yake showing kwamba hata alichokiandika mle either hakijui au aliandikiwa
 
Hatakama ulikuwa kipanga darasani kwa kiasi gani lakini ukishindwa kutafsiri elimu uliyonayo katika mazingira yako ni kazi bure,impact ya taaluma yako kwenye jamii ni nini?
Ulishawahi kujiuliza ni kwanini sikuhizi degree zinadharaulika?Unafahamu kwamba NGOs nyingi sikuhizi hawaangalii degree zaidi ya kuangalia capacity ya delivarence?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…