Roma Mkatoliki amwibua Mwakyembe, adai hana elimu ya kumshauri yeye mwenye digrii 4. Kama anapenda siasa aanzishe chama cha siasa

Roma Mkatoliki amwibua Mwakyembe, adai hana elimu ya kumshauri yeye mwenye digrii 4. Kama anapenda siasa aanzishe chama cha siasa

Return Of Undertaker, Waache double standards. Wasanii wanaposifia wanasiasa wanakaa kimya, wakikosoa shida. Vivyo hivyo kwa viongozi wa dini. Wakisifia na kulamba viatu vya wanasiasa haina shida kabisa, wakikosoa wanaambiwa waache kuchanganya dini na siasa. Juzi nimemsikia Zakary Kakobe anavyosifia juhudi nikajiuliza sana. Ndiyo huyu huyu aliyesema ni tajiri kuliko Serikali?
 
Return Of Undertaker,
Le mutuz ana degree 7 lakini hana mbwembwe

Tuntemeke Sanga alikuwa nazo 6

Wingi wa degree ni ushahidi wa kutojiamini.

Jiulize mtemi Chenge ana degree ngapi? Lakini ukiondoa Wanasayansi, hawa wenye PhD za ngwini hakuna anayemfikia kwa weledi.

Wazungu leo hii hawajivunii degree wala hawataki kuitwa Madokta, unajua kwanini?

Mwisho kabisa Diamond aliyeishia la 7 pale Tandale amemuajiri Le mutuz mwenye degree 7 zote kutoka Marekani na Ulaya

Maendeleo hayana vyama!
 
"Kama msanii unang'ang'ana kuimba siasa na kukosoa serikali basi amua kuachana na muziki uanzishe chama cha siasa. Lakini kama unataka kupata maslahi kwenye muziki, basi nyimbo hizo hazilipi. Haiingii akilini nina shahada nne halafu msanii ambaye hajaenda hata shule anatunga nyimbo za kunikosoa. Wewe na darasa la nne lako sijui la 7 utanionya mimi mwenye degree nne na nimefundisha vyuo vikuu mbalimbali?" Dr.Harisson Mwakyembe (PhD), Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo.!

Kweli Roma kamuibua huyu?

Ujue Roma ana power kuliko maelezo ni pale mwenye degree 4 anang’ang’ana kumjibu mwenye degree moja!

Na Roma ana degree moja,Mwakyembe aache kudanganya umma!

Roma nilikaa naye pale Mabibo Hostel!

Hatari sana aisee!
 
Kama kweli kayasema hayo, basi hayo ndio tunaita matumizi mabaya ya akili.

Hua najiuliza kama hii ndo aina ya viongozi tunaowaamini kufanya maamuzi ya nchi. Je, nchi yetu iko salama kweli?
Natamani huu uzi uwe ni propaganda na isiwe kayasema hayo kweli .
 
Back
Top Bottom