Roma Mkatoliki amwibua Mwakyembe, adai hana elimu ya kumshauri yeye mwenye digrii 4. Kama anapenda siasa aanzishe chama cha siasa

Roma Mkatoliki amwibua Mwakyembe, adai hana elimu ya kumshauri yeye mwenye digrii 4. Kama anapenda siasa aanzishe chama cha siasa

Roma arudi shule jamani

Mtu anaefundisha au aliwahi kufundisha chuo sio wa kumfananisha na alieishia darasa la saba jamani huo ni ukweli usiopingika

Mwakyembe alipasua GPA kubwa Bachelor akabakizwa kuwa mwanataaluma UDSM huwezi fananisha na Msanii yeyote hapa nchini
Kaisadia nini Dunia wewe... Kusoma kasoma yeye ili apate kula na kuishi yeye na familia yake.. Bakhersa hajasoma kumbuka lakini anamuona mwenye Degree ni Fala tu...

Inamaana Mwakyembe siku akikutana na Yesu atamuambia wewe Yesu hujasoma utanishauri nini? IQ aliyotumia Waziri ni Ujinga... aache kujimwambafai...
 
Roma katupa Jiwe Gizani Kwa kupitia fasihi kama tawi la sanaa🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿

Kilicho cha Haki kitafika tu kwa mlengwa hata akiwa nyuma ya duniaaa

Vivaaa akili kubwaaaa
Viva Mwana Hip Hop halisi
Viva baba Ivan
Viva sauti ya wanyongee

Vivaaa Romaaaaaaaa
 
"Kama msanii unang'ang'ana kuimba siasa na kukosoa serikali basi amua kuachana na muziki uanzishe chama cha siasa. Lakini kama unataka kupata maslahi kwenye muziki, basi nyimbo hizo hazilipi. Haiingii akilini nina shahada nne halafu msanii ambaye hajaenda hata shule anatunga nyimbo za kunikosoa. Wewe na darasa la nne lako sijui la 7 utanionya mimi mwenye degree nne na nimefundisha vyuo vikuu mbalimbali?" Dr.Harisson Mwakyembe (PhD), Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo.!

Imbombo jilipo!!!
 
Roma. Tunga wimbo verses nakupa hapa chini, ujue mwanasiasa chunga ulimi kwa Mwanahabari na Msanii, haya tayari huyu babu ni mteja wa msanii, anampa verses kirahisi kabisa;

Roma drs la nne lakini anatisha wa Degree 4, angesoma je?

Elimu haipatikani darasani tu, hata chini ya mti ukapata mafundisho, pengine hata marishoni unaweza fundishwa.mfani jando na unyago

Samweli Doe alikuwa na Dgree? mbona alisumbua?

Idd Amin Dada hata certificate hakuwa nayo, lakini aliitisha Israel

Hitre alitawala Dunia darasa la 2 tu, na wenye Elimu ulaya wakakoma mpaka leo wanalia.

Bakhresa? mbona wasomi wanalipwa mishahara kupitia yeye, anakopesha serikali ya kina Kabudi

Roma anapata hela nyingi kuliko Mwakyembe, uongo jamani

usiogope muimbe hivo tu, na mengine ongeza,
Chorus...........
 
"Kama msanii unang'ang'ana kuimba siasa na kukosoa serikali basi amua kuachana na muziki uanzishe chama cha siasa. Lakini kama unataka kupata maslahi kwenye muziki, basi nyimbo hizo hazilipi. Haiingii akilini nina shahada nne halafu msanii ambaye hajaenda hata shule anatunga nyimbo za kunikosoa. Wewe na darasa la nne lako sijui la 7 utanionya mimi mwenye degree nne na nimefundisha vyuo vikuu mbalimbali?" Dr.Harisson Mwakyembe (PhD), Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo.!

Hakika nakuambieni" kama mtaani kwako hakuna kichaa,jitizame vizuri unaweza kuwa wewe"
 
Degree nne tena? Hawa watu jamii ya Mwakyembe mbona miguu na njia kwa waganga wa kienyeji often kupata "ushauri wa kitaalamu" ingawa hao hata std 3B hawakuliona?

Kitendo cha Waziri kushuka chini na kuanza kujibizana na "standard 4/7" ni ishara tosha hizo degree 4 zilikuwa za kudesa na kukariri tu na wala hazijamsaidia kitu. Otherwise ile sumu ilimuharibu pakubwa
 
Back
Top Bottom