Roma na wenzake wapatikana, wapelekwa Kituo cha Polisi Oysterbay kisha Mwananyamala Hosp na kuachiwa

Roma na wenzake wapatikana, wapelekwa Kituo cha Polisi Oysterbay kisha Mwananyamala Hosp na kuachiwa

Msanii Roma Mkatoliki anadaiwa kupatikana na yupo Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar.

Habari ya akina Roma kupatikana imethibitishwa na Mkurugenzi wa Tongwe Records J. Mada.

Bado hakuna maelezo ya kutosha kuhusiana na wapi walipokuwa na nani waliokuwa wamewashikilia. Kwa sasa wanadaiwa kuwepo kituoni hapo kwa taratibu za kipolisi kwa kuwa jalada la kupotea kwao lilifunguliwa hapo.

Kupatikana kwao kumefuatia wito mkubwa uliokuwa ukipaishwa na wasanii wenzake na mashabiki kuhusu kuachiliwa huru, ndani na nje ya mitandao ya kijamii.

Awali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro alisema bado walikuwa wakiendelea na upelelezi wa tukio la kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake.

Taarifa zaidi zinafuata..

Hadi sasa bado polisi wanamhoji kituoni na kuna waandishi wa habari wapo wanamsubiria pamoja na wadau wengine wa muziki
Waliohojiwa na waandishi ni pamoja na msanii Ney wa Mitego na Rais wa shirikisho la wasanii nchini Simon Mwakifamba

Mwakifamba kasema hivi sasa wamepata nafuu maana hata yeye alikuwa anaogopa

Ney wa Mitego amehojiwa na kusema hii inathibitisha Muziki wa Hip Hop unasikilizwa na watu wengi na una mchango kwenye jamii na wataendelea kuimba

View attachment 492792
View attachment 492791

Bora maana tulikosa raha
 
BASHITE UTATUMIA NGUVU NYINGI KUJISAFISHA
 
Hivi mamlaka zinasemaje kuhusu Ben ? Maana kama Roma aliahidiwa kabla ya jumapili je kwa ndugu yetu Ben ganzi ipo wapi
Mi nafikiri ni muda muafaka sasa kwa mzee wetu saa nane na yeye aende na timu ya waandishi wa blogs kwa RC wa Dar, apatiwe ufumbuzi na ahadi timilifu, kuliko kukaa analalamika kwa kina Sirro.
 
Hizo zinawork kwako tu na wajinga wengine
Ukiwa akili ndogo ni ngumu kutambua kwamba akili yako ni ndogo na kwako kushinda argument ni more important than anything else. Kwa hiyo tufanye tu kwamba mimi ni mjinga na wewe ni mwerevu I hope hii itaboost self-esteem yako na kujiona wewe ndo bingwa humu ndani..😀
 
Serkal iache uhuni isizan watanzania wa sasa wale wa kale, watanzania tunaona sana na kutambua uhuni unaofanywa na serkal, wanataka kutuambia serkal haiusk na uhuni huo
 
Daktar huru ampime polonium, sarin, cyanide, ricin tujue kama wamemtengua neva ya kutungia mistar na atuambie ilikuwaje huko
Kinachoshangaza wamepelekwa mwananyamala..kwani wana malaria?
 
Kama kweli kamanda sirro anatakiwa kuwajibishwa kwa kutoa Taarifa za uongo maana alikanusha kuwa hakuna kituo kinacho mshikiria, lakin kwa upande mwingine tumsamehe tu mzee wawatu kwa sababu mzee wawatu alikuwa msafi ila anatiwa najisi bila ridhaa hana namna mzee wawatu anapitia kipind kigumu sana sasa nadhana atakuwa anataman mda wa kustaafu ufike haraka ili kikombe hiki akihepuke.
Soma vizuri story line . utajua kafikaje hapo
 
Sasa tusubiri kesho watakapo andaliwa mkutano na waandishi wa habari na ili waongee kile walichofundishwa kuongea na kutoa shukrani nyingi sana,kumpamba mkuu wa mkoa na maharamia wenzake.

Mkutano huo utadhaminiwa na GSM.
Nilikuwa naota tu ila yatatokea coz jicho langu la rohoni limeona.

Aibu kubwa sana kwao.
 
Back
Top Bottom