Roma na wenzake wapatikana, wapelekwa Kituo cha Polisi Oysterbay kisha Mwananyamala Hosp na kuachiwa

Roma na wenzake wapatikana, wapelekwa Kituo cha Polisi Oysterbay kisha Mwananyamala Hosp na kuachiwa

Jamani naomba kuuliza!!
Ati yule kijana aliyekuwa anapitapita hapa anauza karanga yupo wapi?!! Muvi lineshanoga sidhani kama nitatoka sasa hivi maana kuna screen mbili hapa, moja Roma nyingine bado haijawashwa ya Nape.
 
Hapa nimeamini walichukuliwa ili issue itrend then leo wawatoe ili kuzima mkutano wa nape. Hii nchi kiki hadi kwenye uhai wa mtu aisee. Sipati picha kama tungekaa kimyaaa yangetokea ya saa8
 
Ujinga tu..Wanatumia kodi zetu kwa mambo ya kijinga
Pesa inayotumika kumtetea Daud Bashite, faru huko mbugani, kuwakata wanasiasa kuwasafirisha usiku kuwapa majaji wapindishe sheria inatosha kujenga kiwanda cha Toyota vx Dodoma na serikali wakaacha kuagiza japan zikanunuliwa nchini na kwa Nchi jirani.
 
Sasa jamiiforum inakuwa kama magazeti ya udaku tu. Nani mwenye uhakika kuwa Bashite ndie alie mshikilia?
Ina maana hata kutafsili picha huwezi au ni hizo posho unazopewa zimekupofusha? Inawezekanaje mtu akasema atahakikisha amepatikana kabla ya j2 na kweli amepatikana leo tusiwe wanafki kwa vitu vilivyo wazi
 
Mwenendo wa kuwaweka Watanzania roho juu upigwe vita kila kona nchini tena kwa nguvu zetu zote. Kama si kelele zetu Watanzania si ajabu Roma angepotea kama Ben Saanane.

Sasa tupaze sauti zetu kwa nguvu zetu zote Ben Saanane naye arudishwe akiwa hai na mzima wa afya. Waliowateka akina Roma ndiyo hao hao waliomteka Ben Saanane.
 
Nnilipomuona makonda anavyoongea jana na ile body language nikajua anajua mahali roma alipo...
Yani hata mtt wa chekechea angeujua huu mchezo. Kuanzia mkutano wa Bashite kule WCB, kuja post ya Diamond kuhusu upoteaji wa Roma, kisha post ya babu tale, na halfu ile body language ya Bashite Jana, ukiunganisha dots huna hata haja ya kufikiria mara mbili km Bashite anahusika na hii movie ambayo director wake ni James wann(pombe)
 
Hivi ni nani anatunga Slogani za kampeni za CCCM? Awamu hii ya tano wangeweka slogani ya Maigizo, Viini macho na kiki ndo kipao mbele cha serikali hii ya Awamu ya tano Ila ile ya serikali ya viwanda wamebuma lakini wasichelewe Slogan siyo bibilia wala msaafu wabadilishe tu tutawaelewa.
 
Wameamua kumwachia bado Ben Saa nane sijui watamwachia lini?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ina maana hata kutafsili picha huwezi au ni hizo posho unazopewa zimekupofusha? Inawezekanaje mtu akasema atahakikisha amepatikana kabla ya j2 na kweli amepatikana leo tusiwe wanafki kwa vitu vilivyo wazi
Kwahiyo leo Mbowe akisema Ben atapatikana, inamaana yeye ndie atakuwa kamshika au ni hizo posho mnazopewa na nyie?
 
Back
Top Bottom