Hizi nchi mbili Uingereza na Marekani naona mara nyingi zinatumia nguvu yao kiuchumi kuwaumiza wasio na hatia na bahati mbaya hakuna anayewalaumu.
Mfano, Marekani alivamia Iraq tukaambiwa kuna nyuklia, lakini hakuna chochote walichowahi kutuonesha mpaka leo, wakavamia tena Libya kwa kisingizio kile kile lakini hakuna walichotuonesha hata baada ya vita ile.
Nashangaa leo wanamuhukumu Abramovich kwasababu tu ana urafiki na Putin, kwao hili ni kosa kubwa wameamua kumuadhibu, naona dunia tunayoishi inaendeshwa na mataifa makubwa mawili yaliyojaa unafiki wa hali ya juu sana.
I wish hao wachina nao wawe na nguvu zaidi kiuchumi waje kuwalainisha hao wajuaji wawili.