Rombo: Amuua mkewe na kisha kujinyonga

Rombo: Amuua mkewe na kisha kujinyonga

Inabidi wanandoa wauwane mpaka wazazi tunapowaambia hatutaki kuoa watuelewe. Maana wengi tunaoa kwa shinikizo la wazazi
 
Haya matukio yanakuwa common Sana nowdays,

Mungu tuepushe na hili pepo.
 
Kama umefanikiwa kupata watoto/ mtoto kabla hujaoa basi usioe lea wanao chapa mbususu maisha yaendelee.

Kama huna mtoto basi tafuta tu mtoto ila achana na mambo ya kuoa.

Ndoa ni moto, kuoa ni kukumbatia moto huku ukijua fika kua ni moto.
Kweli kabisa

Kuoa ni majanga

Ova
 
Ndoa ni kwa ajili ya Mwanaume mwenye akili timamu ilikuwaje huyu bibie akaolewa na huyo mwehu
 
Mwenyekiti wa kitongoji cha Urua chini, kijiji cha Mfuruashe wilayani Rombo, Agustine Moshi(35) amemuua mkewe, Anastasia Agustine (31) kwa kumkata kata na kitu chenye ncha kali na kisha mwenyewe kujiua kwa kujinyonga kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mshereheshaji maarufu wilayani humo (MC), anadaiwa kutenda mauaji hayo usiku wa kuamkia leo Novemba 8, 2021.

Akithibitisha kutokea kwa mauaji hayo leo Novemba 8, Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maiga amesema wawili hao walikuwa na mgogoro wa kimapenzi, ambapo wiki moja iliyopita mke wake huyo alimpeleka dawati la jinsia Rombo.

"Huyu jamaa wiki iliyopita mke wake alimpeleka dawati la jinsia hapa wilayani, walisuluhishwa lakini inaonekana halikuisha na ni suala ambalo inaonekana ni wivu wa mapenzi, hivyo akaamua kuchukua jukumu la kumuua mkewe na kisha kujiua kwa kujinyonga," amesema Kanali Maiga.

Kanali Maiga amesema wanandoa hao wameacha watoto watatu wadogo.

MWANANCHI
Haya maamuzi yanasikitisha sana, ni kheri kuwa single kuliko ku force kuwa double mazafantaz
 
Haya mambo ya wanandoa kuuana kisa wivu wa mapenzi mbona yanazidi kuongezeka sikuhizi!

Kama unajijua una hasira mbaya na huwezi kuzicontrol bora usioe wala kuolewa
Labda serikali inawatoa kafara wananchi wake
 
Haya mauaji yangekuwa yanatokea MARA yangetrend BALAA.

Ila kwa kuwa yanatokea sehemu nyingine. Easy!
 
Kuachana ni kuzuri sana pale inapobidi sema watu hawajuagi tu.

Kuachana kunaepusha mambo kama hayo ya mauaji.

Halafu huwa nawashangaa Viongozi wa dini na ndugu jinsi wanavyolazimishaga mapatano fake ya kinafiki.

Talaka zina faida yake.
Mwanaume yakikuzidi usijali mali na nyumba uliyojenga. Nenda mbali upate amani ya moyo wako.
 
Back
Top Bottom