Muuza Kangala
JF-Expert Member
- Jul 21, 2021
- 1,242
- 4,813
MAHAKAMA ya Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro imemuhukumu Valency Panclas Mtales (43) mkazi wa kijiji cha Mamsera chini, Kwenda jela miaka 30, kwa kosa la kumlawiti mwanaume mwenzie mwenye umri wa miaka 24.
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Regina Futakamba Machi 22 mwaka huu baada ya Mahakama kujiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na mashahidi wanane wa upande wa mashitaka.
Mahakama hiyo chini ya kifungu namba 154 kifungu cha kwanza A cha sheria ya kanuni ya adhabu namba 16 ambayo imefanyiwa marejeo mwaka 2022 ilimtia hatiani mshitakiwa huyo na kutumikia kifungo cha miaka 30 gerezani.
Chanzo: Nipashe