Romy Jones ndani ya bifu zito na Lamata!

Unakumbuka nilikuahidi? Ndio natekeleza kwa vitendo sasa.
Nikileta ubuyu sasa hivi ni exclusive tu, huwezi kuupata kokote!
Umetisha Mama la Mamaa, sisi Wazee kazi yetu ni kutulia zetu kwenye Mkeka huku tumefunga Msuli wakati tukipeluzi Ubuyu wa moto moto kutoka kwa the Queen herself Nifah 🤗
 
Kama ndiivyo basi RJ kazingua sababu hali yake kifedha haikuwa nzuri ndio maana akaanza kujiongeza. Anatakiwa akumbuke kwanini aliitafuta hiyo kazi.

Pale kwa kaka Mondi mambo ya fedha si rahisi kwa kila mtu.
Mwenzangu ana madeni na maisha ya wasanii si unayajua tena?

Ila angemshirikisha Lamata wakajua namna ya kupanga ratiba zake za shootings, kazi hafanyi anataka maokoto.

Mondi kumpa kazi ya kuwa DJ wake rasmi ni bonge la mchongo, hana deni.
 
Watengeneze scene RJ awe kama ameenda kusoma Marekani tena ingenoga kweli maana inge waacha watazamaji kwenye suspense kujua kama jamaa atarudi na cheti ama laaaaaaah director ana kwama wapi
Tatizo ameshazingua sana Lamata amechoka na wasanii wenzie pia hawamtaki.
Hapo kazi kufanyika ni vigumu.
 
Kwa hili nasimama na RJ..

Lamata Sasa kazidi mara ya kwanza alikuwa Neila..Akabadilishwa sasa Bill Jr hapana aisee
 
Nifah mwaka huu kwenye ubuyu hutaki utani.

Wakianzisha nyuzi za mwisho wa mwaka za wachangiaji walioshinda JF idara ya ubuyu nakupigia kura.
 
Nifah mwaka huu kwenye ubuyu hutaki utani.

Wakianzisha nyuzi za mwisho wa mwaka za wachangiaji walioshinda JF idara ya ubuyu nakupigia kura.
Lols!
Asante Mkuu…

Kama umenishawishi kesho niwape ubuyu mwingine hiviiiiii, ninao tele kabatini mwangu.
Ni mimi kuchagua upi wa kuweka na upi wa kusubiri.
 
Lols!
Asante Mkuu…

Kama umenishawishi kesho niwape ubuyu mwingine hiviiiiii, ninao tele kabatini mwangu.
Ni mimi kuchagua upi wa kuweka na upi wa kusubiri.
Weka weka ubuyu.

Halafu ubiyu wako unauweka newsy newsy hivi.

Ubuyu umepimwa kwa viwango vya TBS 🤣🤣

Hatuwezi kuwa tunaongea ma logical fallacy ya logical non sequitur muda wote.

Kazi na dawa 🤣🤣🤣
 
Kwa lolote lile nasimama upande wa RJ.

RJ ni mtu poa sana.
Ni kweli mkuu. Mwaka 2018 nilimpa kazi ya kunitangazia biashara yangu alinifanyia kwa uaminifu wa hali ya juu kama tulivyokubaliana. Pia aliniunganisha na dogo mmoja wa Graphics ambaye naye ni mtu makini na ninafanya nae kazi hadi leo. Romy Jones ni mtu mwema sana. Katika hili siko upande wowote ila ninawasihi wakae chini na kuliweka hili jambo sawa kwa maslahi mapana ya pande zote.
 
Sasa kosa la Lamata ni nini? Mtu hajatokea kutimiza wajibu wake, anaibuka anataka hela.
Tena kwenye igizo ambalo linaendelea…
Sababu zake zinaelezeka mbona ila lamata sio msikiliza wa Sababu za wenzake anajali kazi kuliko utu..
Nakumbuka Naila (Menina) alifiwa na mumewe na wakati huo kajifungua bado anataka aende kwenye Scene kushoot aangalie utu kwanza mengine baadae
 
Mimi pia namkubali mno RJ, ila katika hili kazingua.
Ile ni kazi, kukosekana kwa RJ kama moja ya wahusika wakuu katika tamthilia kuna gharama hadi ya kubadili mtiririko mzima wa story.

Usimtetee sababu ya Wasafi Festival, ana makosa kweli.
Huko Wasafi wanalipana Tsh ngapi? Nahisi pesa wanazolipana ni haba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…