Romy Jones ndani ya bifu zito na Lamata!

Romy Jones ndani ya bifu zito na Lamata!

Weka weka ubuyu.

Halafu ubiyu wako unauweka newsy newsy hivi.

Ubuyu umepimwa kwa viwango vya TBS 🤣🤣

Hatuwezi kuwa tunaongea ma logical fallacy ya logical non sequitur muda wote.

Kazi na dawa 🤣🤣🤣
Basi kesho nauweka kwa heshima yako 🤣🤣🤣

Ubuyu mzito, utatikisa ndoa ya mtu mjini hapa.
 
Sababu zake zinaelezeka mbona ila lamata sio msikiliza wa Sababu za wenzake anajali kazi kuliko utu..
Nakumbuka Naila (Menina) alifiwa na mumewe na wakati huo kajifungua bado anataka aende kwenye Scene kushoot aangalie utu kwanza mengine baadae
Kwa Menina inaweza kuwa kweli alikuwa na makosa ila sio katika hili la RJ.

RJ kazingua, na ndio maana anahaha kumtafuta Lamata waongee wayaweke sawa.
 
Mi ndio nilikuwa nakutegemea wewe ujue?
🤣🤣🤣

Ngoja basi nitawaomba wafuatiliaji wengine watatuambia.
Ila wasanii kazi kama hizi waangalie namna ya kuziweka rasmi
Wawe na mikataba na ratiba zinazo eleweka mtu akikiuka sheria na taratibu zifuatwe
Maana itawakuta mpo kwenye scene mtu ataitwa na mama yake nyumbani ata waacha hapo
 
DJ maarufu nchini, Romeo George ‘Romy Jones’ ameingia katika bifu zito na bosi wake katika tasnia ya filamu mwanamama Leah Mwendamseke ’Lamata’ kwa kile kinachodhaniwa kuwa vita ya kimaslahi.

Wawili hao wamefanya kazi kwa mafanikio katika tamthilia maarufu nchini ya Jua Kali, kabla ya kuibuka kwa majukumu mapya yaliyomzidia Romy Jones kutimiza wajibu wake wa kushiriki ktk tamthilia hiyo.

CHANZO NI WASAFI FESTIVAL!
Ikumbukwe kuwa, licha ya Romy Jones kuwa ndugu wa damu wa Diamond Platinumz, ndiye DJ wake rasmi katika kila tamasha la muziki atakaloshiriki.

Hiyo imepelekea Romy Jones kuwa busy kutokana na utitiri wa shows nyingi ndani ya tamasha hilo ambalo Diamond kama muasisi na mmiliki amewekeza nguvu zake nyingi huko kwa kushiriki binafsi katika kila mkoa ambao kuna ratiba ya kufanyika kwa Wasafi Festival.

Romy Jones baada ya kutingwa na matamasha, akakosa kushiriki kwa ukamilifu na pengine kutokushiriki kabisa kwa sehemu kubwa katika tamthilia hiyo.

Kitendo hiki kilimuumiza sana Lamata ambaye ndiye aliyempa nafasi ya kuigiza kwa mara ya kwanza kupitia tamthilia hiyo kubwa na ilikuwa bahati tu kwa mujibu wake mwenyewe Romy Jones kutokana na mahojiano kadhaa aliyowahi kuyafanya juu ya ushiriki wake katika tamthilia hiyo na nyingine za Kiswahili.

Balaa baina yao lilizuka pale Romy Jones alipokwama kwenye mambo yake, huku akitaka kupewa malipo kutoka kwa uongozi wa Jua Kali ambako hakuwa ameonekana katika shooting kadha wa kadha.

Lamata kama bosi wa tamthilia hiyo hivi sasa amepumzika kwa kiasi kikubwa majukumu kutokana na ujauzito wake kufikia ukingoni karibuni na kujifungua, aliingilia kuweka sawa baada ya mzozo mkubwa kuibuka kati ya mhasibu wake na Romy Jones juu ya malipo.

Alimpigia simu RJ na kuzozana nae kwa kumpa ukweli wa mambo jinsi gani anavyokwamisha shooting, na kutoa maagizo RJ atumiwe laki moja katika simu kwa ajili ya mafuta ya gari kwa RJ kisha amfuate Lamata alipo wakajadili kwa kina, na ikiwa ni pamoja na kulipwa stahiki zake zote.

RJ hakukubaliana na hilo, punde laki moja ilipoingia kupitia simu yake na mhasibu kupiga simu kuthibitisha, RJ akagombana na mhasibu kisha akaurudisha muamala.
Yeye RJ alitaka kuongea wayaweke sawa na sivyo Lamata alivyotaka ‘kumalizana’ nae.

Hadi ninavyoandika hapa, kuna uwezekano mkubwa wa Billy Jr. kutokuonekana tena katika tamthilia ya Jua Kali baada ya kuchokwa na kila mmoja hadi wasanii wenzie kwa ‘uzinguaji’ wake.

RJ mwenyewe anahaha huku na huko kuomba kikao na Lamata bila mafanikio…

Ndimi,

Nifah


View attachment 2844179View attachment 2844182
R.i.P warumi
 
Lakini Romy namuonaga mstaarabu sana, sikutegemea!

Ila kama amewahi kumzingua ndugu yake Diamond mpaka akamsimamisha kazi haishangazi.
Mbabaishaji tu kipimo cha ustaarabu ni pale unapokamilisha kazi ya mtu pindi anapokuamini na ukiona hutaweza unaweka wazi ili mtu atafute njia nyingine, siyo unapokea kazi alafu unaanza kusumbua
 
Back
Top Bottom