Ronaldinho alikuwa zaidi ya Messi Barcelona

Pia Dinho alishinda tuzo ya mwanasoka wa Dunia kipindi hata Malaika wanadekea soka.
Sio kipindi hiki cha Soka kanjanja lililojaa salakasi na uhanithi wa Blatter.

Dinho kashinda tuzo Zidane, De Lima, Figo, Del Piero, Shevshenko, na alama nyingine za Soka zikiwa uwanjani na kwenye pic ya hatari.

Hakika Dinho ni mbarikiwa.
 
ni mchezaji pekee aliyekuwa anapiga pasi huku akiangalia sehemu nyingine kabisa na pasi inafika kwa mlengwa,hakika aliutendea haki mpira na mpir4a ulikuwa unampenda
 
Piga ua garagaza mzee mzima Gaucho alikuwa king Barca nimeamua kumlinganisha na Messi baada ya kuona mafanikio alioyapata akiwa Barca


kaka nakupa tano! Hakika mimi toka nimekua, nimemuona Maradona,Matheus, Zizou, na wengine lakini Naamini sijawahi kuona ka Gaucho.alikua na kila kitu ambacho mchezaji anapaswa kuwa nacho, kuanzia, skills , speed, ball control, flexible, techniques na vionjovingio vingine.alikua ana uwezo wa kutumia miguu yote miwili ukilinganisha na Messi.Kwangu mie kinachombeba Messi ni mguu wa Kushoto.Kwa mtu aliecheza mpira watu wa mguu wa kushoto ni ngumu kumkaba unapotumia mguu wa kulia, kwani muda mwingi anaelekea ,Angle ambayo ni rahisi kumfanyia faul.
Umenifanya nifurahi, kwamba siko peke yangu naeamini katika Dinho!
 
Last edited by a moderator:
Hakunaga zaidi ya Ronaldinho pale Barca... Messi bado sana.... badooooo
 
Dinho ni mtu mwingine kabisa, bado sijaona mtu aliyekua anajua kuchezea mpira wa uwanjani kama yeye. Ila inabidi tujue kuwa kila Nabii na wakati wake hivyo pamoja na ukosefu wa wachezaji wenye kuujua haswa mpira kwa Zama hizi likini Messi kidogo anasifa nyingi zinazokaribia na kile kizazi cha kina Zidane, Lonaldo de Lima, Dinho, Mandieta, Nedved, Edgar Devds, etc maana hawa kweli ushindani ulikua mkubwa kumpata mkari zaidi yao.
 
Daa nikikumbuka lile goli alilowafunga chels huku anakata viuno aaa dinho ni hatare, messi mi nakwambia ni mchezaji wa kawaida sana anaebebwa na timu na mpira wake mlaini wa redcard kwa upinzani kila mara kukiwa na gem ngumu
 


Wanasema " Ukiwa peke yako darasani utakua wa kwanza hata kama hukufaulu"
 
Kwa mliotangulia kukoment wote nawaunga mkono,,, hakuna kama Gaucho na tunapoenda sidhani kama atatokea kama yeye,,
 
Kila mtu na zama zake! Dinho ni entertainer wakati Messi ni mtu wa kazi. Ni kama Dansi (Dinho) na Hip Hop (Messi).
 
Kila mtu na zama zake! Dinho ni entertainer wakati Messi ni mtu wa kazi. Ni kama Dansi (Dinho) na Hip Hop (Messi).


Ebana hebu nyamazia hapohapo.
Narudia kusema Dinho alishushwa ili kutuonesha soka la Mbinguni linavyochezwa.
Unaposema Messi mtu wa kazi then Gaucho ni Entertainer unachuma dhambi, ndio mana nakwambia nyamazia hapohapo.

Kuna vitu Gaucho kavipata kwa kuvitokea jasho, huyo Nesi wako hajavipata.
Sasa je nani ni mtu wa kazi hapo?

Anaitwa Ronaldo De Assis Morreira almaarufu kama Ronaldinho Dinho Gaucho.
Mtu huyu awapo uwanjani inaaminika Malaika huacha shughuli zao huko mbinguni na kumuangalia.
 
soka tofauti na ngoma ya mdumange kwamba anayekatika vizuri ndo mshindi. chezea messi weye!
 
Dah, Mkuu hii ni mpya hebu fafanua.


Hakuwepo Dimbani, ila alikuwepo jukwaani.
Na screen za uwanja zilivyomvuta dah uwanja ulilipuka kwa yowe huku mashuka makuuubwa yenye maandishi ya kumtukuza na kumsifu mtakatifu huyu yakiwa yanapepea.

Washabiki mpaka wa timu pinzani waliungana na washabiki wa AC Milan waliokuwa wamefurika katika Dimba la Sansiro na kuanzia Dakika ya 77 mpaka dakika ya 93 mpira ulipoisha walikuwa wanashangilia na kuimba nyimbo za kumtukuza Dinho Magic.
na ndipo mtangazaji pale uwanjani akamtangaza Dinho kuwa MTM.
 
soka tofauti na ngoma ya mdumange kwamba anayekatika vizuri ndo mshindi. chezea messi weye!


na unapotaka kumfananisha Saint Gaucho na Nesi basi unatakiwa uanze na neno 2002 world Cup Winner Ronaldo de Assis Morreira also known as Ronaldinho Dinho Gaucho...

Hah hah hah haaaaah mchezaji aliewahi kupata kufanya miujiza katika dimba la El Santiago Bernabeu na kupelekea washabiki viburi wa Madrid kuinuka na kumpigia makofi huku wakimsujudia.
Kwa wachezaji wa Barca ni Dinho na Maradona tu waliowahi kupewa heshima hiyo na washabiki wa Madrid.

Chezea Dinho wewe?
Utaarisha.
 
Sifa tumpe lakini ukweli lazima tuuseme,,, ronaldinho, ametisha sana miaka ya 2002 to 2006 baada ya kuja barcelona na miaka hiyo zidane alikuwa anapotelea ndo anastaafu, ronaldo de lima hakuna kitu anaishia, na del piero ndo kabisaaaa so hata yeye hakuwa na competitors wenye peak,,,

Messi anaelekea mbele golini, hana mambo ya kuuza sura kama dinho timu imefungwa lakini dinho anacheka cheka tu,,, messi mtu wa kazi..

Tukatae tukubali messi yupo juu zaidi ya dinho ndo maana wachambuzi wanamuweka level ya best player of all time..

Messi anawekwa class ya kina pele, maradona...

Wakati ronaldinho anawekwa class ya kina ronaldo original, matheus, na wengineo lakini sio level ya kina pele na maradona
 

Wewe kweli unampenda huyu mtu sio kidogo! Big up.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…