Akili zingine ni za kijinga hadi zimepitiliza. Hapo juu kabisa ya jedwali kuna link, hiyo link ukiifuata itakuletea jedwali hili hili original, sasa sijui una sababu gani za kutaka kubishana na redio.
Muda gani Messi atakuchukua kumfikia Gaucho halikuwa swali, nilikuwa NAKEJELI. Ukiwa na akili timamu, utagundua kuwa rekodi zinaonesha kuwa Messi yupo mbele, kwa MAGOLI, VIKOMBE, POPULARITY, FEDHA, THAMANI na UMUHIMU.
Kama chenga ziliwapendeza, basi mjue kuwa Barca wao wamependezwa na soccer. Hivyo unavyoviita vitu adimu, Austin 'Jay Jay' Okocha alivifanya kwenye kombe la Dunia 1994 Marekani na bado havikumfanya awe mwanasoka bora wa dunia.
Mtaumiza kichwa kwa Jealous zenu. Mnakataa hata takwimu kwa wivu,.....by the way, hivi navyokujibu, Barcelona keshamkandamiza Malaga 2 na ni dkk ya 69. Mbao ya kwanza imewekwa kimiani na Lionel Andres 'Leo' Messi na la pili, Cesc Fabregas. Mtaumwa sana mwaka huu na marehemu wenu huyo