Ronaldo de Lima: Kizazi changu ilikuwa ngumu kuwa bora Duniani

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
" Kizazi changu ilikuwa ngumu kuwa bora Duniani" - R9

Gwiji wa kandanda Ronaldo Nazario De Lima ametoa mtazamo wake kuhusu Cristiano Ronaldo na Lionel Messi , kwa kudai kwamba ilikuwa ngumu sana kutambulika kuwa bora Duniani katika kizazi chake.

Ronaldo alikuwa mfalme wa kuweka kambani miaka kadhaa iliyopita na sasa anaangalia soka kwa mbali akiwa Balozi wa Real Madrid.

Licha ya kwamba alikuwa muwazi kwamba Muargentina na Mreno wataendelea kushindana katika tuzo za mchezaji bora Duniani, Ronaldo ametaja ugumu wa kuwa bora Duniani katika kizazi chake.

" Katika kizazi changu kuwa bora Duniani ilikuwa ngumu sana kuliko sasa, bila kutaka kuwashusha Messi na Ronaldo." Alisema Ronaldo alipokuwa kwenye mahojiano na Sport Bild.

" Watashindana katika tuzo ya mchezaji bora wa Dunia katika miaka ijayo , lakini katika kipindi changu kulikwa na [Zinedine] Zidane, Rivaldo, [Luis] Figo, na Mimi na baadae akaja Ronaldinho."

" Hiko ni kizazi ambacho kuwa bora Duniani ilikuwa ngumu sana."

Amesema de lima
 
Hakuna lolote, kwa huyu mashoto Messi hawa wangekuwa wanafikiria kuanzia nafasi ya tatu huko. Yaani simshabikii Messi, lakini nahisi uwezo wake unazidi chuki zangu kwake.
 
Au shadrack nsajigwa.
Dah Fuso Shedrack Nsajigwa. Kuna jamaa nilikutana naye 2011 alikuwa akiishi tabata karibu na fuso Shedrack Nsajigwa. Anasema jamaa alikuwa anajituma kweli kwenda gym uhani kwa jirani yake baadaye anauza genge sijui duka lake jion anawahi mazoezin Na yanga. Nilimpinga kichizi jamaa.

Je Ni kweli mnayemjua Nsajigwa Fuso?
 
Amemaliza kila kitu Ronaldo De Luis Nazario Lima...The Phenomena alikua bora katika kizazi cha dhahabu kwa sasa Messi na Ronaldo wanajaribu tu
 
alichokisema Rinaldo kinaukweli kiasi lakini niktika upande wa ushindani wakizazi chao...nasio katk ubora alionao messi ama cristiano ronaldo na wao...ktk hao aliowataja watu wanaopaswa kuingizwa ktk compatation ya baina ya messi na cristiano kwa mbali ni ronaldo mwenyew na zidane bhasiiii na bado ubora wao haufikii hata kwa messi..mtu aliyeweza kupiga goal 91 ktka msimu mmoja mtu aliyeweza kuchkua tuzo NNE bora ya fifa katika miaka mi4 mfululizo ..mtu ambaye ameivusha agentina nakuipeleka world cup tena kwa nguvu zake nzito kiasi Kile mtu ambaye amekuwa anafnya vyema kila baada ya miaka 2 ..waweza kumfananisha nahao kina delima..delima alikuwa nimchezaji mzuri mnoo lakini alizungukwa na wachezaji wazuri pia ktk team yao ya taifa...watu kama gaucho rivaldo na kaka huwezi acha kuwataja mbele ya mafanikio ya delima katk team ya taifa ..ukimtazama messi kuanzi upigaji chenga ..kasi ..uwezo wakutoa Pasi za mwisho mpaka uwezo wakuzifumania nyavu .hakuna wakumuweka level moja nae hapa....kiasi anajitahidi cristiano nanikatk upande wa magoli tu pekee ...lakini sio ukokotaji mpira wala upigaji chenga wla pasi za mwisho na jinsi ambavyo anaichezesha team
Mara kibao tumekuwa tunaona messi akiwa hayupo na barca NAyO haina pumzi..itazame barca ilivyoondokewa na neymar ..ilivyoondokewa na gaucho ..hakuna aliyetegemea kama itakuwa katk level hizi ..yote hiyo nikwaajili ya uwezo wa messi
zidane alikuwa anacontrol mnoo anapiga chenga pia na kuichezesha team pia...but hakuwa mpigaji mzuri wa mipira iliyokufa kama messi hakuwa mwenye uwezo mkubwa wakupiga chenga watu wanne mpka wa tano kama messi ..hakuwa mfungaji bora hata siku moja ..hakuwahi kuwa nakasi kama messi..hakuwahi na pasi za mwisho nyingi kama messi...messi nimchezaji aliyetemia na uwezo wake dhidi hayo wachezaji waliotajwa hapo nivitu vinavyotengana kama maji na mafuta ..messi kawaacha mbali mnoo
 
hamna lolote kizazi Cha R9. Kizazi kilichokuwa Na challenge kubwa Ni 1992 -1996 hata ukifuatilia UEFA championship league kufunga goli hata moja enzi hizo ilikuwa ngumu. AC Milan Na Ajax Amsterdam, Barcelona Na marceile ya ufaransa.

AC Milan
1. Dejan Cecicevic mserbia
2 . Paulo maldin
3. Franco Baresi
4. Rais George Weah
5. Albertini
6. Boban, ambaye haruna Moshi kaiga Hilo jina kutoka kwake alikuwa mcroatia

Juventus
1. Ravaneli fabrazio
2. Roberto Baggio
3. Gianluca Viali

Beryan Munich
Lother Matthias
2. Oliver bierhoff
3. Jurgen klinsman
4. Rudi voller

Borrusia Dortmund

Chapuisat
Mathias summer
Victor ikpeba mnigria

Marseille
1. Abedi pele

Real Madrid
Ivan Zamorano mchile huyu

Barcelona
Romario
Ronald koeman
Hristo stoichkov

Sasa wanaume Yani enz hizo tishio Na Ni nyakati hizo R de lima alikuwa kinda uholanzi psv pamoja Na gaucho. AJAX AMSTERDAM Dah Ajax ilikuwa tishio chini ya kocha Luis Vaan Gal

Naanza Na waafrika watatu kutoka Nigeria waliipaisha Ajax

Sunday Oliseh
Finidi George
Nwanko Kanu

Wengine

.Frank rijkaard
.Frank de Boer
.Ronald de boer
Patrick cluivert alikuwa 19 yes alipofunga goli la pekee UEFA chmp league 1994 dhidi ya Ac M
ilan
. Clarence seedorf
.edagR davis
. Reinziger
Jari litmanen
. Edwin van der saar

Jezi Yao ilidhaminiwa Na ABN amro bank

Hiki ndio kizazi Cha mpira wenye changamoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…