britanicca
JF-Expert Member
- May 20, 2015
- 16,295
- 33,994
" Kizazi changu ilikuwa ngumu kuwa bora Duniani" - R9
Gwiji wa kandanda Ronaldo Nazario De Lima ametoa mtazamo wake kuhusu Cristiano Ronaldo na Lionel Messi , kwa kudai kwamba ilikuwa ngumu sana kutambulika kuwa bora Duniani katika kizazi chake.
Ronaldo alikuwa mfalme wa kuweka kambani miaka kadhaa iliyopita na sasa anaangalia soka kwa mbali akiwa Balozi wa Real Madrid.
Licha ya kwamba alikuwa muwazi kwamba Muargentina na Mreno wataendelea kushindana katika tuzo za mchezaji bora Duniani, Ronaldo ametaja ugumu wa kuwa bora Duniani katika kizazi chake.
" Katika kizazi changu kuwa bora Duniani ilikuwa ngumu sana kuliko sasa, bila kutaka kuwashusha Messi na Ronaldo." Alisema Ronaldo alipokuwa kwenye mahojiano na Sport Bild.
" Watashindana katika tuzo ya mchezaji bora wa Dunia katika miaka ijayo , lakini katika kipindi changu kulikwa na [Zinedine] Zidane, Rivaldo, [Luis] Figo, na Mimi na baadae akaja Ronaldinho."
" Hiko ni kizazi ambacho kuwa bora Duniani ilikuwa ngumu sana."
Amesema de lima