Rose Mayemba: Nimefukuzwa Makao Makuu kama mbwa na walinzi wa Mbowe. Aeleza Rushwa ya Freeman Mbowe ilivyokwamisha Uchaguzi Mkoa wa Njombe usifanyike

Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Njombe, Rose Mayemba, amedai kutengwa na kunyimwa haki ya kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi wa chama, pamoja na kufanyiwa fujo na walinzi wa chama.

Akizungumza Januari 19, 2025, Dar es Salaam, Mayemba alisema changamoto hizo zilijitokeza wakati wa usaili wa nafasi za Kamati Kuu uliofanyika Makao Makuu ya CHADEMA, ambapo alihisi haki yake ya kupiga kura ilikiukwa.

"Nimekwenda Makao Makuu ya CHADEMA kufanya usaili wa nafasi za Kamati Kuu. Mimi nina wajibu wa kumtafutia mgombea wangu, Tundu Lissu, kura. Ninamuunga mkono hadharani kutokana na sera alizozieleza na hali ya sasa nchini inayomhitaji zaidi kuliko mtu mwingine yeyote,"

Source: Jambo TV
 
Mpka sasa CHADEMA imepoteza credibilit mbele ya watanzania. Sioni cha maana watakachokifanya ili kurudisha imani
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Njombe, Rose Mayemba, amedai kutengwa na kunyimwa haki ya kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi wa chama, pamoja na kufanyiwa fujo na walinzi wa chama.

Akizungumza Januari 19, 2025, Dar es Salaam, Mayemba alisema changamoto hizo zilijitokeza wakati wa usaili wa nafasi za Kamati Kuu uliofanyika Makao Makuu ya CHADEMA, ambapo alihisi haki yake ya kupiga kura ilikiukwa.

"Nimekwenda Makao Makuu ya CHADEMA kufanya usaili wa nafasi za Kamati Kuu. Mimi nina wajibu wa kumtafutia mgombea wangu, Tundu Lissu, kura. Ninamuunga mkono hadharani kutokana na sera alizozieleza na hali ya sasa nchini inayomhitaji zaidi kuliko mtu mwingine yeyote,"

View attachment 3207184

Source: Jambo TV
Safi sana nampenda sana huyu anaishi siasa ya kweli na wito wa kweli
 
Kwani taratibu zinasemaje? Ofisi za Chadema ni mahali pa kufanyia kampeni? Hivi akitokea mtu nae akaanza kumfanyia kampeni Mbowe ingekuwaje? Hao waliomtoa walikuwa wanataka kuepusha shari. Kwenye hili alikosea. Huu ni wakati wa kushusha na sio kupandisha joto. Labda kama lengo ni kupandisha joto ili wadai wanaonewa.

Awe na subra. Mwenyekiti ana nafasi za kuteua wajumbe wa Kamati Kuu. Lissu akishinda hatamtupa.

Amandla...
 
Back
Top Bottom