Hivi yeye mwenyewe huyu huwa ana shughuli gani rasmi hapa duniani ukiondoa hii ya MSEMAJI WA FAMILIA zisizomhusu?
Zamani nilikuwa namchukulia powa huyu mtu lakini sivyo alivyo nilikuwa najidanganya mwenyewe.
Kuna watu duniani wamezaliwa na vipaji maalum hata ukitaka kukutana na Rais wapo watu wapo nje ya serikali wanaweza kukufanyia booking na Rais lakini mtumishi wa ikulu akashindwa.
Huyu Steve baada ya mimi mwenyewe binafsi kutokana na shughuli zangu nimeweza kumjuwa japo kidogo, ilikuwa lazima tuonane na kuzungumza.
Huyu Steve tangu enzi za JK ana access na wakuu wa nchi na kwa sasa ana direct access kwa makamu wa Rais.
Huyu Steve licha ya kwamba gari si mafanikio lakini anatembelea Toyota Prado Tx ya kisasa kabisa na ana dereva.
Huyu huyu Steve kuna mibaba mizima tena walikuwa masustaa wakweli yeye ndio mwenyekiti wao kwenye Uzalendo kwanza, hili ni kundi la watu maarufu kupiga pesa za serikali inayopenda kusifiwa.
Usisahau kwenye hilo kundi wapo Mohammed Hussein Mmachinga, Steven Nemes, Mtwa Kiwelu, Chama Jogoo, Makumbi Juma, Madaraka Suleiman na wengine wengi waliowika kwenye soka la bongo na wasanii wa Bongo Movie lakini ujuwe mwenyekiti wao na founder wa hilo group ni Steve Nyerere.
Kama nia yako tu ni kumjuwa mtu huyu nadhani utakuwa umekiona kitu ndani ya mtu huyu, na nimemshuhudia kwa macho hawa mastaa wote anawamudu na anawagombeza wakizinguwa.
Ningekuwa na mamlaka pale UDSM ningempa degree ya heshima huyu dogo.
Kwenye harusi ndio usiseme kuna harusi moja ya kitajili itafanyika hivi karibuni nimealikwa kikao cha maandalizi mwenyekiti Jack Ghotham, makamu ni huyuhuyu Steve, na bwana harusi ni wale watu wenye shilling yao hapa mjini.
Kwa uchache huyo ndio Steve, ukisikia mtaani kwenu watu wanamsema fulani magari yake ni ya kuazima waambie na wao wakaazime basi kama wataaminiwa kupewa.