Rose Shirima hana kosa lolote, mwenye Makosa ni James Getogo kuibua makosa ya serikali/mwajiri wake

Kesi kama hizi zinamfaa rais kama Magufuri. Kama angekuwepo, mtu angepanda cheo pale
 
Kwa sisi ambao ni walaji hatuhitaji sana kujua ni kwa nini James alirekodi ile video, hatuhitaji kujua kama walikuwa na mahusiano wakaachana bali tu kujua kuwa kuna uwezekano wa kwenda hosp ya serikali na ukapimwa kwa kutumia vitendanishi vilivoisha muda wake.
Ni wazi ktk hili James lazima asulubishwe lakini yeye kaweka ukweli hadharani, sisi ambao si wa kada hiyo hatupaswi kushughulika sana na kiapo,miongozo na miiko ya kazi ya James.
James hawezi kupona ktk hili kwa sababu ni uozo ulionzia juu kushuka chini, kwa kuthibitisha hilo tayari mara moja zile MRDT zilizo expire ziliondoshwa na kuacha zilizobakisha miezi minne ku expire, sitaki kuamini kama James alichanganyikiwa kiasi hicho ashindwe kujua kuwa hizo MRDT bado zina uhai wa miezi minne.

Sisi kama watazamaji wa video ile hatupaswi kuwa na jukumu la kujua majibishano yalianza wapi, bali ujumbe uliobebwa na hiyo clip.
 
Niliishawahi kumnyang'anya na kupasua simu ya workmate wangu baada ya kugundua anamrekodi workmate mwenzake wakiwa pamoja. Tabia ya kipumbavu kabisa!!!
 
Hakuna atakayefukuzwa hapo, wote watapigwa onyo kali na kuhamishiwa mbwinde
 
Hivi wewe hayo maelezo unayoandika unamaanisha video umeiona pekeyako au?
 
Ndio unaulizwa kosa la Rose ni lipo hapo ambalo litamfukuzisha kazi
Wale wote hakuna atakaefukuzwa kazi, Ila rose kama ameweza kuonyesha nyodo zile kwa mtumishi mwenzie vipi kwa wagonjwa?
 
Hapo Tatizo ni moja tuhh ambalo hamlifaham,watalaam wa maabara, na hawa manurse, clinical officer, yani huwa hawaelawani kabisa, kwa hiyo wanafanya kazi kwa kukomoana, mkifuatilia hili swala kwa ukaribu mtajua tuhh.

Hilo tukio ingekua nurse kwa nurse au mtaalam wa maabara kwa mtaalam hatungeona haya mambo..

Yani wana ugomvi baridi toka kitambo sana,,,,
 
Akili za James ni kama za mtoto wa Chekechea
 
Ila dada nesi ni black beauty moja matata sana sasa ukiongeza na dharau zake ndo ananimaliza kabisa.
 
Rose shirima amekwama sana, kama huna mood ya kumjibu mtu kaa kimya

James atakua amezingua (kama yeye ndiye aliyerekodi hiyo video) nje ya hapo anatakiwa apongezwe na apandishwe cheo kwa kusimamia maadili ya kazi yake
 
Kwani imethibitika hiyo video amerekodi James..?
 

Unaposema kaweka Ukweli Hadharani unamaanisha nini?
Unajua maana ya ukweli?

Alionyesha hivyo vifaa vilivyo-expire kwenye video ili kuthibitisha maneno yake?
Kama hakuonyesha, unawezaje kusema ameongea ukweli?

Bado James yupo katika Wakati Mgumu kuthibitisha Madai yake.
Unapotaka kuongea Jambo lolote hadharani itakupasa uwe na vithibitisho ili upate uungwaji mkono.

Lakini kuongea tuu bila kutoa ushahidi WA kile unachoongea inaweza Isiwe nzuri Kwa mtoa hoja.
Ni hatari sana.

Nikimtetea James Getogo huenda ni kweli alichosema lakini approach aliyoitumia sio nzuri. Na ili ujue sio nzuri Angalia kinachoenda kutokea.
 
Rose hana baya na mtu
Ila ni kama jamaa alikua na jambo lake pasono😁😁😁😁
 
Haya sasa James ndo kafukuzwa kazi.Mwenye namba ya Rose nimwoe tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…