Mcharo son
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 4,718
- 3,804
Kesi kama hizi zinamfaa rais kama Magufuri. Kama angekuwepo, mtu angepanda cheo fasta
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa sisi ambao ni walaji hatuhitaji sana kujua ni kwa nini James alirekodi ile video, hatuhitaji kujua kama walikuwa na mahusiano wakaachana bali tu kujua kuwa kuna uwezekano wa kwenda hosp ya serikali na ukapimwa kwa kutumia vitendanishi vilivoisha muda wake.ROSE SHIRIMA HANA KOSA LOLOTE, MWENYE MAKOSA NI JAMES GETOGO KUIBUA MAKOSA YA SERIKALI/MWAJIRI WAKE
Anaandika, Robert Heriel.
Watanzania Wengi tunapenda Sana mambo ya kudandia dandia mambo. Kufuata Mkumbo. Kwenye nchi hii ni rahisi Sana kumchafua MTU na watu wakaamini na kumuona MTU Fulani ni Mbaya.
Taikon natumia Kanuni moja, ukija Kwa upole utajibiwa Kwa upole, ukija kishenzi utajibiwa kiushenzi.
Turudi kwenye mada
Kama ukiitazama Ile video inayoonyesha majibizano makali kiasi ya maafisa wa Afya WA zahanati ya Isgihimulwa Tabora ya Rose Shirima na James Getogo, bila kutumia mihemko basi utagundua Rose Shirima Hana kosa lolote.
Mwenye Makosa hapo ni James Getogo.
Zipo sababu zinazonifanya kuwa na mtazamo huo, sababu hizo ni kama ifuatavyo;
1. Mratibu wa njama na Msaliti.
Mchukua kamera ambaye bila Shaka ni James Getogo akiwa kama kinara wa kutelekeza njama hiyo Kwa lengo alilokuwa analijua yeye mwenyewe.
Ni aibu kuwa na mfanyakazi katika serikali au kampuni au hata kwenye familia kama alivyo James Getogo. Unajua ni kwanini?
Serikali inasiri nyingi, taasisi za Elimu zinamapungufu mengi Mno. Hata hapo nyumbani kwako ulipo yapo makorokoro mengi Sana. Lakini mkiwa kama wanafamilia, au wafanyakazi wa ofisi moja kazi yenu ni kujua nini chakufanya ili kukabiliana na hayo matatizo yalipo.
Lakini sio mmoja wenu kuchonga njama ili kuibua uozo wa familia, au serikali au kampuni. Huyo hafai popote pale.
James Getogo hataonekana kama shujaa Bali ataonekana kama MTU asiyetambua nini anafanya. James Getogo ni Msaliti hafai.
Video Ile ilipaswa irekodiwe na MTU wa nje asiyehusika na hiyo zahanati ndio ingekuwa na ujiko/mantiki.
Lakini kurekodiwa na MTU wa ndani hiyo ni njama. Maana ofisini MTU anaweza kukujaza alafu bila ya wewe kujua akawa anakurekodi ukaonekana wewe ndiye mbaya.
2. Makosa katika Video.
Ile video inamakosa kama ifuatavyo;
I/ video imeanzia katikati,
hatujui walianzia wapi, na mchukua video alipoona amepata alichokuwa anakikusudia akaamua aache kurekodi.
ii/ video imechukuliwa na mshtaki(ambaye ni Be. James Getogo).
Ile video ingekuwa na maana endapo mshitakiwa na mshitaki wangekuwa wanarekodiwa pasipo ya wao kujua ili kuondoa Ile dhana ya njama.
Sasa Be. James ndiye anarekodi unafikiri yeye angetumia Lugha gani kujibishana na MTU asiyejua anarekodiwa?
Au unafikiri Rose Shirima angejua anarekodiwa angeongea maneno makali?
Kumchongea Rose Shirima Kwa kumrekodi video ATI kisa katoa maneno ya shombo sio Pouwa! Hata wewe hapo ofisini kwako MTU anaweza kuja Kwa namna ya kukuchokoza na kukupa karaha mpaka ukajikuta unatoa maneno makali kumbe unarekodiwa, alafu video ikitumwa mtandaoni inarushwa kipande chenye maneno yako makali.
3. Makosa ya kimajukumu na kiwajibu.
Huyo James Getogo ashaambiwa na mfanyakazi mwenzake Aende Kwa incharge alafu anang'ang'aniza kumjaza Muuguzi wa Watu, ulitegemea Muuguzi angemchekea au kumjibu Kwa upole kama yupo Kanisani? Hata Kanisani kuna Wakati hakuna mambo ya upole.
Kifaa kama kime-expire ulitaka Muuguzi afanyeje sasa. Kosa lake ni lipi hapo? Yeye kakuambiwa ndio kime-expire lakini kinaweza kutumika, swali lililokuwa linafuata hapo lingetakiwa; je hakuna hatari yoyote Kutumia kifaa kilicho-expire? Hapo Rose angejieleza kulingana na uelewa wake na Elimu yake. Nani ajuaye kuwa huenda Rose anaelimu Fulani kuhusu vitu ku-expire na muda wake wa matumizi(hiyo ni juu yake sasa)
Alafu huyu James Getogo mpaka anaelekezwa na Rose Shirima kuwa Aende Kwa Incharge kwani yeye hajui taratibu za hiyo Zahanati?
Kumfukuza Kazi Rose Shirima haitakuwa Sawa. Na utakuwa uamuzi wa ajabu Sana.
Majukumu ya Muuguzi yanafahamika.
Matatizo ya namna hiyo maofisini yanapotokea hasa katika mahospitali kunakuwaga na vikao vya Asubuhi kujadili nini kimefanyika, changamoto na kupeana majukumu Kwa Siku Mpya.
James Getogo hakujua kuwa ishu ya vikao ili alete shauri lake kwenye vikao.
Kama huyo Rose Shirima anatabia mbovu ya kujibu Watu nyokonyoko(ambayo sio Tabia nzuri) je ilishindikana kumuweka kwenye kikao wakiwepo wakubwa wake wa kazi?
Au James Getogo alitaka kuiaminisha jamii ya kitanzania kuwa Rose Shirima anamdomo mchafu Kwa clip moja tuu iliyoanzia katikati tena aliyoirekodi yeye?
Come on! Tuache masikhara!
Sitetei Tabia ya majibu ya hovyohovyo na nyokonyoko Kutoka Kwa watumishi WA umma ila najaribu kuelezea kuwa yapo mazingira majibu ya nyokonyoko yanaweza kujitokeza accidentally.
Pia, najaribu kueleza kuwa ni Tabia Mbaya Kwa mfanyakazi au mwanafamilia kutoa nje madhaifu ya ofisi, kampuni au serikali Kwa Watu wasiohusika. Ni usaliti Mkubwa. Pia ni nje ya maadili ya Kazi.
Rose Shirima arudishwe kazini. Huyo James Getogo apewe onyo kali au akapewe semina. Ingawaje ingekuwa kwenye Ofisi binafsi basi angekuwa amefukuzwa kazi muda mrefu Sana.
Sio kazi ya mfanyakazi kufichua maovu ya ofisi anayofanyia Kazi. Hiyo sio kazi yako.
Waachie wenye kazi Yao ambao ni Sisi Raia.
Kumchomesha mwenzako Kwa Aina yoyote tena Kwa Watu wasiohusika Sisi kina Taikon tunaita ni uzuzu! Usaliti na kutojitambua.
Watanzania wengi watamshambulia Rose lakini kimsingi Rose hana kosa lolote. Tena apandishwe cheo.
SABATO NJEMA
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Iangalie hiyo video hapo Chini bila mihemko
Kesi kama hizi zinamfaa rais kama Magufuri. Kama angekuwepo, mtu angepanda cheo fasta. Kuna nyakati linapokuja suala la haki ya mtu kuishi, sheria inaweza kukaa kando kidogo
Hakuna atakayefukuzwa hapo, wote watapigwa onyo kali na kuhamishiwa mbwindeHapo ndio utajua kuwa unapotaka kutatua Jambo unatakiwa ushirkishe Akili yako vyema.
Sasa hapo James Getogo anakazi ngumu Sana kuliko mwenzake.
Huyo Rose ataonywa tuu lakini hawezi kufukuzwa kazi.
Huwezi tatua tatizo Kwa kuzalisha matatizo zaidi, huo sio utatuzi Bali kuleta matatizo.
Hivi wewe hayo maelezo unayoandika unamaanisha video umeiona pekeyako au?Unajua hauelewi kilichotokea,
Mtu wa maabara kawasilisha hoja kuwa Vifaa vya MRDT Test vime-expire.
Rose kamuambia Vitumike kwa wajawazito.
James akasema hawezi kuvitumia,
Rose akasema, basi nenda Kwa incharge.
James kakataa kwenda Kwa incharge.
Rose kasema basi usitumie
James akasema vitumie wewe,
Yaani ni majibizano lakini kama vingetumika Muuguzi asingehusika na madhara kwani mhusika wa vipimo ni MTU wa maabara yaani James,
Alichofanya James ni kuibua Makosa ya serikali/mwajiri wake. Na huyo Rose hapo hiyo kesi haitamuumiza sana
Nchi hii hawashindwi na jambo😂😂
Kwamba Muuguzi anajua kabisa anarekodi, hapo mwanzoni kamera ilivyokuwa inatingishika ni kama aliangalia kamera😀
Nchi hii hawashindwi na jambo
Hivi wewe hayo maelezo unayoandika unamaanisha video umeiona pekeyako au?
Wale wote hakuna atakaefukuzwa kazi, Ila rose kama ameweza kuonyesha nyodo zile kwa mtumishi mwenzie vipi kwa wagonjwa?Ndio unaulizwa kosa la Rose ni lipo hapo ambalo litamfukuzisha kazi
Akili za James ni kama za mtoto wa ChekecheaROSE SHIRIMA HANA KOSA LOLOTE, MWENYE MAKOSA NI JAMES GETOGO KUIBUA MAKOSA YA SERIKALI/MWAJIRI WAKE
Anaandika, Robert Heriel.
Watanzania Wengi tunapenda Sana mambo ya kudandia dandia mambo. Kufuata Mkumbo. Kwenye nchi hii ni rahisi Sana kumchafua MTU na watu wakaamini na kumuona MTU Fulani ni Mbaya.
Taikon natumia Kanuni moja, ukija Kwa upole utajibiwa Kwa upole, ukija kishenzi utajibiwa kiushenzi.
Turudi kwenye mada
Kama ukiitazama Ile video inayoonyesha majibizano makali kiasi ya maafisa wa Afya WA zahanati ya Isgihimulwa Tabora ya Rose Shirima na James Getogo, bila kutumia mihemko basi utagundua Rose Shirima Hana kosa lolote.
Mwenye Makosa hapo ni James Getogo.
Zipo sababu zinazonifanya kuwa na mtazamo huo, sababu hizo ni kama ifuatavyo;
1. Mratibu wa njama na Msaliti.
Mchukua kamera ambaye bila Shaka ni James Getogo akiwa kama kinara wa kutelekeza njama hiyo Kwa lengo alilokuwa analijua yeye mwenyewe.
Ni aibu kuwa na mfanyakazi katika serikali au kampuni au hata kwenye familia kama alivyo James Getogo. Unajua ni kwanini?
Serikali inasiri nyingi, taasisi za Elimu zinamapungufu mengi Mno. Hata hapo nyumbani kwako ulipo yapo makorokoro mengi Sana. Lakini mkiwa kama wanafamilia, au wafanyakazi wa ofisi moja kazi yenu ni kujua nini chakufanya ili kukabiliana na hayo matatizo yalipo.
Lakini sio mmoja wenu kuchonga njama ili kuibua uozo wa familia, au serikali au kampuni. Huyo hafai popote pale.
James Getogo hataonekana kama shujaa Bali ataonekana kama MTU asiyetambua nini anafanya. James Getogo ni Msaliti hafai.
Video Ile ilipaswa irekodiwe na MTU wa nje asiyehusika na hiyo zahanati ndio ingekuwa na ujiko/mantiki.
Lakini kurekodiwa na MTU wa ndani hiyo ni njama. Maana ofisini MTU anaweza kukujaza alafu bila ya wewe kujua akawa anakurekodi ukaonekana wewe ndiye mbaya.
2. Makosa katika Video.
Ile video inamakosa kama ifuatavyo;
I/ video imeanzia katikati,
hatujui walianzia wapi, na mchukua video alipoona amepata alichokuwa anakikusudia akaamua aache kurekodi.
ii/ video imechukuliwa na mshtaki(ambaye ni Be. James Getogo).
Ile video ingekuwa na maana endapo mshitakiwa na mshitaki wangekuwa wanarekodiwa pasipo ya wao kujua ili kuondoa Ile dhana ya njama.
Sasa Be. James ndiye anarekodi unafikiri yeye angetumia Lugha gani kujibishana na MTU asiyejua anarekodiwa?
Au unafikiri Rose Shirima angejua anarekodiwa angeongea maneno makali?
Kumchongea Rose Shirima Kwa kumrekodi video ATI kisa katoa maneno ya shombo sio Pouwa! Hata wewe hapo ofisini kwako MTU anaweza kuja Kwa namna ya kukuchokoza na kukupa karaha mpaka ukajikuta unatoa maneno makali kumbe unarekodiwa, alafu video ikitumwa mtandaoni inarushwa kipande chenye maneno yako makali.
3. Makosa ya kimajukumu na kiwajibu.
Huyo James Getogo ashaambiwa na mfanyakazi mwenzake Aende Kwa incharge alafu anang'ang'aniza kumjaza Muuguzi wa Watu, ulitegemea Muuguzi angemchekea au kumjibu Kwa upole kama yupo Kanisani? Hata Kanisani kuna Wakati hakuna mambo ya upole.
Kifaa kama kime-expire ulitaka Muuguzi afanyeje sasa. Kosa lake ni lipi hapo? Yeye kakuambiwa ndio kime-expire lakini kinaweza kutumika, swali lililokuwa linafuata hapo lingetakiwa; je hakuna hatari yoyote Kutumia kifaa kilicho-expire? Hapo Rose angejieleza kulingana na uelewa wake na Elimu yake. Nani ajuaye kuwa huenda Rose anaelimu Fulani kuhusu vitu ku-expire na muda wake wa matumizi(hiyo ni juu yake sasa)
Alafu huyu James Getogo mpaka anaelekezwa na Rose Shirima kuwa Aende Kwa Incharge kwani yeye hajui taratibu za hiyo Zahanati?
Kumfukuza Kazi Rose Shirima haitakuwa Sawa. Na utakuwa uamuzi wa ajabu Sana.
Majukumu ya Muuguzi yanafahamika.
Matatizo ya namna hiyo maofisini yanapotokea hasa katika mahospitali kunakuwaga na vikao vya Asubuhi kujadili nini kimefanyika, changamoto na kupeana majukumu Kwa Siku Mpya.
James Getogo hakujua kuwa ishu ya vikao ili alete shauri lake kwenye vikao.
Kama huyo Rose Shirima anatabia mbovu ya kujibu Watu nyokonyoko(ambayo sio Tabia nzuri) je ilishindikana kumuweka kwenye kikao wakiwepo wakubwa wake wa kazi?
Au James Getogo alitaka kuiaminisha jamii ya kitanzania kuwa Rose Shirima anamdomo mchafu Kwa clip moja tuu iliyoanzia katikati tena aliyoirekodi yeye?
Come on! Tuache masikhara!
Sitetei Tabia ya majibu ya hovyohovyo na nyokonyoko Kutoka Kwa watumishi WA umma ila najaribu kuelezea kuwa yapo mazingira majibu ya nyokonyoko yanaweza kujitokeza accidentally.
Pia, najaribu kueleza kuwa ni Tabia Mbaya Kwa mfanyakazi au mwanafamilia kutoa nje madhaifu ya ofisi, kampuni au serikali Kwa Watu wasiohusika. Ni usaliti Mkubwa. Pia ni nje ya maadili ya Kazi.
Rose Shirima arudishwe kazini. Huyo James Getogo apewe onyo kali au akapewe semina. Ingawaje ingekuwa kwenye Ofisi binafsi basi angekuwa amefukuzwa kazi muda mrefu Sana.
Sio kazi ya mfanyakazi kufichua maovu ya ofisi anayofanyia Kazi. Hiyo sio kazi yako.
Waachie wenye kazi Yao ambao ni Sisi Raia.
Kumchomesha mwenzako Kwa Aina yoyote tena Kwa Watu wasiohusika Sisi kina Taikon tunaita ni uzuzu! Usaliti na kutojitambua.
Watanzania wengi watamshambulia Rose lakini kimsingi Rose hana kosa lolote. Tena apandishwe cheo.
SABATO NJEMA
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Iangalie hiyo video hapo Chini bila mihemko
Kwani imethibitika hiyo video amerekodi James..?Huyo MTU anayetoa siri ni Nani? Hiyo ndio Mantiki.
Elewa nilichokiandika,
Kwa hiyo kosa la Rose Shirima hapo ni lipi?
Hapo James Getogo angetafuta Mgonjwa wa kutengeneza ndio afanye alichokifanya, lakini kuifitinisha ofisi unayofanyia kazi sio njia sahihi.
Kwa sisi ambao ni walaji hatuhitaji sana kujua ni kwa nini James alirekodi ile video, hatuhitaji kujua kama walikuwa na mahusiano wakaachana bali tu kujua kuwa kuna uwezekano wa kwenda hosp ya serikali na ukapimwa kwa kutumia vitendanishi vilivoisha muda wake.
Ni wazi ktk hili James lazima asulubishwe lakini yeye kaweka ukweli hadharani, sisi ambao si wa kada hiyo hatupaswi kushughulika sana na kiapo,miongozo na miiko ya kazi ya James.
James hawezi kupona ktk hili kwa sababu ni uozo ulionzia juu kushuka chini, kwa kuthibitisha hilo tayari mara moja zile MRDT zilizo expire ziliondoshwa na kuacha zilizobakisha miezi minne ku expire, sitaki kuamini kama James alichanganyikiwa kiasi hicho ashindwe kujua kuwa hizo MRDT bado zina uhai wa miezi minne.
Sisi kama watazamaji wa video ile hatupaswi kuwa na jukumu la kujua majibishano yalianza wapi, bali ujumbe uliobebwa na hiyo clip.
Kwani imethibitika hiyo video amerekodi James..?