Rose Shirima hana kosa lolote, mwenye Makosa ni James Getogo kuibua makosa ya serikali/mwajiri wake

Hii video imeletwa maksud na kimkakati. Sasa hivi hatuzungumzii tena kuhusu "Diwani". Yani Tisi
 
Habari!
Kwa msingi wa kutoa haki na kwa kuwa umekili kuwa kuna mambo hatuyajui yalikoanzia basi, hakuna kukumu ya haki kwa kuzingatia tu yale maongezi tuliyoyaona.

Kuna mambo mengi nyuma ya pazia ambayo yanaweza kufanya hukumu kwao kuwa nzito au nyepesi, makosa kuwa mazito zaidi au mepesi.

Hivyo, tuwape nafasi watakaofatilia kwa ukaribu na kupata yaliyozunguka yukio zima, wapime kulingana na mazingira na sheria za kazi ndo wage na hukumu halisi na zingativu.
 
Watanzania kuanza sasa tuache kulialia maana sisi ndio tunatetea makosa ya kwamba eti ni mambo ya kawaida makazini.
Ukiwa waziri piga pesa atakayevujisha achukuliwe hatua kwa kuvujisha siri za serikali.
Askari kula rushwa watuhumiwa vunja miguu atakayevujisha ashitakiwe kwa kuvujisha siri za ofisi.
 
Imeshajulikana aliyerecord ana makosa:-
-Hana kibali cha kurecord.
-Amem-provoke kisha akamrecord,
-hakumtaarifu kuwa anamrecord, hii ni lazima na ndio maana eneo lenye recording camera linapaswa kuwekwa Warning ya individuals to watch their behaviour.


Sent from my TA-1004 using JamiiForums mobile app
 
Toka lini kuibua makosa ni kosa?

Unaweza ibua Makosa ya familia yako? Badala ya kutafuta namna ya kuyatatua?

Hivi Mkeo akiibua Makosa yako Mbele ya umma ni halali Kwa muono wako?
Au wewe unakampuni na ndio boss alafu mfanyakazi mmoja anaibua Mbele za umma Makosa ya kampuni yako ni Sawa?

Hapo angefanya MTU wa nje ingekuwa Sawa Kabisa.
Sio kama nakataa Watu wasifichue Makosa au maovu, lakini waangalie nafasi zao na majukumu yao
 
Tunaomba hiyo video tuisikie la tuwaachie waliyo iona waijadili.
 

Sasa tuambie kosa la Muuguzi hapo ni lipi? Au hujaiona hiyo video?
 
Aliyerekod alifanya sahihi , video angeipeleka ngazi za juu ( mkuu wao wa kazi ) hapo kituoni Kwa ajili ya utatuz .... Kosa alilolifanya may be kuiweka video public .. hlo ni kosa kubwa sana
inawezekana mkuu wake wa kazi anamla huyo nesi so amekuwa kiburi.
 
Aliyerekod alifanya sahihi , video angeipeleka ngazi za juu ( mkuu wao wa kazi ) hapo kituoni Kwa ajili ya utatuz .... Kosa alilolifanya may be kuiweka video public .. hlo ni kosa kubwa sana
Hao watumishi wote wawili hawana kosa.

Mwenye kosa hazungumzwi.

Kinachozungumziwa happy ni vipimo vya haraka vya Maralia yaani MRDT.

Hivi vipimo ni bure.

Wizara imeweka utaratibu wa kupima watu Maralia mara nyingi hasa wajawazito.

Na utaratibu wa uagizaji wa vifaa na dawa Bohari ya Dawa unawataka vituo kutolokea dawa au vifaa vinavyoexpire ndani ya miezi 3.

Ila Sasa, .........

Sometimes,MSD wanaamua kuchukua mzigo na kukuoetea ili usiharibie kwao, maana mzigo ukiiexpire kwako kuna majibu utatoa.

Kwahiyo ninachokiona hapo, matumizi ya hizo kits zilizoexpire zinatoa tafsiri zifuatazo:
  • Kwanza ni kukwepa kujibu kwanini zimeexpire kwako, maana yake hawapimi.
  • Pili, Wameletewa mzigo unaoexpire ndani ya muda mfupi, na kwa kuwa mfumo wa serikali ni wa kutishiana hawakuweza kukataa.
  • Kwenye ripoti za Manesi Kuna Data zinatakiwa na lazima uoneshe wajawazito wote wamepima Maralia. Sasa wakati nurse anataka wajawazito wapime ili mambo yaende, mtu wa maabara yeye anakwepa kwa kisingizio kuwa MRDT zime-expire. Hapo ndio wakaanza kutoleana maneno.
 

Kasome title vizuri ya Uzi huu ndio muhtasari wa maneno yako.
 
Hizi ni assumption tu, huwezi kuhukumu kwa mtindo huo.

Viwe vimeletwa vinakaribia kuisha muda, vimeletwa vimeisha muda wake, iwe mzigo ulikuwa mkubwa, iwe wateja walipungua bado taratibu ziko wazi.

Pia, kuna utaratibu by policy kama dawa au vitendanishi vikiisha muda wake ni nini kifanyike.

Kuna taratibu na miongozo ya jinsi ya kushughulikia makosa/misconduct sehemu yoyote ya kazi.

Mengine yote yatajengwa na yote yaliyozunguka tukio zima.
 
Hizi ni assumption tu, huwezi kuhukumu kwa mtindo huo.

Pia, kuna utaratibu by policy kama dawa au vitendanishi vikiisha muda wake ni nini kifanyike.
Hiyo Nini kifanyike ndio inayokwepwa hapo.

Kwasababu unadhani kwanini huyo Muuguzi alikuwa anataka vipimo vifanyike, ana manufaa yoyote kwa watu kutumia hivyo vipimo?

Hakuna.

Ishtoshe, MRDT vipimo ni bure.
 
Hiyo Nini kifanyike ndio inayokwepwa hapo.

Kwasababu unadhani kwanini huyo Muuguzi alikuwa anataka vipimo vifanyike, ana manufaa yoyote kwa watu kutumia hivyo vipimo?

Hakuna.

Ishtoshe, MRDT vipimo ni bure.
Nini kifanyike kitatokana na mazingira yote na kukusanya ushahidi.

Suala si mtu kunufaika, bali kutumia kitu kinyume na utaratibu kwa sababu majibu ya hizo device unaziverify vipi kana ni kweli au si kweli? Taratibu za kazi.

Ukienda kwa pilato hufukuliwa mengi sana ambayo huweza kukuzamisha kina kirefu au kukuokoa. Unaweza kupata maoni ya wafanyakazi wenzao pia kwa wapewa huduma mbalimbali.

Kuna maongezi, kuna ushahidi ndani ya kazi zao za kila siku, documentation ya vitu husika na vingine mpaka siku ya tukio na mienendo yao ya jumla ya kazi.

Pia, huyu aliye-record ataeleza kama ni yeye binafsi na nia yake na je ni yeye kaiingiza kwenye mzunguko?

Hapa ni full screening ya utendaji na tukio zima.
 
Kwa hiyo ulitaka mgonjwa apinwe kwa vipimo vilivyopitwa na wakati? Eti siri za Serikali kwenye uhai wa mtu No please

Hata kama karekodi huyo mtaalamu wa maabara nampongeza apandishwe cheo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…