Machame Juu
JF-Expert Member
- Jul 25, 2013
- 1,514
- 3,363
Hii video imeletwa maksud na kimkakati. Sasa hivi hatuzungumzii tena kuhusu "Diwani". Yani Tisi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari!ROSE SHIRIMA HANA KOSA LOLOTE, MWENYE MAKOSA NI JAMES GETOGO KUIBUA MAKOSA YA SERIKALI/MWAJIRI WAKE
Anaandika, Robert Heriel.
Watanzania Wengi tunapenda Sana mambo ya kudandia dandia mambo. Kufuata Mkumbo. Kwenye nchi hii ni rahisi Sana kumchafua MTU na watu wakaamini na kumuona MTU Fulani ni Mbaya.
Taikon natumia Kanuni moja, ukija Kwa upole utajibiwa Kwa upole, ukija kishenzi utajibiwa kiushenzi.
Turudi kwenye mada
Kama ukiitazama Ile video inayoonyesha majibizano makali kiasi ya maafisa wa Afya WA zahanati ya Isgihimulwa Tabora ya Rose Shirima na James Getogo, bila kutumia mihemko basi utagundua Rose Shirima Hana kosa lolote.
Mwenye Makosa hapo ni James Getogo.
Zipo sababu zinazonifanya kuwa na mtazamo huo, sababu hizo ni kama ifuatavyo;
1. Mratibu wa njama na Msaliti.
Mchukua kamera ambaye bila Shaka ni James Getogo akiwa kama kinara wa kutelekeza njama hiyo Kwa lengo alilokuwa analijua yeye mwenyewe.
Ni aibu kuwa na mfanyakazi katika serikali au kampuni au hata kwenye familia kama alivyo James Getogo. Unajua ni kwanini?
Serikali inasiri nyingi, taasisi za Elimu zinamapungufu mengi Mno. Hata hapo nyumbani kwako ulipo yapo makorokoro mengi Sana. Lakini mkiwa kama wanafamilia, au wafanyakazi wa ofisi moja kazi yenu ni kujua nini chakufanya ili kukabiliana na hayo matatizo yalipo.
Lakini sio mmoja wenu kuchonga njama ili kuibua uozo wa familia, au serikali au kampuni. Huyo hafai popote pale.
James Getogo hataonekana kama shujaa Bali ataonekana kama MTU asiyetambua nini anafanya. James Getogo ni Msaliti hafai.
Video Ile ilipaswa irekodiwe na MTU wa nje asiyehusika na hiyo zahanati ndio ingekuwa na ujiko/mantiki.
Lakini kurekodiwa na MTU wa ndani hiyo ni njama. Maana ofisini MTU anaweza kukujaza alafu bila ya wewe kujua akawa anakurekodi ukaonekana wewe ndiye mbaya.
2. Makosa katika Video.
Ile video inamakosa kama ifuatavyo;
I/ video imeanzia katikati,
hatujui walianzia wapi, na mchukua video alipoona amepata alichokuwa anakikusudia akaamua aache kurekodi.
ii/ video imechukuliwa na mshtaki(ambaye ni Be. James Getogo).
Ile video ingekuwa na maana endapo mshitakiwa na mshitaki wangekuwa wanarekodiwa pasipo ya wao kujua ili kuondoa Ile dhana ya njama.
Sasa Be. James ndiye anarekodi unafikiri yeye angetumia Lugha gani kujibishana na MTU asiyejua anarekodiwa?
Au unafikiri Rose Shirima angejua anarekodiwa angeongea maneno makali?
Kumchongea Rose Shirima Kwa kumrekodi video ATI kisa katoa maneno ya shombo sio Pouwa! Hata wewe hapo ofisini kwako MTU anaweza kuja Kwa namna ya kukuchokoza na kukupa karaha mpaka ukajikuta unatoa maneno makali kumbe unarekodiwa, alafu video ikitumwa mtandaoni inarushwa kipande chenye maneno yako makali.
3. Makosa ya kimajukumu na kiwajibu.
Huyo James Getogo ashaambiwa na mfanyakazi mwenzake Aende Kwa incharge alafu anang'ang'aniza kumjaza Muuguzi wa Watu, ulitegemea Muuguzi angemchekea au kumjibu Kwa upole kama yupo Kanisani? Hata Kanisani kuna Wakati hakuna mambo ya upole.
Kifaa kama kime-expire ulitaka Muuguzi afanyeje sasa. Kosa lake ni lipi hapo? Yeye kakuambiwa ndio kime-expire lakini kinaweza kutumika, swali lililokuwa linafuata hapo lingetakiwa; je hakuna hatari yoyote Kutumia kifaa kilicho-expire? Hapo Rose angejieleza kulingana na uelewa wake na Elimu yake. Nani ajuaye kuwa huenda Rose anaelimu Fulani kuhusu vitu ku-expire na muda wake wa matumizi(hiyo ni juu yake sasa)
Alafu huyu James Getogo mpaka anaelekezwa na Rose Shirima kuwa Aende Kwa Incharge kwani yeye hajui taratibu za hiyo Zahanati?
Kumfukuza Kazi Rose Shirima haitakuwa Sawa. Na utakuwa uamuzi wa ajabu Sana.
Majukumu ya Muuguzi yanafahamika.
Matatizo ya namna hiyo maofisini yanapotokea hasa katika mahospitali kunakuwaga na vikao vya Asubuhi kujadili nini kimefanyika, changamoto na kupeana majukumu Kwa Siku Mpya.
James Getogo hakujua kuwa ishu ya vikao ili alete shauri lake kwenye vikao.
Kama huyo Rose Shirima anatabia mbovu ya kujibu Watu nyokonyoko(ambayo sio Tabia nzuri) je ilishindikana kumuweka kwenye kikao wakiwepo wakubwa wake wa kazi?
Au James Getogo alitaka kuiaminisha jamii ya kitanzania kuwa Rose Shirima anamdomo mchafu Kwa clip moja tuu iliyoanzia katikati tena aliyoirekodi yeye?
Come on! Tuache masikhara!
Sitetei Tabia ya majibu ya hovyohovyo na nyokonyoko Kutoka Kwa watumishi WA umma ila najaribu kuelezea kuwa yapo mazingira majibu ya nyokonyoko yanaweza kujitokeza accidentally.
Pia, najaribu kueleza kuwa ni Tabia Mbaya Kwa mfanyakazi au mwanafamilia kutoa nje madhaifu ya ofisi, kampuni au serikali Kwa Watu wasiohusika. Ni usaliti Mkubwa. Pia ni nje ya maadili ya Kazi.
Rose Shirima arudishwe kazini. Huyo James Getogo apewe onyo kali au akapewe semina. Ingawaje ingekuwa kwenye Ofisi binafsi basi angekuwa amefukuzwa kazi muda mrefu Sana.
Sio kazi ya mfanyakazi kufichua maovu ya ofisi anayofanyia Kazi. Hiyo sio kazi yako.
Waachie wenye kazi Yao ambao ni Sisi Raia.
Kumchomesha mwenzako Kwa Aina yoyote tena Kwa Watu wasiohusika Sisi kina Taikon tunaita ni uzuzu! Usaliti na kutojitambua.
Watanzania wengi watamshambulia Rose lakini kimsingi Rose hana kosa lolote. Tena apandishwe cheo.
SABATO NJEMA
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Wapumbavu wengi tu wapo mtu akikutaa kakuepusha na magonjwaMwanaume kuwa na Akili za kipuuzi kama hivyo ni ushamba na Aibu
Hii video imeletwa maksud na kimkakati. Sasa hivi hatuzungumzii tena kuhusu "Diwani". Yani Tisi
Toka lini kuibua makosa ni kosa?
Watanzania kuanza sasa tuache kulialia maana sisi ndio tunatetea makosa ya kwamba eti ni mambo ya kawaida makazini.
Ukiwa waziri piga pesa atakayevujisha achukuliwe hatua kwa kuvujisha siri za serikali.
Askari kula rushwa watuhumiwa vunja miguu atakayevujisha ashitakiwe kwa kuvujisha siri za ofisi.
Video iko wapi wakuu
inawezekana mkuu wake wa kazi anamla huyo nesi so amekuwa kiburi.Aliyerekod alifanya sahihi , video angeipeleka ngazi za juu ( mkuu wao wa kazi ) hapo kituoni Kwa ajili ya utatuz .... Kosa alilolifanya may be kuiweka video public .. hlo ni kosa kubwa sana
Hao watumishi wote wawili hawana kosa.Aliyerekod alifanya sahihi , video angeipeleka ngazi za juu ( mkuu wao wa kazi ) hapo kituoni Kwa ajili ya utatuz .... Kosa alilolifanya may be kuiweka video public .. hlo ni kosa kubwa sana
Hao watumishi wote wawili hawana kosa.
Mwenye kosa hazungumzwi.
Kinachozungumziwa happy ni vipimo vya haraka vya Maralia yaani MRDT.
Hivi vipimo ni bure.
Wizara imeweka utaratibu wa kupima watu Maralia mara nyingi hasa wajawazito.
Na utaratibu wa uagizaji wa vifaa na dawa Bohari ya Dawa unawataka vituo kutolokea dawa au vifaa vinavyoexpire ndani ya miezi 3.
Ila Sasa, .........
Sometimes,MSD wanaamua kuchukua mzigo na kukuoetea ili usiharibie kwao, maana mzigo ukiiexpire kwako kuna majibu utatoa.
Kwahiyo ninachokiona hapo, matumizi ya hizo kits zilizoexpire zinatoa tafsiri zifuatazo:
- Kwanza ni kukwepa kujibu kwanini zimeexpire kwako, maana yake hawapimi.
- Pili, Wameletewa mzigo unaoexpire ndani ya muda mfupi, na kwa kuwa mfumo wa serikali ni wa kutishiana hawakuweza kukataa.
- Kwenye ripoti za Manesi Kuna Data zinatakiwa na lazima uoneshe wajawazito wote wamepima Maralia. Sasa wakati nurse anataka wajawazito wapime ili mambo yaende, mtu wa maabara yeye anakwepa kwa kisingizio kuwa MRDT zime-expire. Hapo ndio wakaanza kutoleana maneno.
Nimeiona, hapo huyo aliyerekodi ana makosa na nesi pia ana makosaNishaiweka hapo juu
Hizi ni assumption tu, huwezi kuhukumu kwa mtindo huo.Hao watumishi wote wawili hawana kosa.
Mwenye kosa hazungumzwi.
Kinachozungumziwa happy ni vipimo vya haraka vya Maralia yaani MRDT.
Hivi vipimo ni bure.
Wizara imeweka utaratibu wa kupima watu Maralia mara nyingi hasa wajawazito.
Na utaratibu wa uagizaji wa vifaa na dawa Bohari ya Dawa unawataka vituo kutolokea dawa au vifaa vinavyoexpire ndani ya miezi 3.
Ila Sasa, .........
Sometimes,MSD wanaamua kuchukua mzigo na kukuoetea ili usiharibie kwao, maana mzigo ukiiexpire kwako kuna majibu utatoa.
Kwahiyo ninachokiona hapo, matumizi ya hizo kits zilizoexpire zinatoa tafsiri zifuatazo:
- Kwanza ni kukwepa kujibu kwanini zimeexpire kwako, maana yake hawapimi.
- Pili, Wameletewa mzigo unaoexpire ndani ya muda mfupi, na kwa kuwa mfumo wa serikali ni wa kutishiana hawakuweza kukataa.
- Kwenye ripoti za Manesi Kuna Data zinatakiwa na lazima uoneshe wajawazito wote wamepima Maralia. Sasa wakati nurse anataka wajawazito wapime ili mambo yaende, mtu wa maabara yeye anakwepa kwa kisingizio kuwa MRDT zime-expire. Hapo ndio wakaanza kutoleana maneno.
Hiyo Nini kifanyike ndio inayokwepwa hapo.Hizi ni assumption tu, huwezi kuhukumu kwa mtindo huo.
Pia, kuna utaratibu by policy kama dawa au vitendanishi vikiisha muda wake ni nini kifanyike.
Nini kifanyike kitatokana na mazingira yote na kukusanya ushahidi.Hiyo Nini kifanyike ndio inayokwepwa hapo.
Kwasababu unadhani kwanini huyo Muuguzi alikuwa anataka vipimo vifanyike, ana manufaa yoyote kwa watu kutumia hivyo vipimo?
Hakuna.
Ishtoshe, MRDT vipimo ni bure.
Kwa hiyo ulitaka mgonjwa apinwe kwa vipimo vilivyopitwa na wakati? Eti siri za Serikali kwenye uhai wa mtu No pleaseHuyo MTU anayetoa siri ni Nani? Hiyo ndio Mantiki.
Elewa nilichokiandika,
Kwa hiyo kosa la Rose Shirima hapo ni lipi?
Hapo James Getogo angetafuta Mgonjwa wa kutengeneza ndio afanye alichokifanya, lakini kuifitinisha ofisi unayofanyia kazi sio njia sahihi.