Rose Shirima hana kosa lolote, mwenye Makosa ni James Getogo kuibua makosa ya serikali/mwajiri wake

Rose Shirima hana kosa lolote, mwenye Makosa ni James Getogo kuibua makosa ya serikali/mwajiri wake

Mimi ukiniletea video ya namna hiyo Kwa kweli sitakuelewa.
Video imerekodiwa na mshtaki.

Kwenye vikao vya kawaida ukishtaki ukweli mbona unakuwa wazi palepale.
Lakini hiyo ya kurekodi hiyo. Tena video inaanzia katikati, hiyo sio rahisi kuielewa.
mkuu bado hujanipata..sio kila mtu kaiona hiyo video..weka link.
 
sikubaliani na maamuzi ya jamaa kumrekodi na kusambaza mtandaoni ila Rose amepata alichostahili
kuleta zengwe kwenye uhai wa mwanadamu mwezio!!

Kosa la rose ni lipi?
Unajua ni mambo mangapi yanayofanyika kwenye nchi hii yanayohatarisha usalama wa Watu kisa umaskini wetu?
Au Kwa vile Rose karekodiwa tena bila ya kujua na aliyemrekodi ni mfanyakazi mwenzake
 
Hapa kwa kweli UMENENA... ningekuwa nafanya rating ningekupa A+++

Hayo majibizano mbona kila Siku yapo maofisini hasa Kwa watu/wafanyakazi wasiowaelewa. Unamuambia kitu MTU hasikii.

Sasa kama anajua vime-expire alitaka Rose afanyeje?
Rose kamuambia nenda Kwa incharge, James kang'ang'ania kumsimamia,
 
Kama mshkaji angekuwa mteja/Mgonjwa angekuwa sahihi Kwa kiwango kikubwa. Lakini wote no wafanyakazi wa hapohapo. Kwa kweli haina mantiki.

Utashangaa, MTU mwingine kwenye Ofisi Fulani sekta nyingine Kwa kukuchukia anakufuata na kukujaza au kukuonyesha mapungufu yako ya kikazi kisha ukianza kupaniki anakurekodi video. Hapo ushapaniki utaongea Kwa mihemko ukiwa hujui unarekodiwa.
Hiyo ni Michezo ya kijinga.
Kazi hizo wafanye Wananchi au serikali iunde kikosi kazi cha kufanya Michezo hiyo kupima ufanisi WA watumishi WA umma.
Unaweza kuta huyo msela kapiga sound demu kamchomolea..Kingine unakuta iyo hospital serikali haijapeleka vifaa wangefanyaje sasa..

Angakausha mshamba huyo.
 
Toka mwanzo wa hili sakata mimi naona huyo binti hana kosa.

Ila ni vile wabongo wengi ni wahanga wa majibu mabaya ya wafanyakazi wa kike, hivyo kupelekea zigo la lawama lote kaangushiwa huyo binti.
 
ROSE SHIRIMA HANA KOSA LOLOTE, MWENYE MAKOSA NI JAMES GETOGO KUIBUA MAKOSA YA SERIKALI/MWAJIRI WAKE

Anaandika, Robert Heriel.

Watanzania tunapenda Sana mambo ya kudandia dandia mambo. Kufuata Mkumbo. Kwenye nchi hii ni rahisi Sana kumchafua MTU na watu wakaamini na kumuona MTU Fulani ni Mbaya.

Taikon natumia Kanuni moja, ukija Kwa upole utajibiwa Kwa upole, ukija kishenzi utajibiwa kiushenzi.

Turudi kwenye mada
Kama ukiitazama Ile video inayoonyesha majibizano makali kiasi ya maafisa wa Afya WA zahanati ya Isgihimulwa Tabora ya Rose Shirima na James Getogo, bila kutumia mihemko basi utagundua Rose Shirima Hana kosa lolote.
Mwenye Makosa hapo ni James Getogo.

Zipo sababu zinazonifanya kuwa na mtazamo huo, sababu hizo ni kama ifuatavyo;

1. Mratibu wa njama na Msaliti.
Mchukua kamera ambaye bila Shaka ni James Getogo akiwa kama kinara wa kutelekeza njama hiyo Kwa lengo alilokuwa analijua yeye mwenyewe.

Ni aibu kuwa na mfanyakazi katika serikali au kampuni au hata kwenye familia kama alivyo James Getogo. Unajua ni kwanini?
Serikali inasiri nyingi, taasisi za Elimu zinamapungufu mengi Mno. Hata hapo nyumbani kwako ulipo yapo makorokoro mengi Sana. Lakini mkiwa kama wanafamilia, au wafanyakazi wa ofisi moja kazi yenu ni kujua nini chakufanya ili kukabiliana na hayo matatizo yalipo.
Lakini sio mmoja wenu kuchonga njama ili kuibua uozo wa familia, au serikali au kampuni. Huyo hafai popote pale.

James Getogo hataonekana kama shujaa Bali ataonekana kama MTU asiyetambua nini anafanya. James Getogo ni Msaliti hafai.

Video Ile ilipaswa irekodiwe na MTU wa nje asiyehusika na hiyo zahanati ndio ingekuwa na ujiko/mantiki.
Lakini kurekodiwa na MTU wa ndani hiyo ni njama. Maana ofisini MTU anaweza kukujaza alafu bila ya wewe kujua akawa anakurekodi ukaonekana wewe ndiye mbaya.

2. Makosa katika Video.
Ile video inamakosa kama ifuatavyo;

I/ video imeanzia katikati,
hatujui walianzia wapi, na mchukua video alipoona amepata alichokuwa anakikusudia akaamua aache kurekodi.

ii/ video imechukuliwa na mshtaki(ambaye ni Be. James Getogo).
Ile video ingekuwa na maana endapo mshitakiwa na mshitaki wangekuwa wanarekodiwa pasipo ya wao kujua ili kuondoa Ile dhana ya njama.
Sasa Be. James ndiye anarekodi unafikiri yeye angetumia Lugha gani kujibishana na MTU asiyejua anarekodiwa?
Au unafikiri Rose Shirima angejua anarekodiwa angeongea maneno makali?

Kumchongea Rose Shirima Kwa kumrekodi video ATI kisa katoa maneno ya shombo sio Pouwa! Hata wewe hapo ofisini kwako MTU anaweza kuja Kwa namna ya kukuchokoza na kukupa karaha mpaka ukajikuta unatoa maneno makali kumbe unarekodiwa, alafu video ikitumwa mtandaoni inarushwa kipande chenye maneno yako makali.

3. Makosa ya kimajukumu na kiwajibu.
Huyo James Getogo ashaambiwa na mfanyakazi mwenzake Aende Kwa incharge alafu anang'ang'aniza kumjaza Muuguzi wa Watu, ulitegemea Muuguzi angemchekea au kumjibu Kwa upole kama yupo Kanisani? Hata Kanisani kuna Wakati hakuna mambo ya upole.
Kifaa kama kime-expire ulitaka Muuguzi afanyeje sasa. Kosa lake ni lipi hapo? Yeye kakuambiwa ndio kime-expire lakini kinaweza kutumika, swali lililokuwa linafuata hapo lingetakiwa; je hakuna hatari yoyote Kutumia kifaa kilicho-expire? Hapo Rose angejieleza kulingana na uelewa wake na Elimu yake. Nani ajuaye kuwa huenda Rose anaelimu Fulani kuhusu vitu ku-expire na muda wake wa matumizi(hiyo ni juu yake sasa)

Alafu huyu James Getogo mpaka anaelekezwa na Rose Shirima kuwa Aende Kwa Incharge kwani yeye hajui taratibu za hiyo Zahanati?
Kumfukuza Kazi Rose Shirima haitakuwa Sawa. Na utakuwa uamuzi wa ajabu Sana.
Majukumu ya Muuguzi yanafahamika.

Matatizo ya namna hiyo maofisini yanapotokea hasa katika mahospitali kunakuwaga na vikao vya Asubuhi kujadili nini kimefanyika, changamoto na kupeana majukumu Kwa Siku Mpya.
James Getogo hakujua kuwa ishu ya vikao ili alete shauri lake kwenye vikao.

Kama huyo Rose Shirima anatabia mbovu ya kujibu Watu nyokonyoko(ambayo sio Tabia nzuri) je ilishindikana kumuweka kwenye kikao wakiwepo wakubwa wake wa kazi?
Au James Getogo alitaka kuiaminisha jamii ya kitanzania kuwa Rose Shirima anamdomo mchafu Kwa clip moja tuu iliyoanzia katikati tena aliyoirekodi yeye?
Come on! Tuache masikhara!

Sitetei Tabia ya majibu ya hovyohovyo na nyokonyoko Kutoka Kwa watumishi WA umma ila najaribu kuelezea kuwa yapo mazingira majibu ya nyokonyoko yanaweza kujitokeza accidentally.

Pia, najaribu kueleza kuwa ni Tabia Mbaya Kwa mfanyakazi au mwanafamilia kutoa nje madhaifu ya ofisi, kampuni au serikali Kwa Watu wasiohusika. Ni usaliti Mkubwa. Pia ni nje ya maadili ya Kazi.

Rose Shirima arudishwe kazini. Huyo James Getogo apewe onyo kali au akapewe semina. Ingawaje ingekuwa kwenye Ofisi binafsi basi angekuwa amefukuzwa kazi muda mrefu Sana.

Sio kazi ya mfanyakazi kufichua maovu ya ofisi anayofanyia Kazi. Hiyo sio kazi yako.
Waachie wenye kazi Yao ambao ni Sisi Raia.
Kumchomesha mwenzako Kwa Aina yoyote tena Kwa Watu wasiohusika Sisi kina Taikon tunaita ni uzuzu! Usaliti na kutojitambua.

Watanzania wengi watamshambulia Rose lakini kimsingi Rose hana kosa lolote. Tena apandishwe cheo.

SABATO NJEMA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mkuu umesahau kuandika namba ya simu.
 
Toka mwanzo wa hili sakata mimi naona huyo binti hana kosa.

Ila ni vile wabongo wengi ni wahanga wa majibu mabaya ya wafanyakazi wa kike, hivyo kupelekea zigo la lawama lote kaangushiwa huyo binti.

Pia watanzania tunapenda SHOBO hata na watu wasiotaka tuwe karibu Yao. Ndio maana tunaona wanaringa na kujishaua.
Watanzania tuelewe kuwa Watu tupo tofauti sana.

MTU kama hataki mazoea na wewe Kwa nini umlazimishe?
 
Shirima NTU wa dili?
Mbona nguvu kubwa inatumika kutetea hii idara ya Afya kwa uzembe wa Hawa watu wanaodili na Afya na uhai wetu Kuna madudud mengi sana huko . Mbona hamtumii hii nguvu kutetea kada zingine kama vile walimu na traffic barabarani.

Hua mnatoa hukumu za haraka kwa walimu na traffic kufukuzwa kazi. Lakin kwa hili mnamtetea sana upuuzi wa huyu nesi. Manesi wengi hupelekea vifo vingi sana vya wagonjwa kwa uzembe wao.
Wana lugha chafu sana kwa wagonjwa hasa wajawazito. Mimi mwenyewe nilishawahi kutaka kumpga vibao nesi. Baada ya kumjibu mke wangu majibu ya kunyia.

Wamama wengi hupoteza watoto kwa uzembe wa Hawa watu na Wala usiwatetee kabisa. Kama anamjibu hivyo mfanyakazi mwenzake. Vipi kuhusu mama mjamzito..
 
Sema wewe na watoto wako na mkeo na ukoo wako wote!
Sipendi limtu linalo penda ku generalize mambo, sasa wewe unajua watu wote Tanzania [emoji1241] ndio utuseme tunapenda kudandia mambo! Tafadhali naomba ukome kabisa unasikia wewe!
Mtu mzima ovyooooooo [emoji35]
 
Mpuuzi sana wewe. Mtu ameokoa masiha ya watu unasema ana nakosa au wewe ndio pisi Yako ile

Ukiyachukulia mambo kimhemko hemko kama hivi utakwama sehemu nyingi.

Mada hujui hata inazungumzia kitu gani.
Wewe ukiulizwa kosa la Muuguzi ni lipi utajibuje?
 
Sema wewe na watoto wako na mkeo na ukoo wako wote!
Sipendi limtu linalo penda ku generalize mambo, sasa wewe unajua watu wote Tanzania [emoji1241] ndio utuseme tunapenda kudandia mambo! Tafadhali naomba ukome kabisa unasikia wewe!
Mtu mzima ovyooooooo [emoji35]

Kwani Nani anataka kupendwa na wewe humu?
 
Ingekuwa wanarekodiwa Sana kazini weledi ungeongezeka.
Wenzetu Ulaya unafanya Kazi unamulikwa na camera Ili kucontrol unavyohudumia watu kwa uadilifu
Hata police wa kule uvaa camera na pia vifaa vya kurekodi KILA kitu unachofanya kama defense chochote kikitokea.
 
Ingekuwa wanarekodiwa Sana kazini weledi ungeongezeka.
Wenzetu Ulaya unafanya Kazi unamulikwa na camera Ili kucontrol unavyohudumia watu kwa uadilifu
Hata police wa kule uvaa camera na pia vifaa vya kurekodi KILA kitu unachofanya kama defense chochote kikitokea.

Yes,
Ila sio MTU kumfanyia uhuni kama alivyofanya James Getogo.
Ukiifuatilie Ile video utagundua kuwa James alikuwa anamchonoa mwenzake, anamlazimishia.
 
Back
Top Bottom