Rose Shirima hana kosa lolote, mwenye Makosa ni James Getogo kuibua makosa ya serikali/mwajiri wake

Vifaa vya kupimia vinatolewa wapi? Tuanzie hapo ili Rose awe na tatizo.
Ikiwa Rose na wengine hupewa vifaa hivyo basi Rose hana kosa.
Na mtu wa maabara amegundua kifaa kilichotumika kupimia malaria hakiko sahihi . Ni wajibu wake kuripoti kwa incharge sio kwa muuguzi, otherwise huyo muuguzi ndio incharge pia.
Mchukua clip ambaye kwa namna fulani huyo wa Maabara au aliyeandaliwa kurekodi Rose alikuwa na njama ovu.
1. Wa kwanza kuwajibika ni incharge
2. Nimtoa vifaa vilivyoisha muda huko stoo.
3. Ni James wa Maabara kwa kurekodi au kumuandaa mtu wa kurekodi na kusambaza hili ni kosa la kimtandao.
4. Ni Rose kwa kutumia lugha isio ya kitaaluma na kubishia taaluma ingine.

Hukumu.
1.Mtoa vifaa kuondolewa kwa kuendelea kutoa vifaa visivyofaa. AFUKUZWE
2. James AFUKUZWE KAZI kwa kukiuka maadili ya kazi kwa kurekodi au kuandaa mtu wa kurekodi mtumishi akiwa kwenye majukumu ya kazi, hususan hilo la afya. Ipo siku atarwkodi wake zetu wakifungua au akiwa chumba cha upasuaji na kusambaza. AFUKUZWE na vyeti vyake KUSHIKILIWA KWANZA.
3. Rose AONYWE au apate barua ya ONYO na kuchunguzwa ikiwa hizo ndio lugha zake AFUKUZWE KAZI.

Ni mimi Bushlawyer

Umeeleza vizuri Mno.

Hao Vijana Wawili waliorekodi hiyo video ni wachokozi, utafikiri hawajui utaratibu wa Kazi.
Unamuuliza MTU asiyehusika kuhusu vifaa unategemea atakujibu nini
 
Dhana kwamba eti kutoa taarifa hii ni aibu kwa ofisi au serikali ni potofu na ya kijinga sana. Pili unachanganya kati ya siri (confidential information) za taasisi na kunyamazia uzembe na uvunjwaji wa taratibu za kazi. Mfano kusema tumia vipimo vilivyo expire kupima wajawazito, hata kama in charge wako amekupa hayo maelekezo (ambayo itakuwa verbally kwa sababu na yeye anajua hawezi kukuandikia barua) ni kosa kubwa. Mwisho kwa nini hudhani kwamba pengine ni mwananchi wa kawaida ndiye aliyechukua hiyo video clip? Kwanza kwa jinsi wengi humu wanavyotetea ujinga kwa kichaka cha kuvujisha siri za taasisi sidhani kama ni mtumishi aliyevujisha hiyo video.

Aliyerekodi hiyo video ni Nani? Huyo James Getogo anaonekana kujua kinachoendelea ndio maana anazidi kumchokoa mwenzake.

Haya tuambie kosa la Rose Shirima ni lipi?
1. Rose Shirima sio incharge
2. Rose Shirima sio MTU wa kutoa vifaa vya hospital.
3. Rose Shirima sio MTU wa maabara
4. Rose Shirima sio mleta vifaa na madawa katika hiyo hospital.

Kosa lake ni lipi hapo?
Au kumjibu maneno ya shombo James Getogo ndio KOSA?
MTU kama ni mpuuzi lazima ajibiwe hivyo ili awe na Akili
 
ROSE SHIRIMA HANA KOSA LOLOTE, MWENYE MAKOSA NI JAMES GETOGO KUIBUA MAKOSA YA SERIKALI/MWAJIRI WAKE

Anaandika, Robert Heriel.

Watanzania Wengi tunapenda Sana mambo ya kudandia dandia mambo. Kufuata Mkumbo. Kwenye nchi hii ni rahisi Sana kumchafua MTU na watu wakaamini na kumuona MTU Fulani ni Mbaya.

Taikon natumia Kanuni moja, ukija Kwa upole utajibiwa Kwa upole, ukija kishenzi utajibiwa kiushenzi.

Turudi kwenye mada
Kama ukiitazama Ile video inayoonyesha majibizano makali kiasi ya maafisa wa Afya WA zahanati ya Isgihimulwa Tabora ya Rose Shirima na James Getogo, bila kutumia mihemko basi utagundua Rose Shirima Hana kosa lolote.
Mwenye Makosa hapo ni James Getogo.

Zipo sababu zinazonifanya kuwa na mtazamo huo, sababu hizo ni kama ifuatavyo;

1. Mratibu wa njama na Msaliti.
Mchukua kamera ambaye bila Shaka ni James Getogo akiwa kama kinara wa kutelekeza njama hiyo Kwa lengo alilokuwa analijua yeye mwenyewe.

Ni aibu kuwa na mfanyakazi katika serikali au kampuni au hata kwenye familia kama alivyo James Getogo. Unajua ni kwanini?
Serikali inasiri nyingi, taasisi za Elimu zinamapungufu mengi Mno. Hata hapo nyumbani kwako ulipo yapo makorokoro mengi Sana. Lakini mkiwa kama wanafamilia, au wafanyakazi wa ofisi moja kazi yenu ni kujua nini chakufanya ili kukabiliana na hayo matatizo yalipo.
Lakini sio mmoja wenu kuchonga njama ili kuibua uozo wa familia, au serikali au kampuni. Huyo hafai popote pale.

James Getogo hataonekana kama shujaa Bali ataonekana kama MTU asiyetambua nini anafanya. James Getogo ni Msaliti hafai.

Video Ile ilipaswa irekodiwe na MTU wa nje asiyehusika na hiyo zahanati ndio ingekuwa na ujiko/mantiki.
Lakini kurekodiwa na MTU wa ndani hiyo ni njama. Maana ofisini MTU anaweza kukujaza alafu bila ya wewe kujua akawa anakurekodi ukaonekana wewe ndiye mbaya.

2. Makosa katika Video.
Ile video inamakosa kama ifuatavyo;

I/ video imeanzia katikati,
hatujui walianzia wapi, na mchukua video alipoona amepata alichokuwa anakikusudia akaamua aache kurekodi.

ii/ video imechukuliwa na mshtaki(ambaye ni Be. James Getogo).
Ile video ingekuwa na maana endapo mshitakiwa na mshitaki wangekuwa wanarekodiwa pasipo ya wao kujua ili kuondoa Ile dhana ya njama.
Sasa Be. James ndiye anarekodi unafikiri yeye angetumia Lugha gani kujibishana na MTU asiyejua anarekodiwa?
Au unafikiri Rose Shirima angejua anarekodiwa angeongea maneno makali?

Kumchongea Rose Shirima Kwa kumrekodi video ATI kisa katoa maneno ya shombo sio Pouwa! Hata wewe hapo ofisini kwako MTU anaweza kuja Kwa namna ya kukuchokoza na kukupa karaha mpaka ukajikuta unatoa maneno makali kumbe unarekodiwa, alafu video ikitumwa mtandaoni inarushwa kipande chenye maneno yako makali.

3. Makosa ya kimajukumu na kiwajibu.
Huyo James Getogo ashaambiwa na mfanyakazi mwenzake Aende Kwa incharge alafu anang'ang'aniza kumjaza Muuguzi wa Watu, ulitegemea Muuguzi angemchekea au kumjibu Kwa upole kama yupo Kanisani? Hata Kanisani kuna Wakati hakuna mambo ya upole.
Kifaa kama kime-expire ulitaka Muuguzi afanyeje sasa. Kosa lake ni lipi hapo? Yeye kakuambiwa ndio kime-expire lakini kinaweza kutumika, swali lililokuwa linafuata hapo lingetakiwa; je hakuna hatari yoyote Kutumia kifaa kilicho-expire? Hapo Rose angejieleza kulingana na uelewa wake na Elimu yake. Nani ajuaye kuwa huenda Rose anaelimu Fulani kuhusu vitu ku-expire na muda wake wa matumizi(hiyo ni juu yake sasa)

Alafu huyu James Getogo mpaka anaelekezwa na Rose Shirima kuwa Aende Kwa Incharge kwani yeye hajui taratibu za hiyo Zahanati?
Kumfukuza Kazi Rose Shirima haitakuwa Sawa. Na utakuwa uamuzi wa ajabu Sana.
Majukumu ya Muuguzi yanafahamika.

Matatizo ya namna hiyo maofisini yanapotokea hasa katika mahospitali kunakuwaga na vikao vya Asubuhi kujadili nini kimefanyika, changamoto na kupeana majukumu Kwa Siku Mpya.
James Getogo hakujua kuwa ishu ya vikao ili alete shauri lake kwenye vikao.

Kama huyo Rose Shirima anatabia mbovu ya kujibu Watu nyokonyoko(ambayo sio Tabia nzuri) je ilishindikana kumuweka kwenye kikao wakiwepo wakubwa wake wa kazi?
Au James Getogo alitaka kuiaminisha jamii ya kitanzania kuwa Rose Shirima anamdomo mchafu Kwa clip moja tuu iliyoanzia katikati tena aliyoirekodi yeye?
Come on! Tuache masikhara!

Sitetei Tabia ya majibu ya hovyohovyo na nyokonyoko Kutoka Kwa watumishi WA umma ila najaribu kuelezea kuwa yapo mazingira majibu ya nyokonyoko yanaweza kujitokeza accidentally.

Pia, najaribu kueleza kuwa ni Tabia Mbaya Kwa mfanyakazi au mwanafamilia kutoa nje madhaifu ya ofisi, kampuni au serikali Kwa Watu wasiohusika. Ni usaliti Mkubwa. Pia ni nje ya maadili ya Kazi.

Rose Shirima arudishwe kazini. Huyo James Getogo apewe onyo kali au akapewe semina. Ingawaje ingekuwa kwenye Ofisi binafsi basi angekuwa amefukuzwa kazi muda mrefu Sana.

Sio kazi ya mfanyakazi kufichua maovu ya ofisi anayofanyia Kazi. Hiyo sio kazi yako.
Waachie wenye kazi Yao ambao ni Sisi Raia.
Kumchomesha mwenzako Kwa Aina yoyote tena Kwa Watu wasiohusika Sisi kina Taikon tunaita ni uzuzu! Usaliti na kutojitambua.

Watanzania wengi watamshambulia Rose lakini kimsingi Rose hana kosa lolote. Tena apandishwe cheo.

SABATO NJEMA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam

Iangalie hiyo video hapo Chini bila mihemko
Yaani wewe maku kweli kweli, ugomvi wa rose na James sisi hautuhusu kinachotuhusu ni dhamira ya rose pamoja na kushauliwa sana bado mbishi na kutoa maneno ya dharau
 
Wewe ndio wale watetezi wa vyeti feki. Lugha ya rose shirima ni lugha mbaya haistahili majibu ya dharau na kutukana mfanyakazi mwenzie kwa kisingizio chochote.
Huyo james getogo anaweza kukutwa na kosa la kimaadili labda kama amerekodi na kusbaza hiyo video. Vinginevyo kama kuna third party anaweza akaonekana hana kosa.
Huyo rose shirima ana act unprofessional kabisa kwa nesi.
Anagongwa na mganga mkuu wa hospital ndiomaana jeuri vile
 
Umeeleza vizuri Mno.

Hao Vijana Wawili waliorekodi hiyo video ni wachokozi, utafikiri hawajui utaratibu wa Kazi.
Unamuuliza MTU asiyehusika kuhusu vifaa unategemea atakujibu nini
Acheni kutetea upuuzi, rose kama anamjibu mfanyakazi mwenzie vile vipi majibu yake kwa wagonjwa?
 
Basi kama kwenye utumishi wa umma kuna takiwa kuwa na siri. Tuwaache mafisadi waendelee kula sasa tunawapigia kelele wa nini na sisi wa nje tunajuaje siri zao kama kuna ethics za kutunza siri za utumishi wa umma.
Hata sheria za umma zinasisitiza kutunza siri.
 
ROSE SHIRIMA HANA KOSA LOLOTE, MWENYE MAKOSA NI JAMES GETOGO KUIBUA MAKOSA YA SERIKALI/MWAJIRI WAKE

Anaandika, Robert Heriel.

Watanzania Wengi tunapenda Sana mambo ya kudandia dandia mambo. Kufuata Mkumbo. Kwenye nchi hii ni rahisi Sana kumchafua MTU na watu wakaamini na kumuona MTU Fulani ni Mbaya.

Taikon natumia Kanuni moja, ukija Kwa upole utajibiwa Kwa upole, ukija kishenzi utajibiwa kiushenzi.

Turudi kwenye mada
Kama ukiitazama Ile video inayoonyesha majibizano makali kiasi ya maafisa wa Afya WA zahanati ya Isgihimulwa Tabora ya Rose Shirima na James Getogo, bila kutumia mihemko basi utagundua Rose Shirima Hana kosa lolote.
Mwenye Makosa hapo ni James Getogo.

Zipo sababu zinazonifanya kuwa na mtazamo huo, sababu hizo ni kama ifuatavyo;

1. Mratibu wa njama na Msaliti.
Mchukua kamera ambaye bila Shaka ni James Getogo akiwa kama kinara wa kutelekeza njama hiyo Kwa lengo alilokuwa analijua yeye mwenyewe.

Ni aibu kuwa na mfanyakazi katika serikali au kampuni au hata kwenye familia kama alivyo James Getogo. Unajua ni kwanini?
Serikali inasiri nyingi, taasisi za Elimu zinamapungufu mengi Mno. Hata hapo nyumbani kwako ulipo yapo makorokoro mengi Sana. Lakini mkiwa kama wanafamilia, au wafanyakazi wa ofisi moja kazi yenu ni kujua nini chakufanya ili kukabiliana na hayo matatizo yalipo.
Lakini sio mmoja wenu kuchonga njama ili kuibua uozo wa familia, au serikali au kampuni. Huyo hafai popote pale.

James Getogo hataonekana kama shujaa Bali ataonekana kama MTU asiyetambua nini anafanya. James Getogo ni Msaliti hafai.

Video Ile ilipaswa irekodiwe na MTU wa nje asiyehusika na hiyo zahanati ndio ingekuwa na ujiko/mantiki.
Lakini kurekodiwa na MTU wa ndani hiyo ni njama. Maana ofisini MTU anaweza kukujaza alafu bila ya wewe kujua akawa anakurekodi ukaonekana wewe ndiye mbaya.

2. Makosa katika Video.
Ile video inamakosa kama ifuatavyo;

I/ video imeanzia katikati,
hatujui walianzia wapi, na mchukua video alipoona amepata alichokuwa anakikusudia akaamua aache kurekodi.

ii/ video imechukuliwa na mshtaki(ambaye ni Be. James Getogo).
Ile video ingekuwa na maana endapo mshitakiwa na mshitaki wangekuwa wanarekodiwa pasipo ya wao kujua ili kuondoa Ile dhana ya njama.
Sasa Be. James ndiye anarekodi unafikiri yeye angetumia Lugha gani kujibishana na MTU asiyejua anarekodiwa?
Au unafikiri Rose Shirima angejua anarekodiwa angeongea maneno makali?

Kumchongea Rose Shirima Kwa kumrekodi video ATI kisa katoa maneno ya shombo sio Pouwa! Hata wewe hapo ofisini kwako MTU anaweza kuja Kwa namna ya kukuchokoza na kukupa karaha mpaka ukajikuta unatoa maneno makali kumbe unarekodiwa, alafu video ikitumwa mtandaoni inarushwa kipande chenye maneno yako makali.

3. Makosa ya kimajukumu na kiwajibu.
Huyo James Getogo ashaambiwa na mfanyakazi mwenzake Aende Kwa incharge alafu anang'ang'aniza kumjaza Muuguzi wa Watu, ulitegemea Muuguzi angemchekea au kumjibu Kwa upole kama yupo Kanisani? Hata Kanisani kuna Wakati hakuna mambo ya upole.
Kifaa kama kime-expire ulitaka Muuguzi afanyeje sasa. Kosa lake ni lipi hapo? Yeye kakuambiwa ndio kime-expire lakini kinaweza kutumika, swali lililokuwa linafuata hapo lingetakiwa; je hakuna hatari yoyote Kutumia kifaa kilicho-expire? Hapo Rose angejieleza kulingana na uelewa wake na Elimu yake. Nani ajuaye kuwa huenda Rose anaelimu Fulani kuhusu vitu ku-expire na muda wake wa matumizi(hiyo ni juu yake sasa)

Alafu huyu James Getogo mpaka anaelekezwa na Rose Shirima kuwa Aende Kwa Incharge kwani yeye hajui taratibu za hiyo Zahanati?
Kumfukuza Kazi Rose Shirima haitakuwa Sawa. Na utakuwa uamuzi wa ajabu Sana.
Majukumu ya Muuguzi yanafahamika.

Matatizo ya namna hiyo maofisini yanapotokea hasa katika mahospitali kunakuwaga na vikao vya Asubuhi kujadili nini kimefanyika, changamoto na kupeana majukumu Kwa Siku Mpya.
James Getogo hakujua kuwa ishu ya vikao ili alete shauri lake kwenye vikao.

Kama huyo Rose Shirima anatabia mbovu ya kujibu Watu nyokonyoko(ambayo sio Tabia nzuri) je ilishindikana kumuweka kwenye kikao wakiwepo wakubwa wake wa kazi?
Au James Getogo alitaka kuiaminisha jamii ya kitanzania kuwa Rose Shirima anamdomo mchafu Kwa clip moja tuu iliyoanzia katikati tena aliyoirekodi yeye?
Come on! Tuache masikhara!

Sitetei Tabia ya majibu ya hovyohovyo na nyokonyoko Kutoka Kwa watumishi WA umma ila najaribu kuelezea kuwa yapo mazingira majibu ya nyokonyoko yanaweza kujitokeza accidentally.

Pia, najaribu kueleza kuwa ni Tabia Mbaya Kwa mfanyakazi au mwanafamilia kutoa nje madhaifu ya ofisi, kampuni au serikali Kwa Watu wasiohusika. Ni usaliti Mkubwa. Pia ni nje ya maadili ya Kazi.

Rose Shirima arudishwe kazini. Huyo James Getogo apewe onyo kali au akapewe semina. Ingawaje ingekuwa kwenye Ofisi binafsi basi angekuwa amefukuzwa kazi muda mrefu Sana.

Sio kazi ya mfanyakazi kufichua maovu ya ofisi anayofanyia Kazi. Hiyo sio kazi yako.
Waachie wenye kazi Yao ambao ni Sisi Raia.
Kumchomesha mwenzako Kwa Aina yoyote tena Kwa Watu wasiohusika Sisi kina Taikon tunaita ni uzuzu! Usaliti na kutojitambua.

Watanzania wengi watamshambulia Rose lakini kimsingi Rose hana kosa lolote. Tena apandishwe cheo.

SABATO NJEMA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam

Iangalie hiyo video hapo Chini bila mihemko
[emoji706]
 
Kosa la rose ni lipi?
Unajua ni mambo mangapi yanayofanyika kwenye nchi hii yanayohatarisha usalama wa Watu kisa umaskini wetu?
Au Kwa vile Rose karekodiwa tena bila ya kujua na aliyemrekodi ni mfanyakazi mwenzake
Makosa ya rose ni lugha chafu, kutogomea vifaa tiba vilivyoisha muda kutoka kwa inchaji na kulazimisha vifaa vitumike
 
Hayo majibizano mbona kila Siku yapo maofisini hasa Kwa watu/wafanyakazi wasiowaelewa. Unamuambia kitu MTU hasikii.

Sasa kama anajua vime-expire alitaka Rose afanyeje?
Rose kamuambia nenda Kwa incharge, James kang'ang'ania kumsimamia,
Acheni kupindisha vitu, rose kasema nenda kwa inchaji tu? Mbona mengine hamsemi?
 
Acheni kutetea upuuzi, rose kama anamjibu mfanyakazi mwenzie vile vipi majibu yake kwa wagonjwa?
Msiwe wanafiki kila mtu anajua ukisha kasirishwa huwezi kuwa na majibu ya staha maijifanye leo ndio mnajua sana kuchambua ya wenzenu wakati hata ninyi huko mnako fanyia majukumu yenu mmesha pigizana sana kelele na wenzenu

Kupishana vituo vya kazi ni jambo la kawaida sana ila mshamba na mwenye kosa namba moja ni huyo mrekodi picha hajui maadili ya kazi za umma

Nakuhakikishia huyo dada atatoka salama maana kosa lake lina weza kuepukika kwa TKO ila huyo msela aliye rekodi kama aliamini anamkomoa huyo dada basi hana akili kwa tukio kama hilo yeye ndio kajikaanga vizuri sana na ndiye mwenye kosa kubwa zaid l
 
Pia watanzania tunapenda SHOBO hata na watu wasiotaka tuwe karibu Yao. Ndio maana tunaona wanaringa na kujishaua.
Watanzania tuelewe kuwa Watu tupo tofauti sana.

MTU kama hataki mazoea na wewe Kwa nini umlazimishe?
Mbona mnaishi kwa hisia bila uhalisia? Mazungumzo ya video yanaonyesha ni ishu za kikazi tu nothing else. Sasa James afanye kazi na nani?
 
Msiwe wanafiki kila mtu anajua ukisha kasirishwa huwezi kuwa na majibu ya staha maijifanye leo ndio mnajua sana kuchambua ya wenzenu wakati hata ninyi huko mnako fanyia majukumu yenu mmesha pigizana sana kelele na wenzenu

Kupishana vituo vya kazi ni jambo la kawaida sana ila mshamba na mwenye kosa namba moja ni huyo mrekodi picha hajui maadili ya kazi za umma

Nakuhakikishia huyo dada atatoka salama maana kosa lake lina weza kuepukika kwa TKO ila huyo msela aliye rekodi kama aliamini anamkomoa huyo dada basi hana akili kwa tukio kama hilo yeye ndio kajikaanga vizuri sana na ndiye mwenye kosa kubwa zaid l
Wachaga mnateteana
 
Yes,
Ila sio MTU kumfanyia uhuni kama alivyofanya James Getogo.
Ukiifuatilie Ile video utagundua kuwa James alikuwa anamchonoa mwenzake, anamlazimishia.
Ukifatilia video unaona wazi dada ndio analazimisha vifaa vitumike vilivyoharibika
 
Makosa ya rose ni lugha chafu, kutogomea vifaa tiba vilivyoisha muda kutoka kwa inchaji na kulazimisha vifaa vitumike
Hiyo inapigika chenga vizuri kabisa mzee na usije ukadhani serikali hapo itatoa jibu kwamba vipimo viliisha mda wake hilo sahau

Hapo lazima mrekodi video zigo limuamgukie aambiwe alikuwa na ugomvi binafsi baada ya kukataliwa kimapenzi na vipimo alivyo ambiwa avitumie havikuwa vimeisha mda wake
 
Unaweza ibua Makosa ya familia yako? Badala ya kutafuta namna ya kuyatatua?

Hivi Mkeo akiibua Makosa yako Mbele ya umma ni halali Kwa muono wako?
Au wewe unakampuni na ndio boss alafu mfanyakazi mmoja anaibua Mbele za umma Makosa ya kampuni yako ni Sawa?

Hapo angefanya MTU wa nje ingekuwa Sawa Kabisa.
Sio kama nakataa Watu wasifichue Makosa au maovu, lakini waangalie nafasi zao na majukumu yao
Tofautisha ishu ya familia na ishu ya umma,
 
Ukifatilia video unaona wazi dada ndio analazimisha vifaa vitumike vilivyoharibika
Ukisikiliza kwa makini dada hajatamka wazi wazi kulazimisha vifaa vitumike ila james kaambiwa aende kwa incharge akamweleze.
 
Tofautisha ishu ya familia na ishu ya umma,
Msio jua kanuni za utumishi wa umma mnaonekana tu kifupi
kwa tunao jua utendaji wa serikali ni kwamba james anakosa kubwa zaidi la kiutumishi kuliko hiyo dada
 
Ukifatilia video unaona wazi dada ndio analazimisha vifaa vitumike vilivyoharibika

Huyo Dada analazimisha kama Nani hapo?
Yeye ni MTU wa maabara?,
Yeye ni incharge?
Yeye ni Mganga Mkuu hapo?

Huyo James ndiye analazimisha Kwa sababu keshaambiwa Aende Kwa incharge lakini yeye anasema haendi, anataka kuendeleza mabishano yasiyo na kichwa wala miguu

Alafu huyo James ndiye kamfuata mwenzake kwenye Ofisi yake.
 
"Mtu akikukataa kimapenzi usimfanyie hivyo mapenzi ni hiyari, ninyi ni timu moja"
 
Back
Top Bottom