Rose Shirima hana kosa lolote, mwenye Makosa ni James Getogo kuibua makosa ya serikali/mwajiri wake

Rose Shirima hana kosa lolote, mwenye Makosa ni James Getogo kuibua makosa ya serikali/mwajiri wake

Sasa Kama anapikwa Mkeo au Mama yako au wewe mwenyewe, Rose kama Muuguzi anahusikaje? Hiyo ndio hoja.

Rose sio MTU wa maabara.
Rose sio incharge
Sasa niambie Rose anahusikaje kwenye vipimo vya MKE wako au wewe mwenyewe Kwa scenario ya Ile video?

Unajua majukumu ya Muuguzi?
Lakini kihualisia ile sehem itakuwa na shida sana wao kwa wao so hakuna nidham hii ina affect wagonjwa video imechangia kujua udhaifu wao kila zuri lina kuja na baya lake
 
Me naona wazidi kurekodi zaidi maana watasimamia misingi afya ni uhai maana jambo dogo lina lina affect mwili

Unachosema ni kizuri lakini inategemea na anayerekodi ni Nani.

MTU ukishakuwa sehemu ya taasisi Fulani unakuwa sehemu ya mfumo huo.
Unapaswa mjue namna ya kutatua matatizo ya hiyo taasisi, ndio kazi yenu hiyo mbali na kazi ya kuhudumia jamii.
 
ROSE SHIRIMA HANA KOSA LOLOTE, MWENYE MAKOSA NI JAMES GETOGO KUIBUA MAKOSA YA SERIKALI/MWAJIRI WAKE

Anaandika, Robert Heriel.

Watanzania Wengi tunapenda Sana mambo ya kudandia dandia mambo. Kufuata Mkumbo. Kwenye nchi hii ni rahisi Sana kumchafua MTU na watu wakaamini na kumuona MTU Fulani ni Mbaya.

Taikon natumia Kanuni moja, ukija Kwa upole utajibiwa Kwa upole, ukija kishenzi utajibiwa kiushenzi.

Turudi kwenye mada
Kama ukiitazama Ile video inayoonyesha majibizano makali kiasi ya maafisa wa Afya WA zahanati ya Isgihimulwa Tabora ya Rose Shirima na James Getogo, bila kutumia mihemko basi utagundua Rose Shirima Hana kosa lolote.
Mwenye Makosa hapo ni James Getogo.

Zipo sababu zinazonifanya kuwa na mtazamo huo, sababu hizo ni kama ifuatavyo;

1. Mratibu wa njama na Msaliti.
Mchukua kamera ambaye bila Shaka ni James Getogo akiwa kama kinara wa kutelekeza njama hiyo Kwa lengo alilokuwa analijua yeye mwenyewe.

Ni aibu kuwa na mfanyakazi katika serikali au kampuni au hata kwenye familia kama alivyo James Getogo. Unajua ni kwanini?
Serikali inasiri nyingi, taasisi za Elimu zinamapungufu mengi Mno. Hata hapo nyumbani kwako ulipo yapo makorokoro mengi Sana. Lakini mkiwa kama wanafamilia, au wafanyakazi wa ofisi moja kazi yenu ni kujua nini chakufanya ili kukabiliana na hayo matatizo yalipo.
Lakini sio mmoja wenu kuchonga njama ili kuibua uozo wa familia, au serikali au kampuni. Huyo hafai popote pale.

James Getogo hataonekana kama shujaa Bali ataonekana kama MTU asiyetambua nini anafanya. James Getogo ni Msaliti hafai.

Video Ile ilipaswa irekodiwe na MTU wa nje asiyehusika na hiyo zahanati ndio ingekuwa na ujiko/mantiki.
Lakini kurekodiwa na MTU wa ndani hiyo ni njama. Maana ofisini MTU anaweza kukujaza alafu bila ya wewe kujua akawa anakurekodi ukaonekana wewe ndiye mbaya.

2. Makosa katika Video.
Ile video inamakosa kama ifuatavyo;

I/ video imeanzia katikati,
hatujui walianzia wapi, na mchukua video alipoona amepata alichokuwa anakikusudia akaamua aache kurekodi.

ii/ video imechukuliwa na mshtaki(ambaye ni Be. James Getogo).
Ile video ingekuwa na maana endapo mshitakiwa na mshitaki wangekuwa wanarekodiwa pasipo ya wao kujua ili kuondoa Ile dhana ya njama.
Sasa Be. James ndiye anarekodi unafikiri yeye angetumia Lugha gani kujibishana na MTU asiyejua anarekodiwa?
Au unafikiri Rose Shirima angejua anarekodiwa angeongea maneno makali?

Kumchongea Rose Shirima Kwa kumrekodi video ATI kisa katoa maneno ya shombo sio Pouwa! Hata wewe hapo ofisini kwako MTU anaweza kuja Kwa namna ya kukuchokoza na kukupa karaha mpaka ukajikuta unatoa maneno makali kumbe unarekodiwa, alafu video ikitumwa mtandaoni inarushwa kipande chenye maneno yako makali.

3. Makosa ya kimajukumu na kiwajibu.
Huyo James Getogo ashaambiwa na mfanyakazi mwenzake Aende Kwa incharge alafu anang'ang'aniza kumjaza Muuguzi wa Watu, ulitegemea Muuguzi angemchekea au kumjibu Kwa upole kama yupo Kanisani? Hata Kanisani kuna Wakati hakuna mambo ya upole.
Kifaa kama kime-expire ulitaka Muuguzi afanyeje sasa. Kosa lake ni lipi hapo? Yeye kakuambiwa ndio kime-expire lakini kinaweza kutumika, swali lililokuwa linafuata hapo lingetakiwa; je hakuna hatari yoyote Kutumia kifaa kilicho-expire? Hapo Rose angejieleza kulingana na uelewa wake na Elimu yake. Nani ajuaye kuwa huenda Rose anaelimu Fulani kuhusu vitu ku-expire na muda wake wa matumizi(hiyo ni juu yake sasa)

Alafu huyu James Getogo mpaka anaelekezwa na Rose Shirima kuwa Aende Kwa Incharge kwani yeye hajui taratibu za hiyo Zahanati?
Kumfukuza Kazi Rose Shirima haitakuwa Sawa. Na utakuwa uamuzi wa ajabu Sana.
Majukumu ya Muuguzi yanafahamika.

Matatizo ya namna hiyo maofisini yanapotokea hasa katika mahospitali kunakuwaga na vikao vya Asubuhi kujadili nini kimefanyika, changamoto na kupeana majukumu Kwa Siku Mpya.
James Getogo hakujua kuwa ishu ya vikao ili alete shauri lake kwenye vikao.

Kama huyo Rose Shirima anatabia mbovu ya kujibu Watu nyokonyoko(ambayo sio Tabia nzuri) je ilishindikana kumuweka kwenye kikao wakiwepo wakubwa wake wa kazi?
Au James Getogo alitaka kuiaminisha jamii ya kitanzania kuwa Rose Shirima anamdomo mchafu Kwa clip moja tuu iliyoanzia katikati tena aliyoirekodi yeye?
Come on! Tuache masikhara!

Sitetei Tabia ya majibu ya hovyohovyo na nyokonyoko Kutoka Kwa watumishi WA umma ila najaribu kuelezea kuwa yapo mazingira majibu ya nyokonyoko yanaweza kujitokeza accidentally.

Pia, najaribu kueleza kuwa ni Tabia Mbaya Kwa mfanyakazi au mwanafamilia kutoa nje madhaifu ya ofisi, kampuni au serikali Kwa Watu wasiohusika. Ni usaliti Mkubwa. Pia ni nje ya maadili ya Kazi.

Rose Shirima arudishwe kazini. Huyo James Getogo apewe onyo kali au akapewe semina. Ingawaje ingekuwa kwenye Ofisi binafsi basi angekuwa amefukuzwa kazi muda mrefu Sana.

Sio kazi ya mfanyakazi kufichua maovu ya ofisi anayofanyia Kazi. Hiyo sio kazi yako.
Waachie wenye kazi Yao ambao ni Sisi Raia.
Kumchomesha mwenzako Kwa Aina yoyote tena Kwa Watu wasiohusika Sisi kina Taikon tunaita ni uzuzu! Usaliti na kutojitambua.

Watanzania wengi watamshambulia Rose lakini kimsingi Rose hana kosa lolote. Tena apandishwe cheo.

SABATO NJEMA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam

Iangalie hiyo video hapo Chini bila mihemko
Anatakiwa aliwe kichwa kauza siri za kambi
 
Wewe ndio wale watetezi wa vyeti feki. Lugha ya rose shirima ni lugha mbaya haistahili majibu ya dharau na kutukana mfanyakazi mwenzie kwa kisingizio chochote.
Huyo james getogo anaweza kukutwa na kosa la kimaadili labda kama amerekodi na kusbaza hiyo video. Vinginevyo kama kuna third party anaweza akaonekana hana kosa.
Huyo rose shirima ana act unprofessional kabisa kwa nesi.
Alikuwa pushed kutoa lugha ile. Haikuja tu.
 
Shrima ameonyesha nyodo pale tuu alipomwambia "wewe nae ni mwanaume? Katika wanaume na ww upo??
 
watanzania tuna jisahau sijui ama ndo ujuvi mwingi
kwamba jamaa angepeleka ngazi za juu kwa maamuzi, sijui angesema vikao vya asubuhi daaah yaani tunasahau kabisa menejiment zetu zilivyo zimejaa mapungufu kibao wata amua nini cha maana tena unakuta wao ndio wameuza dawa zilizo kwenye muda wa matumizi na kuleta dawa/vipimo vilivyo isha muda

alafu ndio ukashtaki, hizi menejiment ambazo mkuu wa idara anamkura mfanyakazi na ww ukamshtaki hahahaha watanzania bwana.

Pia watanzania hapohapo tunashindwa kutofautisha mambo binafsi na mambo ya Kazi. MTU kuliwa sio kosa kisheria.
Ile kuleta mapenzi kazini ndio KOSA.

Sasa tuambie Kwa Muktadha wa Ile video, kosa la Rose ni lipi?
Na Kati ya Rose na James Nani amekosea zaidi?
 
Kuna kitu Cha kujifunza apa,na sijui waafrika tumerogwa na Nani,hii Ndo Hali halisi ya maisha ya huko maofsni kwa watu,binafsi sijapendezwa na majibu ya huyo nesi na pia anaonesha ualisia ulivyo hakuna heshima na hajali chochote huyo jamaa naona tu hakufata chaneli husika kufikisha ujumbe lakini walau ujumbe umefika.ukweli usemwe manesi wengi Wana shida kwenye kuwajibu wagonjwa wanawaudumia wajirekeshe na wafate taratibu za taaluma zao kwani ndicho walichogua kwenye maisha yao na kupitia hiyo kazi mungu anawabariki.Wakumbuke Kila mtu Ana nafasi yake ktk maisha ya apa duniani na hakuna kazi nzuri kuliko ulionayo.
 
Shrima ameonyesha nyodo pale tuu alipomwambia "wewe nae ni mwanaume? Katika wanaume na ww upo??

Na ndivyo ilivyokuwa inatakiwa iwe hivyo.

Kitakachofuata ataonywa, ila Watu mfano WA James Getogo majibu Yao yanapaswa yawe hivyo au makali zaidi ya hapo.

Fikiria wanaume Wawili wanamuandama Mwanamke, wanamchukua video huku wakimchokoachokoa,
Alafu vitu wanavyomuuliza hahusiki navyo, anawaambia basi waende Kwa incharge hawataki wanamuandama zaidi, unafikiri angejibuje.
 
Kwa maelezo ya rose yanathibitisha vipimo vimeisha muda wake
Wapi amekiri vimeisha mda wake? Usitumie hisia zako kwa kusikiliza huyo mshamba aliue dhamiria kijilipua kwenye video
 
Unachosema ni kizuri lakini inategemea na anayerekodi ni Nani.

MTU ukishakuwa sehemu ya taasisi Fulani unakuwa sehemu ya mfumo huo.
Unapaswa mjue namna ya kutatua matatizo ya hiyo taasisi, ndio kazi yenu hiyo mbali na kazi ya kuhudumia jamii.
Pia ina wezekana hakuna wa kufunga paka kengere so mpaka kufikia hatua ya kurekodi maana yake hatua huwa azichukuliwi hakuna nidham miongoni mwao so hiyo karma
 
Uchaga unatoka wapi mkuu hapa, twende tu na facts, JAMES AMEIVUA NGUO WIZARA NZIMA, KWANINI SHAURI ASILIPELEKE KWENYE NGAZI HUSIKA MPAKA ACHUKUWE MAVIDEO HALAFU AYARUSHE MTANDAONI, HOW FOOLISH HE IS!
Waziri kasema dawa na vifaa tiba vipo nadhani kile kituo kina uzembe wa kutofatilia so ile video ita saidia pia kwa vituo vingine kujikumbusha wajibu wao
 
Pia watanzania hapohapo tunashindwa kutofautisha mambo binafsi na mambo ya Kazi. MTU kuliwa sio kosa kisheria.
Ile kuleta mapenzi kazini ndio KOSA.

Sasa tuambie Kwa Muktadha wa Ile video, kosa la Rose ni lipi?
Na Kati ya Rose na James Nani amekosea zaidi?
mkuu ma ofisini hawana uwezo wa kutatua changamoto kuambiana jamsi alipeleke huko ni kudanganyana (japo taratibu zinataka hivyo) vipi kwetu ama ndo wale wa kutwambia subiri nimalize kula ndo nije nikusaidie ujifungue
 
Kosa ni la serekali moja kwa moja ila Rose katengenezwa awe mbaya ili apoteze kazi kwa chuki au kisasi fulani cha james.

Kama James angekua na nia njema angeenda kumrecord na incharge tuone msimamo wake, pengine ni amri ya serekali vifaa vitumike hivyohivyo sisi tutajuaje? James alitaka nini Rose afanye? Je Rose atumie mshahara wake kwenda kununua vifaa?

Kinacho onekana James anachuki fulani tu na huyo dada ila katengeneza cover ya kuonekana yeye ni mwema na huyo dada ni mbaya ila ubaya ni wa serekali siyo wa Rose.
 
Back
Top Bottom