Rose Shirima hana kosa lolote, mwenye Makosa ni James Getogo kuibua makosa ya serikali/mwajiri wake

Rose Shirima hana kosa lolote, mwenye Makosa ni James Getogo kuibua makosa ya serikali/mwajiri wake

Kwa ututez huu wa kuzunguzunguka itakua una undungu na rose ishu iko hivi robert alitaka apewe mrdt yaan vipimo vya maralia rose ndio mwenye mamlaka hayo rose akampa robert vipimo vya maralia vilivyokwisha muda wa matumiz robert akagoma kwa kulinda uhai wa wateja maana unaweza kumwambia mgonjwa huna maralia akaenda kujifia ila rose akasisitiza robert atumie vipimo hivyo hivyo vikiwa vimekwisha mda na ikibid awapime wajawazito robert akakataa ndio rose akawa mkal nakumrushia maneno ya dharau robert
Huyo Robert ni snitch, ameonekana hana hatia kwasababu amerekodi yeye hivyo asingeongea maneno makali

Lengo ni ku mprovoke mwenzake ili apate alichokitaka

Aliambiwa aende kwa incharge ila akazudi kumprovoke mwenzie

Inaonekana walikua na ugomvi wa siku nyingi
 
Msipende sana kulishwa habari za uongo.. tafuteni habari.. tizama video hii..

kwa hii video na amelezo rise yuko sahihi, huyo jamaa ni mjinga sana, na anaonekana ana bifu na huyo dada
 
Huu nao ni upumbavu...Yani watu wanakufa kwa kutumia vifaa vilivyoexpire jamaa anafichua halafu wananchi tuko upande wa kuitetea serikali???

Kweli CCM tawala milele daima Amen
 
Huyo Robert ni snitch, ameonekana hana hatia kwasababu amerekodi yeye hivyo asingeongea maneno makali

Lengo ni ku mprovoke mwenzake ili apate alichokitaka

Aliambiwa aende kwa incharge ila akazudi kumprovoke mwenzie

Inaonekana walikua na ugomvi wa siku nyingi

Muulize kama wote wangekuwa wanarekodiwa anafikiri Rose angejibu vile?

Au huyo Robert alivyokuwa anajibiwa angekuwa naye anarekodiwa alafu hajui kuwa anarekodiwa response yake ingekuwa hivyo?

Robert/James ni Snitch, mfinishaji, anaroho ya husda, na hafai Kwa kazi sio Kwa serikali tuu Bali hata sekta binafsi
 
Unajua hauelewi kilichotokea,
Mtu wa maabara kawasilisha hoja kuwa Vifaa vya MRDT Test vime-expire.
Rose kamuambia Vitumike kwa wajawazito.
James akasema hawezi kuvitumia,
Rose akasema, basi nenda Kwa incharge.
James kakataa kwenda Kwa incharge.
Rose kasema basi usitumie
James akasema vitumie wewe,
Yaani ni majibizano lakini kama vingetumika Muuguzi asingehusika na madhara kwani mhusika wa vipimo ni MTU wa maabara yaani James,

Alichofanya James ni kuibua Makosa ya serikali/mwajiri wake. Na huyo Rose hapo hiyo kesi haitamuumiza sana
vifaa havija expire bali vinakaribia ku expire mwezi wa 4, hivyo alitaka vianze kutumika kwanza hivyo,. video ukiitazama kwa mihemko utahukumu jambo lisilo sahihi
 
vifaa havija expire bali vinakaribia ku expire mwezi wa 4, hivyo alitaka vianze kutumika kwanza hivyo,. video ukiitazama kwa mihemko utahukumu jambo lisilo sahihi

Sasa Kwa nini James amefanya hivyo?
Unajua kuna mambo yanashangaza mno.
 
Hizo MRDT zina expire mwezi wa nne.. hivyo mkunga Rose alikuwa sahihi kuanza toa mzigo huo..

Mtaalamu wa Maabara amekosa weledi...amekosa Doctors'ethical conduct..amekosa maadili ya kiutumishi ..ametress pass kwenye ofisi ya mwenzake. Yani ana makosa kibaoo .

Adhabu itamuhusu
Kwahiyo mtaalam wa Maabara hana akili au hajui kusoma vizuri.
Mtaalam kasema zime expire na ndiye aliye kaa darasani miaka 3 kusomea kada yake.
Alfu afisa mtumishi anasema zita expire mwezi 4... Nani mkweli mtaalam wa maabara mwenye taaluma au Afisa utumishi?
 
Huu nao ni upumbavu...Yani watu wanakufa kwa kutumia vifaa vilivyoexpire jamaa anafichua halafu wananchi tuko upande wa kuitetea serikali???

Kweli CCM tawala milele daima Amen

Kama vifaa vime-expire Rose angetakiwa afanyeje?
Rose sio MTU wa maabara kumbuka,

Je James Getogo kama tayari anajua vifaa vime-expire hajui taratibu za kufuata ili vifaa vipya viletwee?
Kumbuka ameshaambiwa na Rose basi asivitumie kama vime-expire
 
Muulize kama wote wangekuwa wanarekodiwa anafikiri Rose angejibu vile?

Au huyo Robert alivyokuwa anajibiwa angekuwa naye anarekodiwa alafu hajui kuwa anarekodiwa response yake ingekuwa hivyo?

Robert/James ni Snitch, mfinishaji, anaroho ya husda, na hafai Kwa kazi sio Kwa serikali tuu Bali hata sekta binafsi
[emoji2]james, daah sio taikoon Robert
 
Sasa Kwa nini James amefanya hivyo?
Unajua kuna mambo yanashangaza mno.
kupishana kazini kupo, ni kawaida,ila yawezekana, rose akiwa kama msimamizi wa store ya vifaa huwa anambania james kupiga dili, hivyo anaweza kuwa na chuki na huyo bibie. kiufupi kafanya hivyo kumkomoa, kumbe anafanya ujinga
 
Kwahiyo mtaalam wa Maabara hana akili au hajui kusoma vizuri.
Mtaalam kasema zime expire na ndiye aliye kaa darasani miaka 3 kusomea kada yake.
Alfu afisa mtumishi anasema zita expire mwezi 4... Nani mkweli mtaalam wa maabara mwenye taaluma au Afisa utumishi?

Hapa kuna utata.
Ila Kwa mujibu wa mada, kosa la Rose lipo wapi?
 
kupishana kazini kupo, ni kawaida,ila yawezekana, rose akiwa kama msimamizi wa store ya vifaa huwa anambania james kupiga dili, hivyo anaweza kuwa na chuki na huyo bibie. kiufupi kafanya hivyo kumkomoa, kumbe anafanya ujinga

😂😂😂
Ntu ya Dili.

Hawa Watu wanajuana vizuri.
Ila James alichofanya ni Akili ya kijinga ambayo Kwa MTU aliyesoma asingeweza kuifanya
 
Kama vifaa vime-expire Rose angetakiwa afanyeje?
Rose sio MTU wa maabara kumbuka,

Je James Getogo kama tayari anajua vifaa vime-expire hajui taratibu za kufuata ili vifaa vipya viletwee?
Kumbuka ameshaambiwa na Rose basi asivitumie kama vime-expire
Inawezekana tupo tunabishana hata na hatujui mgawanyo wa kazi kwenye zahanati yao ukoje?

Kwanini mtaalamu wa maabara apeleke taarifa kwa rose kuwa vifaa vime expire? Rose ana majukumu gani kwenye hiyo ofsi?
Nafikri tunaweza hukumu yule au huyu bila kujua exactly aliyekuwa responsible kutokana na mgawanyo wa kazi wa siku husika kwenye kituo chao.
 
ROSE SHIRIMA HANA KOSA LOLOTE, MWENYE MAKOSA NI JAMES GETOGO KUIBUA MAKOSA YA SERIKALI/MWAJIRI WAKE

Anaandika, Robert Heriel.

Watanzania Wengi tunapenda Sana mambo ya kudandia dandia mambo. Kufuata Mkumbo. Kwenye nchi hii ni rahisi Sana kumchafua MTU na watu wakaamini na kumuona MTU Fulani ni Mbaya.

Taikon natumia Kanuni moja, ukija Kwa upole utajibiwa Kwa upole, ukija kishenzi utajibiwa kiushenzi.

Turudi kwenye mada
Kama ukiitazama Ile video inayoonyesha majibizano makali kiasi ya maafisa wa Afya WA zahanati ya Isgihimulwa Tabora ya Rose Shirima na James Getogo, bila kutumia mihemko basi utagundua Rose Shirima Hana kosa lolote.
Mwenye Makosa hapo ni James Getogo.

Zipo sababu zinazonifanya kuwa na mtazamo huo, sababu hizo ni kama ifuatavyo;

1. Mratibu wa njama na Msaliti.
Mchukua kamera ambaye bila Shaka ni James Getogo akiwa kama kinara wa kutelekeza njama hiyo Kwa lengo alilokuwa analijua yeye mwenyewe.

Ni aibu kuwa na mfanyakazi katika serikali au kampuni au hata kwenye familia kama alivyo James Getogo. Unajua ni kwanini?
Serikali inasiri nyingi, taasisi za Elimu zinamapungufu mengi Mno. Hata hapo nyumbani kwako ulipo yapo makorokoro mengi Sana. Lakini mkiwa kama wanafamilia, au wafanyakazi wa ofisi moja kazi yenu ni kujua nini chakufanya ili kukabiliana na hayo matatizo yalipo.
Lakini sio mmoja wenu kuchonga njama ili kuibua uozo wa familia, au serikali au kampuni. Huyo hafai popote pale.

James Getogo hataonekana kama shujaa Bali ataonekana kama MTU asiyetambua nini anafanya. James Getogo ni Msaliti hafai.

Video Ile ilipaswa irekodiwe na MTU wa nje asiyehusika na hiyo zahanati ndio ingekuwa na ujiko/mantiki.
Lakini kurekodiwa na MTU wa ndani hiyo ni njama. Maana ofisini MTU anaweza kukujaza alafu bila ya wewe kujua akawa anakurekodi ukaonekana wewe ndiye mbaya.

2. Makosa katika Video.
Ile video inamakosa kama ifuatavyo;

I/ video imeanzia katikati,
hatujui walianzia wapi, na mchukua video alipoona amepata alichokuwa anakikusudia akaamua aache kurekodi.

ii/ video imechukuliwa na mshtaki(ambaye ni Be. James Getogo).
Ile video ingekuwa na maana endapo mshitakiwa na mshitaki wangekuwa wanarekodiwa pasipo ya wao kujua ili kuondoa Ile dhana ya njama.
Sasa Be. James ndiye anarekodi unafikiri yeye angetumia Lugha gani kujibishana na MTU asiyejua anarekodiwa?
Au unafikiri Rose Shirima angejua anarekodiwa angeongea maneno makali?

Kumchongea Rose Shirima Kwa kumrekodi video ATI kisa katoa maneno ya shombo sio Pouwa! Hata wewe hapo ofisini kwako MTU anaweza kuja Kwa namna ya kukuchokoza na kukupa karaha mpaka ukajikuta unatoa maneno makali kumbe unarekodiwa, alafu video ikitumwa mtandaoni inarushwa kipande chenye maneno yako makali.

3. Makosa ya kimajukumu na kiwajibu.
Huyo James Getogo ashaambiwa na mfanyakazi mwenzake Aende Kwa incharge alafu anang'ang'aniza kumjaza Muuguzi wa Watu, ulitegemea Muuguzi angemchekea au kumjibu Kwa upole kama yupo Kanisani? Hata Kanisani kuna Wakati hakuna mambo ya upole.
Kifaa kama kime-expire ulitaka Muuguzi afanyeje sasa. Kosa lake ni lipi hapo? Yeye kakuambiwa ndio kime-expire lakini kinaweza kutumika, swali lililokuwa linafuata hapo lingetakiwa; je hakuna hatari yoyote Kutumia kifaa kilicho-expire? Hapo Rose angejieleza kulingana na uelewa wake na Elimu yake. Nani ajuaye kuwa huenda Rose anaelimu Fulani kuhusu vitu ku-expire na muda wake wa matumizi(hiyo ni juu yake sasa)

Alafu huyu James Getogo mpaka anaelekezwa na Rose Shirima kuwa Aende Kwa Incharge kwani yeye hajui taratibu za hiyo Zahanati?
Kumfukuza Kazi Rose Shirima haitakuwa Sawa. Na utakuwa uamuzi wa ajabu Sana.
Majukumu ya Muuguzi yanafahamika.

Matatizo ya namna hiyo maofisini yanapotokea hasa katika mahospitali kunakuwaga na vikao vya Asubuhi kujadili nini kimefanyika, changamoto na kupeana majukumu Kwa Siku Mpya.
James Getogo hakujua kuwa ishu ya vikao ili alete shauri lake kwenye vikao.

Kama huyo Rose Shirima anatabia mbovu ya kujibu Watu nyokonyoko(ambayo sio Tabia nzuri) je ilishindikana kumuweka kwenye kikao wakiwepo wakubwa wake wa kazi?
Au James Getogo alitaka kuiaminisha jamii ya kitanzania kuwa Rose Shirima anamdomo mchafu Kwa clip moja tuu iliyoanzia katikati tena aliyoirekodi yeye?
Come on! Tuache masikhara!

Sitetei Tabia ya majibu ya hovyohovyo na nyokonyoko Kutoka Kwa watumishi WA umma ila najaribu kuelezea kuwa yapo mazingira majibu ya nyokonyoko yanaweza kujitokeza accidentally.

Pia, najaribu kueleza kuwa ni Tabia Mbaya Kwa mfanyakazi au mwanafamilia kutoa nje madhaifu ya ofisi, kampuni au serikali Kwa Watu wasiohusika. Ni usaliti Mkubwa. Pia ni nje ya maadili ya Kazi.

Rose Shirima arudishwe kazini. Huyo James Getogo apewe onyo kali au akapewe semina. Ingawaje ingekuwa kwenye Ofisi binafsi basi angekuwa amefukuzwa kazi muda mrefu Sana.

Sio kazi ya mfanyakazi kufichua maovu ya ofisi anayofanyia Kazi. Hiyo sio kazi yako.
Waachie wenye kazi Yao ambao ni Sisi Raia.
Kumchomesha mwenzako Kwa Aina yoyote tena Kwa Watu wasiohusika Sisi kina Taikon tunaita ni uzuzu! Usaliti na kutojitambua.

Watanzania wengi watamshambulia Rose lakini kimsingi Rose hana kosa lolote. Tena apandishwe cheo.

SABATO NJEMA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam

Iangalie hiyo video hapo Chini bila mihemko
Umefuka Moshi wa kuni mbichi kiongozi..!!!
 
Kama vifaa vime-expire Rose angetakiwa afanyeje?
Angetakiwa asimlazimishe avitumie
Rose sio MTU wa maabara kumbuka,
ila ndiyo msimamizi wa stoo
Je James Getogo kama tayari anajua vifaa vime-expire hajui taratibu za kufuata ili vifaa vipya viletwee?
Sio kazi yake, Kazi ya Rose hiyo
Kumbuka ameshaambiwa na Rose basi asivitumie kama vime-expire
Pale kasema kwa jazba tu, kwamba basi acha upite hivi....inaonekana alikuwa anaendelea kuvitumia na ndiyo mazoea yao.

James amefichua kuwa kumbe hospitali za serikali huwa zina mazoea ya kutumia vifaa vilivyoexpire...Na kama hivyo basi inaonekana hiyo ni dalili tosha hata dawa wanazotupa huwa sometimes zimeexpire.
James is a Hero.
 
Back
Top Bottom