Rose Shirima hana kosa lolote, mwenye Makosa ni James Getogo kuibua makosa ya serikali/mwajiri wake

Rose Shirima hana kosa lolote, mwenye Makosa ni James Getogo kuibua makosa ya serikali/mwajiri wake

Robatiii. Unaongelea usiri kwenye swala la afya? Kweli? Watu wakifa uzembe ni wa nani? Kama sisi tena tunatetea makosa. Hii nchi tumevurugwa kwakweli. Akitokea mtu akapost swala la dawa Feki au dawa zilizo expire napo tena mtamuita msaliti kwa kutoa siri za serikali?
Umepata majibu ya leo?
 
Rose shirima amekwama sana, kama huna mood ya kumjibu mtu kaa kimya

James atakua amezingua (kama yeye ndiye aliyerekodi hiyo video) nje ya hapo anatakiwa apongezwe na apandishwe cheo kwa kusimamia maadili ya kazi yake

Hiyo ni Dawa ya Watu wenye Tabia za kukuchokoa chokoa kama huyo James Getogo. Hapo angetakiwa mzabe hata kibao kimoja. Ili aache SHOBO.

Yeye kama kaona kajibiwa vibaya si angeondoka, alafu afuate taratibu za kisheria.
Lakini yeye ndiye mchokozi.
 
Rose hana baya na mtu
Ila ni kama jamaa alikua na jambo lake pasono😁😁😁😁


James Getogo ni mchokozi.
Ni wale wafanyakazi ambao wanalazimisha mazoea/ukaribu.
MTU kama unaona hataki mazoea na wewe si uachane naye. Fanyeni yaliyoleta ofisin.
 
James Getogo ni mchokozi.
Ni wale wafanyakazi ambao wanalazimisha mazoea/ukaribu.
MTU kama unaona hataki mazoea na wewe si uachane naye. Fanyeni yaliyoleta ofisin.

Jemsi limeshampata la kumpata
 
Pole yake.
Iwe funzo Kwa Sisi wengine.

Hivi kijana mzima unawezaje kuwekeana majibizano na Mdada tena ofisini?
Mimi najuaga Wadada Kwa Wadada ndio wanakuwaga na ligi.

Mwanaume kurushiana maneno na mwanamke popote pale ni fedheha
Sasa huyu kavuka mipaka kaamua kurusha maneno sehemu ya kazi, officini.... sijui kama anaijua hata code of conduct ya aina ya kazi na office yake
 
Mwanaume kurushiana maneno na mwanamke popote pale ni fedheha
Sasa huyu kavuka mipaka kaamua kurusha maneno sehemu ya kazi, officini.... sijui kama anaijua hata code of conduct ya aina ya kazi na office yake

Pole yake.
 
Sasa mafisadi huwa mnawapopoa wa nini wakati wanafanya madudu ndani ya utumishi wa umma na utumishi una takiwa kuwa na siri🤣 Tanzania ina vituko

Kwa mujibu wa Ile video ukiambiwa utaje kosa la Rose linalompasa kufukuzwa kazi utalitaja Mkuu?

Lakini kosa la James Getogo lipo wazi na ni kubwa
 
Kwa mujibu wa Ile video ukiambiwa utaje kosa la Rose linalompasa kufukuzwa kazi utalitaja Mkuu?

Lakini kosa la James Getogo lipo wazi na ni kubwa
Hapo ndo alipo chomokea rose. Ila kwa swala kwamba kutumika vifaa vilivyo expire sio swala geni kwa Tanzania. Imeleta mixed message. Ilibidi hata serikali iseme inatoa onyo pia kwa wengine wasije wakatumia vifaa vilivyo expire.
 
Takribani wiki moja tangu kusambaa kwa video ya watumishi wawili wa afya wakibishana juu ya matumizi ya vipimo vilivyosadikika kuisha muda wake, Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) kimesema kimebaini kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu baina ya watumishi hao.

Kufuatia video hiyo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na Waziri wa Maendeleo ya Jinsia na Makundi Maalum, Dk Dorothy Gwajima walisema watafanya uchunguzi.

Kama hiyo haitoshi, Halmashauri ya Wilaya Uyui ilitangaza kuwasimamisha kazi muuguzi huyo aliyetajwa kwa jina la Rose Shirima na mteknolojia wa maabara aliyetajwa kwa jina la James Chuchu waliokuwa wakifanya kazi katika zahanati ya Ishilimuya Kata ya Bukumbi, ili kupisha uchunguzi.

Taarifa iliyotolewa na TANNA leo Januari 12, imesema kabla ya kuanza kurekodiwa kwa video hiyo, kulikuwepo na lugha za matusi zinazodaiwa kutolewa na James Chuchu kwa Rose Shirima hali iliyofanya muuguzi huyo naye kumjibu kwa lugha isiyo na staha bila ya kufahamu kuwa anarekodiwa.

Video hiyo ilimwonyesha Rose Shirima akishinikiza matumizi ya vipimo vya malaria vilivyoelezwa kuisha muda wake, huku Chuchu akipinga kitendo hicho.

“Hakuna vitendanishi vyovyote vilivyoisha muda wake ambavyo vilikuwa vinatumika katika kituo hicho kama ilivyokuwa inaelezwa na mtekinolojia wa maabara, isipokuwa vitendanishi vilivyopo vinakaribia kuisha muda wake yaani bado vina miezi 3 mbele.

“Hivyo alichokuwa anasimamia muuguzi kilikuwa sahihi kwa kufuata utaratibu wa mfumo wa udhibiti bidhaa lakini pia alikuwa akisimamia maamuzi ya kikao chao cha ndani,” imesema taarifa ya TANNA.

Kupitia taarifa hiyo, TANNA imelaani tukio la kurekodiwa kwa mtumishi huyo kwa kile kilichodai ndani yake kuna chembechembe za udhalilishaji wa utu na unyanyasaji wa kijinsia.
#mwananchiupdates

Screenshot_20230112-172252_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom