Rostam Aishtaki Mwanahalisi

Hii miCCM sijui haijui kama hawa mahindi na maarabu wanaurafiki wa mashaka?

Ubaguzi.... Ukabila, Udini, Umajimbo, Ukanda!! Tuwakome Mafisadi kwa ufisadi wao please! Hawa Chenge, Richmomd, Karamagi, Balali Makapa....wote ni wamatumbi kabisa, ni CCM na Wanatuua polepole kwa ufisadi wao!
 
Sasa huyu RA anashangaza kweli, Kaspian ni kampuni yake na hao Richmond wanatumia email adress ya Kaspian, hapo kweli hakuna mahusiano????
 
Sasa huyu RA anashangaza kweli, Kaspian ni kampuni yake na hao Richmond wanatumia email adress ya Kaspian, hapo kweli hakuna mahusiano????

Kama nilivyowaeleza tokea mwanzo na nauhakika hiyo ndiyo dira ya Mwanahalisi(Hakikisha unapata nakala ya Jtano) Mahakamani ndipo tutakapopata ukweli wa Mambo
 
Huku ndiko kunakopangwa na CCM ili kujaribu kuzima hoja na kuwafanya watu waogope kusema,rostam hana ubavu wa kushitaki kwani hilo ni wazo ambalo mafisadi walitakiwa wawahi mapema kuwashitaki wanaowaumbua na huku kuchelewa kupelekwa mahakamani wao mwanzo ni kuwapa nafasi ya kufanya hivyo na ndio wameanza subirini wengine ambao watafuata hifadhi ya mahakama.
 
Jamani Tusimbeze na kumdharau RA
 
Haya yalioandikwa inawezekana ni sawa lakini je Mbona kila dili anakutwa yeye?

Kila kitu anaonewa?

Wanasheria wa mwana halisi nafikiri inabidi wachukue Mabox ya mafaili yote. Kila uchafu wote hili kuonyesha huyu mtu siyo msafi. Kuanzia EPA, Kagoda stailmpaka Richie
 
Mkoloni na mwizi mwenye uraia wa utata ROstam Azizi ni shemeji ya mkuu wa kaya. Kiburi chote hiki kinapata nguvu toka somewhere.

Rostam anaweza akashinda hii case na mwanahalisi wajiandae kupigana vizuri na wasipuuzie hii case. Wale wana JF wenye nia ya kuchangia kwa hali na mali kwenye case ya mwanahalisi wafanye hivyo lakini wasishangae kama akishinda hii case.

Ukiwa unalipwa mamilioni ya dola na serikali ya Tanzania kila mwezi, unakuwa na uwezo wa kununua kila jaji hapo Tanzania na kushawishi matokeo ya case dhidi yako.

Hili jambo ni zito na muhimu sana, ni kipimo pia cha uadilifu wa Kikwete.
 
Ni vizuri sana RA amekwenda mahakamani mimi kama Mtanzania ningependa kujua ukweli wa mambo.

Tunachojua RA ni Mtuhumiwa na Kampuni ya Richmond ni Kampuni ya Mfukoni. Na kingine ni kwamba yeye ana uhusiano na Dowans ambayo ndiyo iliyoinunua Richmond.

Karamagi, Msabaha, Ex-waziri Mkuu wote wameisha sema ni Kampuni hewa. Cha kushangaza RA kama ana share na Dowans alipata wapi contact za kampuni hewa hili imuuzie Mkataba wa Richmond?

Mahakamani tu ndipo EL, Karamagi, wafanyakazi wa Wizara nk watatwambia nani ni nani.

Kama ni ya Kinara wa nchi na hilo tulijue. Nafikiri hili kwa watanzania ni kama neema. Hila pia watanzania wakikomaa vizuri bila kumtelekeza mwanahalisi, ukweli tunaoutafuta tutaupata.

Jaji sijui kuongwa ataongwa tu kama wananchi hatutakuwa makini na jinsi kesi inavyokwenda. Siku hizi watu waliowengi wanajua sheria akitokea mslaliti ajue mbele ya safari tutaulizana. Kinachotakiwa haki itendeke kwa RA na pia kwa mwanahalisi.
 
Hili jambo ni zito na muhimu sana, ni kipimo pia cha uadilifu wa Kikwete.
Mwafrika wa kike naomba kukataa kuwa hiki ndicho kipimo cha kikwete,anaweza kumtosa kuwafurahisha nyie then RA akaendelea kupeta,ndiyo staili mpya nayotumika na kuna mtu ndiye aliwashauri,na wanamtumia sana kwa sasa.

1.Angalia suala la EPA,watu wameshajulikana ila wameachwa bila kushugulikiwa,sie tumefurahi ila hakuna cha ziada.

2.Suala la BOT,Ripoti imetoka naikafanywa siri,kuna nini ndani ya hiyo ripoti ambacho watanzania wengine hawatakiwi kukifahamu.

3.Kuanguka kwa mara ya pili kwa Lowassa,Tumeshangilia,ila nini kimefanyika baada ya watu hwao kujiuzuru.

4.Suala la Buzwagi,Je ni nani keshachukuliwa hatua,na ilikuwa sawa kwa watu hao kusaini mkataba huko nje?

Mie nitapima Uadilifu wa kikwete kama akiruhusu serikali ya Umoja wa kitaifa kule Zanzibar na kumng'oa Gray Mgonja,huyu ndiye source ya haya matatizo yote.He is their Head-teacher when you talks about all dirty deals,the king of spinning in the government.na hata ushauri wa kwenda kusajili TANGOLD huko Nje ni wake,

Mama,
siko tayari tena kufungwa bao la kisigino,Je uko tayari tena!!Mwache aende mahakamani ili aje atuambie who owns RDC?
 
He is not serious since he want to show tanzanian that he is above the law. Let him ggo to the court and the whole antion to see how corrupt he is.
 
Mfa maji haachi kutapatapa, yeye anadhani watanzania ni matahira ila iko siku hawa mafisadi watatamani dunia ipasuke, subiri.
 
Kwa mara nyingine tena mnajaribu kumdanganya Kubenea kuwa unao ushahidi wa kumsaidia ktk kesi yake na mh RA.napenda kuwaambia kwanza kuwa jamaa hawezi kuwa amekurupuka kufungua kesi kwani ni wazi nae ana wanasheria wake kadhaa ambao wamemshauri vema.Najua mfuasi mwaminifu wa malecela unafuraha sana now
 
Ukisikia mimi nakuunga mkono na kukubali ukifanya vyema ES ni kwenye maswala kama haya .You have said it all .Nakupongeza kabisa na sasa huyu jamaa nadhani kalengeshwa na ndiyo mwisho wake sasa .
SASA HUKU NDIO KUMTISHIA NYAU,RA HAWEZI KULENGESHWA NA MTU,ANA AKILI YA KUTOSHA NA KWA HAKIKA ATASHINDA KESI HII.
 
Kaka acha kukaa na kuota ndoto kwanza kuwa na mawakili kibao sio ushindi katika kesi,nyie mnaishia kupiga kelele humu jf na wala hamtatoa pua zaenu mahakamani.Kennedy Fungamtama anawatosha kabisa.Na zamu ya Raiamwema imefika staytuned watoto wa walalahoi.
 
SASA HUKU NDIO KUMTISHIA NYAU,RA HAWEZI KULENGESHWA NA MTU,ANA AKILI YA KUTOSHA NA KWA HAKIKA ATASHINDA KESI HII.

Ni kweli Rostam Atashinda kesi maana yeye ni shemeji ya Kikwete na ndiye anafanya dirt job ya JK!
 
SASA HUKU NDIO KUMTISHIA NYAU,RA HAWEZI KULENGESHWA NA MTU,ANA AKILI YA KUTOSHA NA KWA HAKIKA ATASHINDA KESI HII.

Dikteta
Mie nimeona kwanza jina then nikasema kuna kazi .Kusoma comments zikatoa majibu ya mawazo yangu .Karibu kaka .Njoo slow hapa ni JF.Personalities attack hazina room hapa .Unamvaa Mzee ES kwa uhuru wake wa mawazo ? Mbona unasema Rostam ambaye unamwita Mh.Wakati sote tunamjua ni mwizi tu , atashinda na hupingwi ? Anaweza kupata wnasheria wakamwingiza mkenge ili aishe vile vile .The guy is iranian ndiyo maana hajali maisha ya Watanzania .
 
I still believe the man has every right kuwasue mwanahalisi after all hakuna chombo chochote cha sheria kilichomstaki kuwa ufisadi au rushwa

Yes i have my doubts about the man lakini i wont fall into playa hating eti nimchukie tuu kwa sababu kahusishwa na rushwa...nop, thats not how i operate. Na nikitazama media ya Tanzania, well i am not surpprised at all

Got for it Rostam huko mahakamani ndio tutajua PUMBA NI ZIPI NA MCHELE NI UPI
 
Ubaguzi.... Ukabila, Udini, Umajimbo, Ukanda!! Tuwakome Mafisadi kwa ufisadi wao please! Hawa Chenge, Richmomd, Karamagi, Balali Makapa....wote ni wamatumbi kabisa, ni CCM na Wanatuua polepole kwa ufisadi wao!

Bora useme wewe maana hapa hawana focus kabisa na wanajidai wana ushahidi kumbe ni ushabiki ambao mahakama kamwe haiwezi kudeal nao,rangi ya rostam sio ushahidi wa kesi mahakamani.
 
wacheni haki ya mungu iijiidhirishe
ni wakati wa kusali na kuomba....mama mchungaji rwakatare alipotangaza kuna watoto wa kishirikina wengi wal;ipinga na kulaani ananua watoto sasa mungu kajiidhirisha mtoto yuleyule kakutwa ankula fuvu la mtu....hivyo tuwaache hawa mafisadi wanapojaribu kucheza na nguvu za mungu wacheni mungu ajiidhirishe
hata yona alimezwa na samaki kwa manufaa ili akawaokoe watu ...so hata huyu kwenda mahakamani mapenzi ya mung kufukua mengi yaliyojifisha
mungu uinuliwe kwa hili
 
Sasa huyu RA anashangaza kweli, Kaspian ni kampuni yake na hao Richmond wanatumia email adress ya Kaspian, hapo kweli hakuna mahusiano????
Kaka acha kukurupuka richmond hawajapata kutumia email ya richmond bali ni dowans.RA ataprove kirahisi kabisa kuwa yeye hausiki a \richmond kama alivyoanza wakili Tenga wa Richmond kusema last month kuwa kampuni ipo na inawenyewe,sasa kama mwenyewe akijitokeza na KUBENEA atatoa ushahidi gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…