Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani biashara zake zina Magumashi hadi aishi kwa hofu!? hiyo hofu inasababishwa na nini!!??Rostam hofu yake ni biashara zake ndo imemfanya aombe msamaha.
Mkuu yuko sahihi sababu ni malalamiko ya wakati wote a ndo hivyo tu nchi ya waova mpaka waogaIla mfano kwa jinsi mwenendo mzima wa kesi ya Mbowe ulivyokuwa, halafu mwisho wa siku ikaonekana ana kesi ya kujibu! unaweza kusema Rostam alikuwa sahihi kwa kauli yake ya kwanza.
Mfanyabiashara, Rostam Aziz amekiangukia Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT), akiomba radhi kutokana na kauli aliyoitoa dhidi ya Mahakama nchini.
Rostam ameomba radhi saa chache baada ya JMAT kutoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari, kikimtaka mfanyabiashara huyo athibitishe tuhuma alizotoa dhidi ya Mahakama au aombe radhi hadharani.
Rostam, Juni 26, mwaka huu mbele ya waandishi wa habari alisema, "Hakuna mwekezaji atawekeza kwenye nchi ambayo kesi ikipelekwa hapo Kisutu kiongozi yoyote anaweza kupiga simu akaielekeza mahakama nini cha kufanya.”
Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Rostam alizungumzia faida za uwekezaji wa sekta binafsi katika uendeshaji wa bandari, akirejea mkataba wa ushirikiano uliosainiwa na Serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu uwekezaji na uendelezaji wa bandari nchini.
Hata hivyo, sakata hilo limeibua hisia tofauti za wananchi, wengine wakikosoa kutokana na kile wanachoeleza kuwa, baadhi ya vifungu vya mkataba huo vina kasoro na hatari kwa masilahi ya nchi.
JMAT ilitangaza kusikitishwa na kauli hiyo ikisema, "Anapaswa athibitishe kauli yake akibainisha jina la Jaji na lini alipewa maagizo na Serikali kutoa maamuzi kinyume na taratibu zilizopo. Akishindwa kutoa uthibitisho, tunamtaka atumie jukwaa lile lile kuomba radhi kwa uzito ule ule.”
Baada ya taarifa hiyo, Rostam leo Jumanne, Julai 4, 2023 amezungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, akieleza alichokizungumza siyo kusudio lake ni kuteleza kwa ulimi.
"Kwa sababu ya kutambua na kuheshimu dhima, hadhi na wajibu wa kikatiba wa Mahakama, ningependa kusema yafuatayo.
"Ningependa kuuhakikishia umma, kwamba wakati nikizungumzia uwekezaji halikuwa kusudio langu kuidharau Mahakama," amesema.
Alichokizungumza, amesema ameteleza ulimi na si kusudiolake.
"Niliteleza ulimi, maana kusudio langu lilikuwa ni kueleza kuhusu uwekezaji nchini na maana yangu ilikuwa ni kwamba, ili tupate uwekezaji nchini hatuna budi kuendana na taratibu," amesema.
MWANANCHI
Tapeli limekamatika, linajikutaga tajiri msomi, wakati ni _sh_zi mtupuMfanyabiashara, Rostam Aziz amekiangukia Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT), akiomba radhi kutokana na kauli aliyoitoa dhidi ya Mahakama nchini.
Rostam ameomba radhi saa chache baada ya JMAT kutoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari, kikimtaka mfanyabiashara huyo athibitishe tuhuma alizotoa dhidi ya Mahakama au aombe radhi hadharani.
Rostam, Juni 26, mwaka huu mbele ya waandishi wa habari alisema, "Hakuna mwekezaji atawekeza kwenye nchi ambayo kesi ikipelekwa hapo Kisutu kiongozi yoyote anaweza kupiga simu akaielekeza mahakama nini cha kufanya.”
Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Rostam alizungumzia faida za uwekezaji wa sekta binafsi katika uendeshaji wa bandari, akirejea mkataba wa ushirikiano uliosainiwa na Serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu uwekezaji na uendelezaji wa bandari nchini.
Hata hivyo, sakata hilo limeibua hisia tofauti za wananchi, wengine wakikosoa kutokana na kile wanachoeleza kuwa, baadhi ya vifungu vya mkataba huo vina kasoro na hatari kwa masilahi ya nchi.
JMAT ilitangaza kusikitishwa na kauli hiyo ikisema, "Anapaswa athibitishe kauli yake akibainisha jina la Jaji na lini alipewa maagizo na Serikali kutoa maamuzi kinyume na taratibu zilizopo. Akishindwa kutoa uthibitisho, tunamtaka atumie jukwaa lile lile kuomba radhi kwa uzito ule ule.”
Baada ya taarifa hiyo, Rostam leo Jumanne, Julai 4, 2023 amezungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, akieleza alichokizungumza siyo kusudio lake ni kuteleza kwa ulimi.
"Kwa sababu ya kutambua na kuheshimu dhima, hadhi na wajibu wa kikatiba wa Mahakama, ningependa kusema yafuatayo.
"Ningependa kuuhakikishia umma, kwamba wakati nikizungumzia uwekezaji halikuwa kusudio langu kuidharau Mahakama," amesema.
Alichokizungumza, amesema ameteleza ulimi na si kusudiolake.
"Niliteleza ulimi, maana kusudio langu lilikuwa ni kueleza kuhusu uwekezaji nchini na maana yangu ilikuwa ni kwamba, ili tupate uwekezaji nchini hatuna budi kuendana na taratibu," amesema.
MWANANCHI
Kwerikweri!! [emoji1787],MZILANKENDE VOICEKazi kweli kweli!
Ameunga tawi alilotaka kulikata bila kujua ndipo alipokaa...Tukisema mahakama zinahongwa sana na kila mmoja wetu ana ushahidi wa hilo, halafu ajabu, msemaji akose hata tukio/mfano mmoja wa kuthibitisha madai yake, kwangu naona ni jambo la ajabu sana.
Huu msamaha wa Rostam ni janja ya kuisafisha CCM, na mahakama, hapo Rostam ameamua kujichafua yeye kwa kukiri kusema uongo, na kuwasafisha CCM na mahakama.
Acheni kuidhalilisha nchi yetu. Hakuna mtu ambaye anajidharau anaweza fanikiwa kwa jambo lolote. Rushwa zipo duniani kote hata huko anakosema kuko salama ni kwakua anajua huko anaweza manipulate hao watu kwakua amebeba interests zao. Stop this none sense, we are a sovereign country na katu hatuwezi kuheshimika pasipo kujiheshimu.Ila mfano kwa jinsi mwenendo mzima wa kesi ya Mbowe ulivyokuwa, halafu mwisho wa siku ikaonekana ana kesi ya kujibu! unaweza kusema Rostam alikuwa sahihi kwa kauli yake ya kwanza.
Nilijua tu, lazima angelegea na kuomba radhi, kutoa shutuma bila kuwa na ushahidi wa kutosha wa shutuma dhidi ya wale unaowalalamikia ni udhaifu, lakini pia, tena zaidi, kama wale unaowalalamikia ni wenzako - CCM.
Sasa matokeo yake Rostam kwa sababu ya kutokuchagua cha kuzungumza, na wapi akizungumze, amejikuta ameenda kutengeneza maadui zaidi ya yule Dr. Slaa aliyemdhamiria, hapo sasa kwa msamaha wake, amejikuta amejichafua yeye mwenyewe, na kuwasafisha wachafu - CCM na mahakama zake.
Kaogopa tu mkwara, ila alichokisema ni kweli. Kwamba simu moja tu inatengeneza hukumu yenye matakwa ya mpiga simuMfanyabiashara, Rostam Aziz amekiangukia Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT), akiomba radhi kutokana na kauli aliyoitoa dhidi ya Mahakama nchini.
Rostam ameomba radhi saa chache baada ya JMAT kutoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari, kikimtaka mfanyabiashara huyo athibitishe tuhuma alizotoa dhidi ya Mahakama au aombe radhi hadharani.
Rostam, Juni 26, mwaka huu mbele ya waandishi wa habari alisema, "Hakuna mwekezaji atawekeza kwenye nchi ambayo kesi ikipelekwa hapo Kisutu kiongozi yoyote anaweza kupiga simu akaielekeza mahakama nini cha kufanya.”
Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Rostam alizungumzia faida za uwekezaji wa sekta binafsi katika uendeshaji wa bandari, akirejea mkataba wa ushirikiano uliosainiwa na Serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu uwekezaji na uendelezaji wa bandari nchini.
Hata hivyo, sakata hilo limeibua hisia tofauti za wananchi, wengine wakikosoa kutokana na kile wanachoeleza kuwa, baadhi ya vifungu vya mkataba huo vina kasoro na hatari kwa masilahi ya nchi.
JMAT ilitangaza kusikitishwa na kauli hiyo ikisema, "Anapaswa athibitishe kauli yake akibainisha jina la Jaji na lini alipewa maagizo na Serikali kutoa maamuzi kinyume na taratibu zilizopo. Akishindwa kutoa uthibitisho, tunamtaka atumie jukwaa lile lile kuomba radhi kwa uzito ule ule.”
Baada ya taarifa hiyo, Rostam leo Jumanne, Julai 4, 2023 amezungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, akieleza alichokizungumza siyo kusudio lake ni kuteleza kwa ulimi.
"Kwa sababu ya kutambua na kuheshimu dhima, hadhi na wajibu wa kikatiba wa Mahakama, ningependa kusema yafuatayo.
"Ningependa kuuhakikishia umma, kwamba wakati nikizungumzia uwekezaji halikuwa kusudio langu kuidharau Mahakama," amesema.
Alichokizungumza, amesema ameteleza ulimi na si kusudiolake.
"Niliteleza ulimi, maana kusudio langu lilikuwa ni kueleza kuhusu uwekezaji nchini na maana yangu ilikuwa ni kwamba, ili tupate uwekezaji nchini hatuna budi kuendana na taratibu," amesema.
MWANANCHI
Kama kweli kuna Jaji anae Chukua hongo ili apindishe haki za watu au ya Mtu,Basi huyo Jaji hata uwona ufalme wa Mungu!!Majaji na Hongo ni kama Uji na Mgonjwa.