Rostam Aziz awaomba radhi majaji, asema ULIMI ULITELEZA

Rostam Aziz awaomba radhi majaji, asema ULIMI ULITELEZA

Nafikiri hakuna mtu mjanja na ambaye amezicheza siasa za Tanzania Kwa ustadi mkubwa kuliko rostam Aziz, mtu Mmoja mwenye akili za mbali sana, mjanja...tafsiri ya jambo hili ni baya au zuri ni zao la mtizamo tu...watu wenye akili hufanya kama alivyofanya yeye, anawaomba msamaha then behind the scene mnampigia yeye magoti Kwa Kila kitu.
Rostam na Chenge hawa watu hawakosei kabisa.
 
Tapeli limekamatika, linajikutaga tajiri msomi, wakati ni _sh_zi mtupu

Na mate natema pthu!
hapo ulipo unatumia bundle yeye anamgao wake kupitia kampuni za Mitandao ya simu anayomiliki hisa nyingi sana

uki charge simu hapo anakula mgao kupitia umeme anaouza kupitia symbion ambayo zamani iliitwa Dowans kabla ya hapo iliitwa Richmond

sasa hivi anasambaza Gesi za kupikia

huyu Mdosi anasambaza zile necessity goods mwanzo mwisho

hapo staki kukupa breaking news ya matokeo ta zabuni ya kusambaza pembejeo za kilimo

ukiskia Serikali inaruhusu exports ya mazao ujue anacheka

ukiskia vibali vya kuruhusu mzigo fulani uingie bila ya kodi kupambana na Inflation mwenzio anaitikia Kidumu Chama Cha Mapinduzi
 
Ulimi hautelezagi hivyo,Yaani uzungumzie umuhimu wa uwekezaji halafu useme Majaji wa Kisutu wanapigiwa simu kupewa maelekezo?mbona ni mada mbili tofauti kabisa?kuteleza gani huko.

Kaogopa jamaa watamsubiria kwenye vyumba vyao vya kesi wambane mbavu,kaona isiwe shida,ila ukweli unabaki palepale tu.
hapo alokusudia na ndio ukweli

kuna watu walifungiwa Akaunti zao za kibiashara na hata walipokwenda kufungua kesi ma Register walikataa kusajili hizo kesi

kuna Mfanyabishara zama za mawe alichukua mkopo mkubwa Bank na wakati anaendelea na marejesho akaunti yake ikafungwa kwa maelekezo …Bank wakaendelea kumpa riba na penalt za kushindwa kulipa , jamaa akakimbilia kwny sheria kuweka zuio hata kufunguliwa tu kesi akazuiawa na hatimae akapoteza Nyumba ya dhamana

kuna Choko mmoja alikuwa ananizingua nikamchana sana akashtaki kimtaa Mtaa kuwa nithibitishe kuwa Yeye ni choko …nikawaambia tu njia za kuthibitisha hilo zinaweza pia zikaonekana kama namdhalilisha zaid …na kwa kufupisha mjadala naomba radhi kwa kuwa sipo tayari kuthibitisha sio kuwa ziwezi kuthibitisha
 
Kauli ya Rostam Ina harufu ya ukweli. Mission aliyokuwa nayo Magufuli, kwa mfano, Ilikuwa ni kuincontroll mahakama, na alifanikiwa to some extent. Na nadhani Hilo ndio Rostam alikuwa nalo moyoni.

All in all, since hakuwa na ushahidi beyond reasonable shadow of doubts, amefanya vizuri kujikanyaga kanyaga kuomba radhi.

Lakini kwa mazingira yale ya kipindi Cha Magufuli, uhuru wa mahakama na hata Supremacy ya Bunge, vilishawekwa rehani.
 
Huyo Rostam kaongea ukweli, ila inabidi aombe msamaha kutokana na biashara zake kuwa na makandokando mengi, hivyo anajua ni rahisi kukomolewa. Inshort mtu mchafu hawezi kusimamia ukweli maana ataingia matatizoni.

Hata hivyo hatuhitaji Rostam atuambie kuwa mahakama zetu hupewa maagizo toka nje, kwani mwenendo wa uendeshaji wao wa kesi na hukumu wanazotoa huonyesha kabisa ni msukumo kutoka nje.
 
Hataki malumbano yasiyokuwa na afya, yeye anatengeneza ajira wengine wanatafuta ajira.
 
Rostam halalamikiwi wala kutishwa, hapo nimeandika tabia zake zilizomfanya akajifunga mwenyewe, kama angekuwa anajielewa na wewe unaamini alichokisema mwanzo.

Mlitakiwa/alitakiwa kupeleka ushahidi mahakamani kwamba mahakama hazipo huru, lakini kuomba radhi maana yake Rostam amekiri alisema uongo, kwamba hana ushahidi wa kile alichokizungumza, hapo sijamtisha yeyote.

Nikwambie kitu, huu msamaha Rostam alioomba, ukiutazama kwa undani kabisa utauona una manufaa kwa CXM yake, ni kama amekisafisha chama chake kijanja bika nyie wengine kujua hilo, msimtetee mtu anayeijua dhambi, akaisema, lakini ajabu mwisho wa siku akaamua kuomba radhi kwa kuisema kwake.
Matajiri wengi Kama akina Rostam wakiwa na kesi Mahakamani huwa Wana honga sana,hasa wakiwa wao ndiyo wakosaji! Ndiyo maana hapa Tanzania tuna msemo unaosema kua "Tajiri hafungwi,na walioko Jela wengi ni masikini tu!!
 
Mfanyabiashara, Rostam Aziz amekiangukia Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT), akiomba radhi kutokana na kauli aliyoitoa dhidi ya Mahakama nchini.

Rostam ameomba radhi saa chache baada ya JMAT kutoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari, kikimtaka mfanyabiashara huyo athibitishe tuhuma alizotoa dhidi ya Mahakama au aombe radhi hadharani.

Rostam, Juni 26, mwaka huu mbele ya waandishi wa habari alisema, "Hakuna mwekezaji atawekeza kwenye nchi ambayo kesi ikipelekwa hapo Kisutu kiongozi yoyote anaweza kupiga simu akaielekeza mahakama nini cha kufanya.”

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Rostam alizungumzia faida za uwekezaji wa sekta binafsi katika uendeshaji wa bandari, akirejea mkataba wa ushirikiano uliosainiwa na Serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu uwekezaji na uendelezaji wa bandari nchini.

Hata hivyo, sakata hilo limeibua hisia tofauti za wananchi, wengine wakikosoa kutokana na kile wanachoeleza kuwa, baadhi ya vifungu vya mkataba huo vina kasoro na hatari kwa masilahi ya nchi.

JMAT ilitangaza kusikitishwa na kauli hiyo ikisema, "Anapaswa athibitishe kauli yake akibainisha jina la Jaji na lini alipewa maagizo na Serikali kutoa maamuzi kinyume na taratibu zilizopo. Akishindwa kutoa uthibitisho, tunamtaka atumie jukwaa lile lile kuomba radhi kwa uzito ule ule.”

Baada ya taarifa hiyo, Rostam leo Jumanne, Julai 4, 2023 amezungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, akieleza alichokizungumza siyo kusudio lake ni kuteleza kwa ulimi.

"Kwa sababu ya kutambua na kuheshimu dhima, hadhi na wajibu wa kikatiba wa Mahakama, ningependa kusema yafuatayo.

"Ningependa kuuhakikishia umma, kwamba wakati nikizungumzia uwekezaji halikuwa kusudio langu kuidharau Mahakama," amesema.

Alichokizungumza, amesema ameteleza ulimi na si kusudiolake.

"Niliteleza ulimi, maana kusudio langu lilikuwa ni kueleza kuhusu uwekezaji nchini na maana yangu ilikuwa ni kwamba, ili tupate uwekezaji nchini hatuna budi kuendana na taratibu," amesema.

MWANANCHI
King maker kapatikana. Naona kakubali yaishe kiungwana
 
Back
Top Bottom