Rostam na Chenge hawa watu hawakosei kabisa.Nafikiri hakuna mtu mjanja na ambaye amezicheza siasa za Tanzania Kwa ustadi mkubwa kuliko rostam Aziz, mtu Mmoja mwenye akili za mbali sana, mjanja...tafsiri ya jambo hili ni baya au zuri ni zao la mtizamo tu...watu wenye akili hufanya kama alivyofanya yeye, anawaomba msamaha then behind the scene mnampigia yeye magoti Kwa Kila kitu.
hapo ulipo unatumia bundle yeye anamgao wake kupitia kampuni za Mitandao ya simu anayomiliki hisa nyingi sanaTapeli limekamatika, linajikutaga tajiri msomi, wakati ni _sh_zi mtupu
Na mate natema pthu!
Messi na Ronaldo haoRostam na Chenge hawa watu hawakosei kabisa.
hapo alokusudia na ndio ukweliUlimi hautelezagi hivyo,Yaani uzungumzie umuhimu wa uwekezaji halafu useme Majaji wa Kisutu wanapigiwa simu kupewa maelekezo?mbona ni mada mbili tofauti kabisa?kuteleza gani huko.
Kaogopa jamaa watamsubiria kwenye vyumba vyao vya kesi wambane mbavu,kaona isiwe shida,ila ukweli unabaki palepale tu.
Ukweli mchungu.
Huyo kanjibai ni mhuni tu.
Huyo kanjibai ni mhuni tu.
Kweli kabisa dada mkubwa.kama vile wewe mlala hoi
Huwa wanachukua sana tu, na wakati mwingine hawapewi bali hupokea vitisho vya dola na kufanya kulingana na matakwa ya watawala.Kama kweli kuna Jaji anae Chukua hongo ili apindishe haki za watu au ya Mtu,Basi huyo Jaji hata uwona ufalme wa Mungu!!
Sio muungwana, bali sio msafi, na aliwaosema nao wanajua uchafu wake, hivyo walikuwa wanataka wamwage mboga maana yeye Kamwanga ugali.ROSTAM ni muungwana
Matajiri wengi Kama akina Rostam wakiwa na kesi Mahakamani huwa Wana honga sana,hasa wakiwa wao ndiyo wakosaji! Ndiyo maana hapa Tanzania tuna msemo unaosema kua "Tajiri hafungwi,na walioko Jela wengi ni masikini tu!!Rostam halalamikiwi wala kutishwa, hapo nimeandika tabia zake zilizomfanya akajifunga mwenyewe, kama angekuwa anajielewa na wewe unaamini alichokisema mwanzo.
Mlitakiwa/alitakiwa kupeleka ushahidi mahakamani kwamba mahakama hazipo huru, lakini kuomba radhi maana yake Rostam amekiri alisema uongo, kwamba hana ushahidi wa kile alichokizungumza, hapo sijamtisha yeyote.
Nikwambie kitu, huu msamaha Rostam alioomba, ukiutazama kwa undani kabisa utauona una manufaa kwa CXM yake, ni kama amekisafisha chama chake kijanja bika nyie wengine kujua hilo, msimtetee mtu anayeijua dhambi, akaisema, lakini ajabu mwisho wa siku akaamua kuomba radhi kwa kuisema kwake.
King maker kapatikana. Naona kakubali yaishe kiungwanaMfanyabiashara, Rostam Aziz amekiangukia Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT), akiomba radhi kutokana na kauli aliyoitoa dhidi ya Mahakama nchini.
Rostam ameomba radhi saa chache baada ya JMAT kutoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari, kikimtaka mfanyabiashara huyo athibitishe tuhuma alizotoa dhidi ya Mahakama au aombe radhi hadharani.
Rostam, Juni 26, mwaka huu mbele ya waandishi wa habari alisema, "Hakuna mwekezaji atawekeza kwenye nchi ambayo kesi ikipelekwa hapo Kisutu kiongozi yoyote anaweza kupiga simu akaielekeza mahakama nini cha kufanya.”
Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Rostam alizungumzia faida za uwekezaji wa sekta binafsi katika uendeshaji wa bandari, akirejea mkataba wa ushirikiano uliosainiwa na Serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu uwekezaji na uendelezaji wa bandari nchini.
Hata hivyo, sakata hilo limeibua hisia tofauti za wananchi, wengine wakikosoa kutokana na kile wanachoeleza kuwa, baadhi ya vifungu vya mkataba huo vina kasoro na hatari kwa masilahi ya nchi.
JMAT ilitangaza kusikitishwa na kauli hiyo ikisema, "Anapaswa athibitishe kauli yake akibainisha jina la Jaji na lini alipewa maagizo na Serikali kutoa maamuzi kinyume na taratibu zilizopo. Akishindwa kutoa uthibitisho, tunamtaka atumie jukwaa lile lile kuomba radhi kwa uzito ule ule.”
Baada ya taarifa hiyo, Rostam leo Jumanne, Julai 4, 2023 amezungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, akieleza alichokizungumza siyo kusudio lake ni kuteleza kwa ulimi.
"Kwa sababu ya kutambua na kuheshimu dhima, hadhi na wajibu wa kikatiba wa Mahakama, ningependa kusema yafuatayo.
"Ningependa kuuhakikishia umma, kwamba wakati nikizungumzia uwekezaji halikuwa kusudio langu kuidharau Mahakama," amesema.
Alichokizungumza, amesema ameteleza ulimi na si kusudiolake.
"Niliteleza ulimi, maana kusudio langu lilikuwa ni kueleza kuhusu uwekezaji nchini na maana yangu ilikuwa ni kwamba, ili tupate uwekezaji nchini hatuna budi kuendana na taratibu," amesema.
MWANANCHI