Rostam Aziz awaomba radhi majaji, asema ULIMI ULITELEZA

Rostam Aziz ameomba radhi kwa majaji akisema ulimi uliteleza na hakumaanisha ambacho alikisema kuhusu majaji kuhongwa. Nadhani amefanya jambo la kiungwana sana.
Kafanya "jambo la kiungwana sana", huku akishaufikisha ujumbe alionuia kuufikisha kwa wahusika.
 
Duh....nimejikuta nacheka mwenyewe!!!!!
 
Rostam ni mtu mkubwa, wa mipango mingi, hatakiwi kujihusisha na wanasiasa uchwara hawa. Nampongeza na asijihusishe tena kujibizana jibizana na watu wadogo km slaa
 
"Kama nilisema..." bado haamini kuwa alisema.

Nami naomba kuuliza swali hapa kuhusiana na hii mistari miwili inayosemekana alisema Rostam.
Hawa wawekezaji wa ndani kama yeye, na wao wanafuata na hizo "zinazo ongoza uwekezaji Duniani"?

Naona ni kama muda si mrefu, hata hawa akina Aziz wataanza kupeleka miswada (kupitia kwa serikali yao hii), ili na wao walindwe na hizo taratibu za kidunia.
Hizi Mahakama zetu na majaji wamekwishadharaulika na hawa watu.

Kama yeye anawekeza hapa katika mazingira haya, kwa nini hao wengine toka nje waone shida?

Huu ni ulaghai tu wanaotumia hawa watu kutudhalilisha.
 
Kwa hiyo na upuuzi wote aliozungumza ni kuteleza ulimi??
 
Heh heh ujumbe keshawafikishia hao waheshimiwa majaji na mahakimu, huwezi ukalinganisha majaji , mahakimu na wanasheria wetu na wale wa nchi jirani ya Kenya, hawa wasomi wetu ni wa hovyo kupitiliza, eti tuna wanasheria kama Fatuma Karuma, Tundu Lissu, Kibatalla,Mwakyembe na wengineo. Hawa huwezi kuwalinganisha na wa enzi za akina Lamwai, Mabero Marando, Ringo Tenga, Jaji Nyirabu, Warioba...
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hatariii tupuu
 
Haukumpa fidia dhidi ya udhalilishaji huo??
 
Kwahio aliteleza Ulimi ?!!! Alitaka kusema nini kama Ulimi Unsingeteleza ?!!! Kwamba mahakama zinafaa na kutenda wajibu wake kulingana na taratibu ?

Hii mimi ndio naita unafiki.... Ila ndio yaleyale Baniani Mbaya.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…