Rostam Aziz: Historia ya Dkt. Slaa haimpi uhalali wa kujifanya anajali maslahi ya Mtanzania. Kampuni zangu hazihusiki na uwekezaji wa DP World

Binafsi siwezi msikiliza Dr Mihogo na Njaa zake badala yake nitamsikoliza na kumpa attention Rostam Kwa sababu kwanza ni mlipa Kodi na Mwajiri ila huyo mwingine ni njaa zinamsumbua ni WA kupuuzwa ,ameshazeeka hana jipya Kwa umri wake..
Rostam kaongelea kuhusu ufanisi wa bandari,na amesema kama kuna maboresho kwenye mkataba yafanyike

Ova
 
Ana taka kusema walio muonga ubalozi (kama anavyo sema) hawana uadilifu pia?

Je huyo mwenye kutoa huo ubalozi ni nani?

Kama ni namba moja basi ina maana ata yeye viwanda vyake anavyo dai vilifunguliwa kwa kuwa alifanya kwa uadilifu, tuanze kujiuliza maswali kuanzia hapo?

Hizi sinema za wafanya biashara kuita press zimerejea tena!

Miqka ile ndio kulikuwa na hizi mambo, huku manji kule marehemu Mengi, huku sijui nani!
 
Na wa Dr Mihogo je? Hana moral authority kunyooshea wenzake vidole. Ameasi Kanisa,ameasi familia yake na ameasi chama chake.
Kwa hiyo mtu aliyeshindwa kuhimili genye zake akaasi kanisa na kupiga mzigo akikuambia kaona nyoka ndani ya shuka kitandani kwako utampinga na kutoamini kwa vile kaasi kanisa?
Hulka binafsi hazina nafasi katika kusema ukweli wa raslimali za taifa.
Rostam ni mwizi na mjanja mjanja tuu wa raslimali za taifa.
 

Attachments

  • jesus-christ-painting-come-follow-me-by-brent-borup-pano.jpg
    29.2 KB · Views: 3
  • 7e4102ad0c92c5950194791ec05771da.jpg
    52.1 KB · Views: 2
  • 3b0386280d5ffee5bd15771c651cb9bb64f15577.jpg
    62.7 KB · Views: 2
Nyerere, Omari Ally Juma na wengine wengi mikono ya hawa fisi inahusika sana.
Ni kweli hakuna jambo baya lolote ambalo limetokea nchi hii zama hizi na huyu jamaa hajahusika au kufahamu mpango huo.
Nashangaa watu wa aina hii huyu Mama anajihusisha nao kwa karibu.
Ni sawa na kumtunza nyoka kwenye mfuko wa koti
 
Binafsi toka apigwe na kutupiwa nje nguo zake na Josephine Mushumbusi baada ya mama kuanza kukopa kwa kutumia Jina na Cheo cha ufirst lady na jamaa kukimbia chadema. Hana uzalendo wala hawezi sema kitu nikamsikiliza. Hata ahutubie kwa kimachame huku anajichana chana au kichina ngozi za mwili wake.
Yeye sasa ni liability na sio asset tena.
 
Haya maneno yanauma sana
Na ndio ukweli wenyewe, sisi watu weusi tunaongea sana, na wengi tunatumia mdomo kama sehemu ya kupata ajira/uteuzi.
Bora tuwasikilize hawa wenye uwezo mkubwa waliofanya vitu 'tangible' vyenye uthibitisho, na wasiotaka teuzi wala ajira, kwa kuwa walishajitosheleza na wako 'level' nyingine.​
 


Tujiulize kwanini Chadema hawamsemi Rostam. Ukweli hakuna ushahidi wowote wa Rushwa na nawapongeza wapinzani kwa hili. Ndiyo uzui wa kuwa na wapinzani ambao nao wanajua biashara. Ukaribu wa Rostam na Raisi Samia hauna maana moja kwa moja kwamba ni Rushwa . Rostam anaweza kuwa mshauri wa Raisi bila kuwa mla rushwa! inawezekana kabisa. Tumekuwa na utamaduni wa kuropoka na kusingizia watu vitu bila kuwa na ushahidi. Dr Slaa kila mtu anajua ni mbinafsi na ni mimi mimi mimi kila wakati.
 
Fisadi papa limeguswa kunako lime kurupuka, kama hausiki si akae kimya tuu, kuanza kusema mwenzie sio muadilifu yeye ana audilifu gani au uzalendo gani 🤔🤔 nimechukua kahawa yangu nasubiria mafuriko ya majibu kutoka upande wa pili, uzuri wanajuana ngoja wavuane nguo
Nb: hadi sasa rosti tamu amesha pigwa 3:1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…