ndoto ya kimweri
JF-Expert Member
- Jul 14, 2021
- 413
- 979
Huyu Rostam anataka kuhamisha watu kwenye mjadala wa bandari ili wapore kilaini tumeshuka huyu alitupiga kwenye vocha feki tunakumbuka sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dkt. Slaa ni mtumishi wa Mungu na mwanasiasa mkongwe.Binafsi siwezi msikiliza Dr Mihogo na Njaa zake badala yake nitamsikoliza na kumpa attention Rostam Kwa sababu kwanza ni mlipa Kodi na Mwajiri ila huyo mwingine ni njaa zinamsumbua ni WA kupuuzwa ,ameshazeeka hana jipya Kwa umri wake...
Atajibiwa na Dr.SlaaMnataka kumjibu?,[emoji28][emoji28]
Ataweka clip wakati slaa ananunuliwa na CCM,rostam ni king maker,siyo mwenzio,mtikila Hana hamu huko kaburiniAsubirie mizinga na mabomu toka kwa Slaa. Utawekwa ukweli kuhusu maslahi yake kwa DP workd atajuta kumsema
Alimuua Mtikila?Ataweka clip wakati slaa ananunuliwa na CCM,rostam ni king maker,siyo mwenzio,mtikila Hana hamu huko kaburini
Hakumjali hata Mungu Bali nnyyegge zake akaasi upadre,hakika ni mbinafsi“Huyu ndugu yangu Dkt. Slaa sijui nimjibu nini maana historia yake haimpi heshima wala uhalali wa kujifanya ni mtu wa kujali maslahi ya Watanzania, siku zote amejijali yeye binafsi na maslahi yake binafsi.” – Mfanyabiashara Rostam Aziz
Mtikila aliongea shit kuhusu rostam,rostam akaita waandishi akionesha risiti za hela alizompa mtikila..huwezi amini mchungaji alishushuka asipate la kusemaAlimuua Mtikila?
Slaa hawezi kumwogopa Rost..tam, alimtikisa sana tu
Labda ni hiyo kumgharamia Rais kwenye kutengeneza na kuizindua Royal Tour.Duh sasa yeye Rostam anauzalendo gani?
Nani asiyejua kuwa alifanya kama rushwa apewe miradi kifisadi?Labda ni hiyo kumgharamia Rais kwenye kutengeneza na kuizindua Royal Tour.
Lazima ajitete sana kwa sababu ndiye aliyewaleta DP.Mbona kama Rostam anajitetea sana.
Kuna kitu hakiko sawa
Siyo Mturuki, ni persian wa kutoka Iran.Huyu sijui mturuki mfanyabiashara hatatushawishi kwa lolote.
Yuko kimkakati asimtaje Jpm maana anajua alichofanyiwa.
Hoja zake mfu hazinunuliki
Mfanyabiashara mkubwa nchini Rostam Aziz amezungumza na waandishi wa habari Juni 26, 2023 ambapo ameeleza mambo mbalimbali ikiwemo sakata la bandari ya Dar na kuhusika kwake kwenye uwekezaji huo mkubwa.
---
Juzi katika mdahalo pale hoteli ya Serena nilisema kuwa sihusiki na hili jambo (mkataba wa bandari) kibiashara. Ningekuwa nahusika nisingekuwa jasiri wa kuyasema yale niliyoyasema katika mdahalo ule.
Unapohusika na jambo huwezi kulijadili, na pia huwezi kuwa na uwezo au neutrality (hali ya kutofungamana na upande wowote) ya kuzungumzia jambo lenyewe, hivyo ningekaa pembeni na kuacha wengine wajadili.
Mimi kama Rostam na kampuni zangu hatuhusiki na uwekezaji au utakaokuwa uwekezaji wa kampuni ya DP WORLD.
Mimi ni mfanyabiashara na nimewekeza ndani na nje ya nchi, na nimetangaza jina la Tanzania kote duniani kwa kuwavutia wawekezaji waje kuwekeza katika nchi yetu ili tuweze kupata ajira na tuimarisha uchumi wetu.
Watu wanapiga porojo na ninawapa changamoto waende mahakamani. Mimi ninaaminiwa na benki za ndani na za nje ndiyo maana wananikopesha,” amesema na kuongeza “Rais (John) Magufuli asigefungua viwanda vyangu kama mimi sio mfanyabiashara halali.
Mimi sifanyi kazi na serikali, huwezi kusikia Rostam anaomba tenda serikalini au anauza hata sindano serikalini. Mimi ni mfanyabiashara ninayefanya biashara na sekta binafsi ndio maana huwezi kunituhumu kuwa nimetoa rushwa au nimekula rushwa. Hayo maneno (ya Dkt. Slaa) ni ya uropokaji tu na yasiyifanyiwa utafiti.
Historia ya Dkt. Slaa haimpi heshima wala uhalali wa kujifanya eti yeye ni mtu wa kujali maslahi ya Watanzania. Siku zote amejijali yeye binafsi na maslahi yake binafsi.
Dkt. Slaa aliacha kazi ya utumishi wa Mungu kanisani baada ya utovu wa maadili kwa kuona maisha yake ni bora zaidi kuliko utumishi wa Mungu. Historia yake ni historia ya kukosa uaminifu an uadilifu.
Dkt. Slaa hakujiunga upinzani kutokana na imani yake kwa sababu jina lake lilikatwa alipogombea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na sababu iliyotolewa wakati wa kukatwa jina lake ni sababu ya kukosa uadilifu alipokuwa mtumishi wa Mungu kanisani.
Huyu Bwana Dkt. Slaa anaangalia maslahi yake binafsi, hakuwa mwanachama wa CHADEMA bali alipoona jina lake limekatwa (alipogombea kupitia CCM) ndio akahamia CHADEMA
Watanzania wakumbuke kuwa, huyu mtu (Dkt. Slaa) alipokuwa CHADEMA mwaka 2015 alikisaliti chama chake wakati kukiwa kinaelekea kwenye uchaguzi, alikisaliti chama chake kwa kuhongwa, alihongwa ndipo akaasi na kukisaliti chama chake (CHADEMA). Alikaa zake pale Serena baada ya pale akapanda ndege kwenda Canada na kisha akapewa ubalozi
Kwa kifupi Dkt. Slaa hana uadilifu wala uaminifu wa kunisema, mtu ambaye hana msimamo, mbinafsi , anayeangalia maslahi yake na hajawahi kuchangia chochote katika uchumi wa nchi yetu kazi yake ni kupiga tu mdomo. Mtu wa namna hii kumjibu ni shida lakini ni lazima wakati mwingine umjibu
Historia ya Dkt . Slaa inatosha kabisa kueleza kuwa yuko tayari kupandikiza chuki na uhasama kwa ajili ya maslahi yake binafsi, kwa Kiswahili kifupi huyu jamaa (Dkt. Slaa) ni 'kizabizabina' ni fitina, mbinafsi. Na ni mtu wa kusema chochote na lolote na wakati wowote kwa maslahi yake binafsi"
Dkt. Slaa ananiita mimi fisadi, sasa mimi (Rostam) nafanya kazi na sekta binafsi wala sifanyi kazi na serikali nakuwaje fisadi, kwa hiyo nawafisadi sekta binafsi wenzangu, je watakubali nao? Sijawahi kupata skendo ya serikali na wala sijawahi kuomba ku-supply hata sindano serikalini
---
My Take
CCM na Team ya Magufuli mje na nyinyi mtujibu mlimnunua Dr. Slaa kwa bei gani